#COVID19 Naomba kupewa majibu ya Maswali haya yahusuyo COVID-19

Rohombaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
13,055
10,339
Dah! Mnisamehe tu

1. Kama COVI-19 inaambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwa njia ya vitone vidogo vya majimaji vinavyotokana na kupiga chafya, kukohoa au kuongea naye. Kwanini marehemu anayedhaniwa alikufa kwa covid19 anaogopewa zaidi ya mtu aliyehai na hajapimwa?

2. Watu wawili, wanaishi, wanakula, wanalala pamoja. Iweje muwaambie wajitenge mita 2 wakiwa kwenye vyombo vya usafiri au nyumba za ibada?

3. Kupima watu ndiyo sifa ya kwanza ya upambanaji wa COVID19. Afrika Kusini inayosifiwa barani Afrika imeweka lengo la vipimo 25,000 kwa siku, kwa idadi yao ya karibu 60m bila kumrudia mtu itachukua miaka 7 hivi kupima watu wote. Hapa sijaelewa

4. Tunawapima watu badala ya kuwachukua wale wasioambukizwa na kuwaweka sehemu salama. Sisi tunawachukua wale wagonjwa na kuwahifadhi huku tukiwaacha wale wazima warudi kwenye jamii ambayo haijapimwa ambapo wanaweza kupata hatari ya kuambukizwa.

Hapa naomba kufafanuliwa wakuu

Msinichoke kuuliza ujinga

Sent using Beretta ARX 160
 
Ndiyo maana mapema sana tuliambiwa tuombe kwa imani zetu, kama haikueleweka majibu ndiyo yamo kwenye maswali yako.

In short tumtegemee zaidi Mungu.
 
Upo sahihi.Njia ya muafaka ya kudhibiti COVID-19 ni kupima na kuwatenga wenye ugonjwa.South Korea wamefanikiwa sana kwa mkakati huu
 
Mimi mwenyewe nina swali la kijinga hapa, hivi sie Tanzania tuna uhakika gani kwamba corona haikuwepo Tz kabla ya yule mdada wa Arusha?
 
Mkuu sina jibu, ya maswali yako ila serikali napendekeza ipige lock dowm mabaa na pubic transport tuanze tumia baiskel au boda boda.maana juzi nilipanda dala dala jamaa karibu akawa anapiga chafya kama zote nilipata tabu sana.
 
Mkuu sina jibu,ya maswali yako ila serikali napendekeza ipige lock dowm mabaa na pubic transport tuanze tumia baiskel au boda boda.maana juzi nilipanda dala dala jamaa karibu akawa anapiga chafya kama zote nilipata tabu sana
Sio lazima serikali waamue kufanya hivyo, hilo lipo ndani ya uwezo wako ,fanya, haujakatazwa.
 
Kwa nini unaanza kwa kujihukumu kwamba unauliza "maswali ya kijinga"? Nionavyo mimi kama mtu amefariki dunia kwa Covid-19 uwezekano wa mtu asiye na virusi kuambukizwa upo na kuzuia au kufanya maziko kwa "namna ya pekee" kunalenga pia kuzuia au kupunguza maambukizi ya Covid-19. Kumbuka kwenye maziko huwa wafiwa huwa wako kwenye majonzi na wanaweza wasitilie maanani sana ushauri wa kiafya kutokana na uchungu walionao kwa wakati huo wa kumpoteza mpendwa wao.

Sisi wanadamu tuko 'limited'. Mfano, ukienda hospitali na mtoto asiye mgonjwa, unakatazwa kuingia naye wodini, lakini akiugua analazwa wodini. Ina maana kwamba mtoto ambaye si mgonjwa akiwa wodini anaweza kupata au kuambukizwa ugonjwa na akishaambukizwa kuna kulazwa ambako hakuepukiki.

Zuio la kiafya linalotolewa huwa linalengo kuzuia au kupunguza maambukizi ambayo mtu anaweza kupata. Mfano, mchana mtu anakutakana na watu mbalimbali na anaweza akagusa maeneo mbalimbali pia yenye maambukizi. Lakini wakati wa kulala 'assumption' ni kwamba mume na mke wana uhakika kwamba hakuna aliyekwisha ambukizwa kati yao. Kama yupo, basi ni vizuri kujitenga na wanafamilia wengine kwa lengo lilelile la kuzuia au kupunguza maambukizi.

Linapotokea janga kama hili, kila nchi inachukua hatua za dharura kulingana na uzito wa janga lenyewe. Hata kama kuna utaratibu wa kupima watu ni hatua mojawapo ambayo nchi husika imechukua. Inawezekana baada ya muda, utaratibu huo unaweza kubadilishwa au kuendelea nao kulingana na uwezekano na mahitaji ya nchi husika.

Ni rahisi kuwatenga walioambukizwa kwa vile ni wachache (na baadhi yao wanapona) kuliko kuwatenga wale ambao hawajapimwa na kupatikana na virusi. Huu ni utaratibu wa kawaida sana.
 
Hiyo no 4 sasa sijui huwa wanacheza mchezo gani hapo
Ni mchezo wa kitoto wa "kajifiche" usio na sheria. Wengine huonekana (hawakujificha inavyostahili) na wengine hupiga kelele "hunipati nimejificha", hahahahaaaa!

Wabunge wa CHADEMA wakajifungia, ati kujihakikishia wako salama ya maambukizi. Baada ya kifungo chao, cha kulazimishwa na Kamanda wa makanda wao, wakarudi Bungeni kushiriki shughuli za bunge na wabunge ambao hawajapimwa. Nani mjanja?
 
Ni mchezo wa kitoto wa "kajifiche" usio na sheria. Wengine huonekana (hawakujificha inavyostahili) na wengine hupiga kelele "hunipati nimejificha", hahahahaaaa!

Wabunge wa CHADEMA wakajifungia, ati kujihakikishia wako salama ya maambukizi. Baada ya kifungo chao, cha kulazimishwa na Kamanda wa makanda wao, wakarudi Bungeni kushiriki shughuli za bunge na wabunge ambao hawajapimwa. Nani mjanja?
Hapo ndo utajua kuwa wenda wazim niwengi duniani
 
Dah...Bado naendelea kuuliza..msinichoke..
Kama lengo la chanjo yoyote...ni kuulinda mwili usipatwe na maambukizi..... pamoja na kuutokomeza ugonjwa wenyewe...
Sasa...
Ukichanja chanjo ya uviko unaambukizwa.......
Ukichanja chanjo ya uviko unasambaza...na bado unatakiwa uendelee na kutojichanganya kwenye mikusanyiko na bado uendelee kuvaa barakoa.......
Bado sielewi .... :cool:
 
Back
Top Bottom