Maswali ya kuuliza Wizara ya Viwanda na Biashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali ya kuuliza Wizara ya Viwanda na Biashara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FJM, Aug 10, 2011.

 1. F

  FJM JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa walio Dodoma au wenye access na wachangiaji wa mjadala wa Wizara wa Viwanda na Biashara sasa hivi Dodoma naomba niwasilishe yafuatayo:

  1: Brela
  Kuna tatizo kubwa sana pale Brela. Kufanya Company name search peke yake inachukuwa SIKU TATU! na kwa kila jina unalipia Tshs 15,000/=

  Sielewi ni kwa nini leo hii 2011 ku-search jina inachukuwa siku tatu? this should take note less than 3 seconds. Ukiangalia kwenye website ya Brela kuna section wana-name search na ukijaribu kutumia hii option mara nyingi unapata response kuwa jina bado halijachukuliwa, lakini ukienda kule Brela wanakuambia jina tayari limeshachukuliwa. Nilipouliza wakasema bado hawajaweka information zote online! hii ni zaidi ya mwaka sasa nafuatilia, lakini bado majibu ni yale yale kuwa details bado hazijawekwa online. Kwa nini Brela wasiweke details zote online, mtu unafanya name search, application, then una-print form zako unaenda kulipia Brela?. Huu 'UJIMA' mpaka lini. Tutashindana vipi na nchi nyingine kibiasha kama hata vitu vidogo kama name search inachukuwa siku tatu?

  Tanzania tunazidi kushuka katika list ya cost of doing business na katika vitu ambavyo vimekuwa vinatajwa sana ni mfumo mbaya wa kuanzisha biashara, sheria zilizopindapinda kwenye mambo ya kodi n.k

  2. Form za kuhamisha share (share transfer)
  Kuna kituko kwenye hili. Ukitaka kupata hizi form za kuhamisha shares (e.g unamuuzia mtu mwingine shares) unaenda kununua hizi form 'HASSAN PRINTERS'!!! Sio TRA au Brela- ni HASSANA PINTERS! Hii ni aibu kupindukia. Kwa nini wasiweke kwenye website either za TRA au Brela then unajaza form zako wakati wa ku-submit ndio unalipia. Huu usumbufu wa kuzunguka mjini unatafuta Hassan Printers iko wapi mwaka huu wa 2011 ni wa nini?
   
Loading...