Maswali ya msingi sana

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,488
51,065
1. Hivi kwa utaratibu wa nyumba kumikumi, Ikulu nayo ina mjumbe wake?

2. Je Mtaa ambao Ikulu ipo nao una mwenyekiti wake wa serikali ya mtaa?

3. Je Rais naye anapiga kura kuchagua mwenyekiti wa serikali za mitaa?

4. Je wakazi wanaoishi ndani ya Ikulu kama mke wa Rais, mayaya na wengineo nao wanajiandikisha kwenye kuchagua viongozi wa serikali za mtaa?

5. Je Rais Magufuli amejiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa?

6. Je Rais kupokea gawio siku ya uchaguzi, haoni kuwa anaathiri zoezi la wananchi kwenda kupiga kura kwa kukaa kumuangalia yeye badala ya kwenda kupiga kura?

Na je haoni kuwa kuitisha hafla ya jambo hilo kuna watu kutokana na kuwa busy kushughulikia jambo hilo hawataweza kupata nafasi ya kushiriki zoezi la kupiga kura?
 
Naunga mkono hoja, siku ya uchuguzi kikawaida huwa hakuna shughuli nyingine yoyote zaidi ya uchaguzi na watu wakimaliza kupiga kura hutulia majumbani mwao.

Ukisikia event ya Ikulu ni saa 4:00 ujue kufika hapo ni saa 1:00 asubuhi.

Hao wakuu wote wanaopeleka gawio usikute sio wote taasisi zao zimeisha hamia Dodoma, hivyo kuwanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura.

Kati ya haki zote, the most important baada ya haki ya kuishi, no haki ya kupiga kura.

Tukubali, tukatee kwenye awamu hii tuna tatizo la consideration, there are things we are not considerate of others

Enzi za wengine, Jumapili ni siku ya mapumziko hakuna public events unless ni social or recreational, lakini pia ni siku ya ibada kwa wengine. Kufanya public events siku za ibada na kusababisha wengine kushindwa kushiriki ibada zao ni kama kujipa umuhimu zaidi ya yule anayeabudiwa!.

All and all, kwa vile na yeye anapangiwa lets excuse him and shift the blame kwa wanaompangia public events siku ya uchaguzi na siku za ibada za baadhi ya watu. Sio yeye ni wasaidizi wake.

Kitu ambacho ni most important kwa taifa lolote ni it's people, wabunge ndio wawakilishi wa people, mtu anazuia wananchi wasione live kile kitu walichowatuma wawakilishi wao, lakini sasa live ni shughuli zote za mtu mmoja!.

Tena hata ka live ka kipindi cha maswali na majibu, kukitokea shughuli ya mtu mmoja muhimu zaidi, ile live pia inakatwa tunahamia kule!. Where is the consideration for others?.
P
 
Missile of the Nation,
NDIYO.

Ikulu ina mjumbe,

Ndiyo ikulu inamwenyekiti wa mtaa,

Ndiyo rais anapiga kura na alijiandikisha Dodoma na alikuwa live,

Wote waliomo ikulu wenye umri wa kupiga kura ndiyo hujiandikisha na kupiga kura.

Hayo ya Gawio, akionekana live wengi wataenda kupiga kura maana ni one man show.
 
Pascal Mayalla, Mkuu vip unajindaa kwenda misa ya kwanza wale jamaa zetu nao si wameshahamia dodoma ndo maana mavuno mwaka huu mmezidiwa na St Joseph.
 
Pascal Mayalla, Wewe siku hizi hata ukisema mazuri sikuamini, anyway umeongea jambo la maana ingawa unajaribu kukwepesha anayestahili lawama asilaumiwe.

Hivi unadhani hatujui kwamba Rais wako hujipangia haya matukio na akipangiwa ana uwezo wa kukataa au kukubali? Kama yeye siyo sehemu ya haramu kwa nini anashiriki?
 
Naunga mkono hoja, siku ya uchuguzi kikawaida huwa hakuna shughuli nyingine yoyote zaidi ya uchaguzi na watu wakimaliza kupiga kura hutulia majumbani mwao.

Ukisikia event ya Ikulu ni saa 4:00 ujue kufika hapo ni saa 1:00 asubuhi.

Hao wakuu wote wanaopeleka gawio usikute sio wote taasisi zao zimeisha hamia Dodoma, hivyo kuwanyima haki yao ya msingi ya kupiga kura.

Kati ya haki zote, the most important baada ya haki ya kuishi, no haki ya kupiga kura.

Tukubali, tukatee kwenye awamu hii tuna tatizo la consideration, there are things we are not considerate of others

Enzi za wengine, Jumapili ni siku ya mapumziko hakuna public events unless ni social or recreational, lakini pia ni siku ya ibada kwa wengine. Kufanya public events siku za ibada na kusababisha wengine kushindwa kushiriki ibada zao ni kama kujipa umuhimu zaidi ya yule anayeabudiwa!.

All and all, kwa vile na yeye anapangiwa lets excuse him and shift the blame kwa wanaompangia public events siku ya uchaguzi na siku za ibada za baadhi ya watu. Sio yeye ni wasaidizi wake.

Kitu ambacho ni most important kwa taifa lolote ni it's people, wabunge ndio wawakilishi wa people, mtu anazuia wananchi wasione live kile kitu walichowatuma wawakilishi wao, lakini sasa live ni shughuli zote za mtu mmoja!.

Tena hata ka live ka kipindi cha maswali na majibu, kukitokea shughuli ya mtu mmoja muhimu zaidi, ile live pia inakatwa tunahamia kule!. Where is the consideration for others?.
P

Paschal umeongea jambo la maana
Rais anajifikiria yeye tu hafikirii wengine
Leo ni siku ya uchaguzi, kitendo cha kuchanganya ratiba ya uchaguzi na mambo mengine ya kikazi ni distraction kubwa kwa zoezi la uchaguzi

Lakini leo siyo siku ya kazi, pia ni siku ya ibada kwa watu wengi, Kitendo cha kuwadrag watu kwenye siku yao ya mapumziko wakafanye kazi siyo tu ni kuingilia haki yao ya kupumzika lakini pia ni kuwanyima utulivu wa akili na muda wa kwenda kufanya ibada.

IKULU iache kudhani kuwa raisi ndo mtu mwenye umuhimu pekee katika nchi hii, kila mtu ana umuhimu wake.
 
Back
Top Bottom