maswali ya kijinga, majibu ya kukatisha tamaa

toghocho

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
1,172
198
hey wana jf; kuna watu wanauliza maswali ambayo ni ya kizushi, dawa yao kuwajibu dry, kama hivi

(kwenye foleni mwisho)
S:we ndo wa mwisho kwenye line?
J: hapana mi ni wa kwanza tumesimama kinyumenyume

(kwenye basi mama amebeba mtoto)
S: mtoto wangu mzuri ee?
J: huyo ni mtoto?

(kwenye daladala, class, hotelini,cafe na maeneo kama hayo-siti iko wazi)
S:Kuna mtu hapa?
J: yeah, kuna mzimu wa bibi yako.


ongezea na maswali na majibu ya namna hiyo...
 
Nimeishia kucheka tu hata kuongezea sina hamu. Nimecheka sana lol! Hii safi sana mkuu
 
162_3.jpg k
 
(asubuhi)
S: umelalaje?
J: kifudifudi.

(mama akimwambia mtoto)
mama: unataka kulia eeh?
jirani: amechoka kushoto?!

(kwenye interview)
S: una mpango wa kuendelea na kazi mumeo akitoka masomoni?
J: hapana, nilienda kusomea digrii ya engineering ili nikae nyumbani kupika maandazi!

(kwenye interview)
S: utajionaje miaka mitano kutoka sasa
J: kwenye kioo kama ninavyojiona sasa na nilivyokuwa najiona kila siku
 
WIFE : You tell a man
something, it goes in
one ear and comes out
of the other.
HUSBAND : You tell a
woman something: It
goes in both ears and
comes out of the mouth.
 
Searching...100%
Loading...100%
Network Connected !

Kwenye bus toka Mbeya kwenda Dar
S. Kwan nawe kaka unaelekea Dar ?
J. Hapana naelekea Zambia ?
 
kwenye daladala,nimechelewa kushuka kituoni,abiria mmoja akajifanya kununua kesi, ananiuliza mbona umechelewa ulikuwa umelala nn?
nikamjibu NILIKUWA NAOGA,watu walicheka mpaka basi
 
Chumbani tulikuwa na jamaaa yangu tunapiga zetu story mda ukafika wa kuondoka, basi nikamwuliza ndiyo unaondoka, sikilizia jibu alilotoa akasema NO.. Ndo naingia....
 
kwenye daladala,nimechelewa kushuka kituoni,abiria mmoja akajifanya kununua kesi, ananiuliza mbona umechelewa ulikuwa umelala nn?
nikamjibu NILIKUWA NAOGA,watu walicheka mpaka basi
HII nimeipenda mkuu, ya kuoga kwenye daladala!!!
 
Back
Top Bottom