Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na drama za ndugu zetu Kenya, Rwanda na Zambia kufunga mipaka tuliyochorewa na wakoloni bila kujali hapo mwanzo sote tulikuwa ndugu. Katika hili tujiulize yafuatayo:-
1. Karibu asilimia tisini ya Madereva wa Tanzania wanaopimwa mpakani wanakutwa positive na wengi wapo hapo mpakani zaidi ya wiki mbili kusubiri hivyo vipimo. Mbona hatuletewi maiti zao? Mbona hakuna wanaoletwa na ambulance kwa kuzidiwa?
Kwanini nauliza hivyo?
Tukumbuke mpakani pale hakuna huduma nzuri, hakuna huduma za afya, chakula cha shida. Kwa mazingira hayo si rahisi mgonjwa wa Corona kuhimili kwa zaidi ya siku 14 bila kuzidiwa kwa kadiri tunavyoelezwa
2. Inaelezwa Raia na Madereva wao wanaotokea Tanzania, kwa karibu asilimia tisini wanapopimwa mpakani ili kuruhusiwa kuingia kwao vipimo huonyesha negative
Je, Ugonjwa huu unawabagua wageni? Unawashambulia wa Tanzania pekee?
Ki ukweli kwa trend inavyoendelea hakika kuna watu wataumbuka. Hadi mwishoni mwa mwezi huu wa tano na mwanzoni mwa mwezi wa sita lazima ama watanzania tuumbuke kwa kiburi chetu ama wenzetu waumbuke kwa kutaka kuleta Sanaa ndani ya jumba la Corona!
Muda siko zote ndo msema ukweli wa kweli.
Sent using Jamii Forums mobile app