Maswali ya nyongeza ya waheshimiwa wabunge naona bora yasiwepo

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Bungeni kuna maswali ya msingi yanayoulizwa na Waheshimiwa Wabunge na majibu ya maswali haya yanajibiwa kwa maandishi yaliyofanyiwa utafiti lakini kwa maswali ya nyongeza mjibu maswali hana majibu sahihi na hii inapelekea kutoa majibu ambayo hayaridhishi.

Mimi nina ushauri kuwa majibu ya nyongeza yasiwepo Bungeni na siyo majibu sahihi na yanapoteza muda. Hata maswali ya msingi kwa asilimia kubwa hayana utekelezaji na huwa ni kuridhisha wauliza maswali. Mimi sioni faida ya kuwa na maswali na majibu Bungeni.

Kipindi hiki kifutwe na Bunge lifanye kazi zake za msingi kama kujadili bajeti na sheria mbalimbali ili kupunguza muda na posho.
 
Kwanza bunge lenyewe halitakiwi kukaa zaidi ya wiki moja
 
Back
Top Bottom