Maswali ya Kujiuliza Juu ya Kauli ya Mama Diamond juu ya Baba Diamond

Tatizo lipo ..
Mwanamke shule Hana
Probably mchawi/mshirikina
Obviously alikuwa mcharuko..
Now kapata mtoto superstar..

Wanajamii wanaingizwa kwenye total confusion
Background ya yule mama kama ulivyosema alikuwa mchrk,mswahili sana,pia kaishi thug life sana
Sema tu pesa imekosea njiaaa
Alipopata tu anataka kuishi kwa kukomoa watu na kulipiza fulani
Ila yule mama lazima atambue jamii inamjuaa
Tokea kitambo ila wanamuangalia tu

Ova
 
1. Mama Diamond anasema kuwa, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamond, inakuaje tena (yeye huyo huyo) aseme kwamba, mzee Abdul aliikataa mimba? Alikataaje kitu (mimba) ambacho si chake? Na kama ni kweli ALIIKATAA, maana yake ni kwamba, basi mama Diamond alitaka kumpa hiyo mimba.
Kwanini alitaka kumpa kitu (mimba) ambacho siyo chake? Kwa lugha rahisi alitaka KUMBAMBIKIA). Je, kosa la mzee Abdul ni kukataa kubambikwa?


2. Mama Diamond amesema kwamba, mzee Abdul hakuwa baba mzazi wa Diamond—alikuwa ni baba mlezi tu. Pia, yeye huyo huyo akasema tena kuwa, mzee Abdul aliahidi kumlea Diamond lakini HAKUMLEA (rudia hilo neno—HAKUMLEA). Na hata yeye (mama Diamond) hakuwahi kuishi kwa mzee Abdul—na hata picha walizoonekana wakiwa pamoja (kipindi Diamond akiwa mtoto), ilikuwa tu wamepita kumsalimia mzee Abdul hapo Magomeni alipokuwa akiishi.
Je, mtu ambaye umesema hakuwa baba mzazi wa mtoto, na umesisitiza kuwa HAKUMLEA, hicho cheo cha "BABA MLEZI" kilitoka wapi? Alikuwa analea nini?

3. Mama Diamond amesema, mzee Abdul alikataa mimba (ubaya), lakini pia amesema, hakuwa akihudumia kama alivyoahidi (ubaya), pia amesisitiza kuwa, mimba haikuwa yake (ubaya). Kwa lugha rahisi, mama Diamond ameamua kumpaka UBAYA mzee Abdul.
Kama hayo ni kweli, je, hizo pesa ambazo mama Diamond alikuwa anapewa mara kwa mara na Diamond ili akampatie mzee Abdul zilikuwa zinakwenda kwa mzee Abdul kama nani? (Maana mtoto hakumzaa yeye, na wala hakumlea).

4. Mama Diamond amesema, alimpa Diamond ubini wa Abdul kwa sababu (mzee) Abdul ndiye aliyempeleka hospitali kujifungua. Pamoja na hayo, amesisitiza kuwa bwana Salum Nyange (anayemtaja kuwa ndiye baba mzazi wa Diamond), alikuwa anakwenda Tandale kumangalia mtoto (Diamond) kama kawaida. Maana yake ni kwamba, mzee Salum Nyange hakumkataa mtoto. Swali: Inawezekanaje mtu yule yule (mzee Abdul) aliyetaka kubambikwa mimba akaikataa, ndiye akasimama kidete kumpeleka mama Diamond hospitali?
Kama mwenye mimba (Salum Nyange) alikuwepo na hakukataa mimba, ilikuwaje mama Diamond ampe mtoto (Diamond) u-bini wa mtu mwingine (mzee Abdul) kisa tu alimpeleka hospitali kujifungua? Je, ilikuwaje mzee Abdul akaahidi KUMLEA Diamond ilhali baba mzazi wa Diamond (bwana Salum Nyange) alikuwa hai na alikuwa anakwenda kumwangalia mtoto?
You are such a great thinker....mama amejichanganya sana.
 
Back
Top Bottom