Maswali ya kumuuliza Mungu (Muendelezo: uwiano katika Maisha!

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
686
589
Wanasheria wenyewe wanasema 'equal treatment before the law' - utawala wa sheria.
Lakini hata katika baadhi ya maandiko ya kidini yanasisitiza kwamba 'Wanadamu wote ni sawa mbele za Mungu'.

Lakini Je huu usawa unatoka wap? Je kuna uwiano sawa wa maisha baina ya watu? Je wote wako sawa katika mienendo yao ya maisha? Na kama hakuna uwiano na Mungu ni wa wote inakuwaje wengine ni matajiri wengine maskini? Hivi ni kweli kwamba hawa matajiri wanamuomba Mungu kuliko maskini? Wengine husema ni jitihada na pia vitabu vya maandiko vinasema 'asiyefanya kazi na asile' ikimaanishajitihada katika kazi, lakini ukiangalia kwa upana unaona watu wanajibidisha sana wengine hufanya kazi ngumu zaidi ya wale matajiri au wenye pesa nyingi sasa hapa yamaanisha jitihada nazo si suluhisho? Je ni kweli Mungu hataki kuwamiminia mibaraka na hawa wadogo wenye maisha duni nao wapate wawe kama matajiri? kiujumla swali kubwa ni 'kwa nini Mungu aruhusu utofauti huu katika maisha ukizingatia katuumba yeye na sisi ni wake' 'kwa nini akubali utofauti huu?

Kwa utofauti huo wa maisha inaweza kufika sehemu na kuanza ku-doubt uwepo wa Allah, na doubt inaweza kuwakwa maskini na tajiri. Nahii ni moja ya changamoto katika imani.
Kinachoondoa tofauti hiyo ni kifo tu lakini jambo kubwa ni kwa nini aruhusu tofauti hizi katika maisha?
 
Panua hii teolojia yako ya 'makosa ya Mungu' uanzishe jumuiya/kanisa lako la'TUMJUE MUNGU KWA UNDANI'
Utapata wafuasi/wanachama wengi tu!
 
Wanasheria wenyewe wanasema 'equal treatment before the law' - utawala wa sheria.
Lakini hata katika baadhi ya maandiko ya kidini yanasisitiza kwamba 'Wanadamu wote ni sawa mbele za Mungu'.

Lakini Je huu usawa unatoka wap? Je kuna uwiano sawa wa maisha baina ya watu? Je wote wako sawa katika mienendo yao ya maisha? Na kama hakuna uwiano na Mungu ni wa wote inakuwaje wengine ni matajiri wengine maskini? Hivi ni kweli kwamba hawa matajiri wanamuomba Mungu kuliko maskini? Wengine husema ni jitihada na pia vitabu vya maandiko vinasema 'asiyefanya kazi na asile' ikimaanishajitihada katika kazi, lakini ukiangalia kwa upana unaona watu wanajibidisha sana wengine hufanya kazi ngumu zaidi ya wale matajiri au wenye pesa nyingi sasa hapa yamaanisha jitihada nazo si suluhisho? Je ni kweli Mungu hataki kuwamiminia mibaraka na hawa wadogo wenye maisha duni nao wapate wawe kama matajiri? kiujumla swali kubwa ni 'kwa nini Mungu aruhusu utofauti huu katika maisha ukizingatia katuumba yeye na sisi ni wake' 'kwa nini akubali utofauti huu?

Kwa utofauti huo wa maisha inaweza kufika sehemu na kuanza ku-doubt uwepo wa Allah, na doubt inaweza kuwakwa maskini na tajiri. Nahii ni moja ya changamoto katika imani.
Kinachoondoa tofauti hiyo ni kifo tu lakini jambo kubwa ni kwa nini aruhusu tofauti hizi katika maisha?
Ikiwa huwezi kumpangia binaadamu mwenzako jinsi ya kutumia Mali zake je,itawezekana vp kwa Mungu kutaka kumpangia cha kufanya au kumkosoa?
 
Ameshatuita wana wake kwa nini atupe utofauti na sisi wote kwake ni sawa? hatumpangii lakini kwa nini afanye hivyo na huku ni Mungu wa haki!!
 
Eeh kwan kuna watu hawapumui au wajazaliwa au hawali au hawafi au hawaendi choo sasa huo ndio usawa..kama mvua inavyo nyesha kwa mapenzi ya muumba tena bila kuzingatia sijui nani anamkashifu Mungu asipate ama apate..ndio jinsi anavyo tu treat equally..mengine ni jitihada na akili ya mtu binafsi..kwani wote walizaliwa uchi lkn wengine wakamiliki utajiri lukuki lkn wataondoka uchi
Piga kazi kwa bidii sali saana..ndio kazi uliyo itiwa hapa duniani..hata matajiri walianza kama maskini tatizo tumetofautiana nidham ya pesa..
 
Ameshatuita wana wake kwa nini atupe utofauti na sisi wote kwake ni sawa? hatumpangii lakini kwa nini afanye hivyo na huku ni Mungu wa haki!!
Sasa kama haumpangii kwanini uhoji maamuzi yake? unafikiri ni haki ya nani amevunja kwa kufanya hivi afanyavyo?
 
Back
Top Bottom