Maswali ya Dr. Slaa 2015, Matokeo yametoka March 1, 2018.

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,202
12,898
Dr. Slaa aliwauliza wenzie ndani ya kamati huyu anayekuja ni Asset au Liability? Lakini Dr. Slaa aliambulia matusi na kupakaziwa propaganda kuwa alifungiwa na mkewe ndani..! jamani...!

Chadema hamkutendea haki Dr. Slaa, Kiukweli mulimdhalilisha sana kumuambia ameungiwa na mkewe ili asije huku mulimfedhehesha sana sana tena sana lakini leo hii naamini munaona bora mungebaki na Dr wenu maana ata aliyeshika kiti chake pale hapamtoshi, Namkunukuu Julius Mtatiro " Mzee wa Mahaba! Karibu nyumbani, vijana tuliokulia upinzani tulikimbia huko bila kukushirikisha, kulitushinda! .
.
Si kwamba tulishindwa kupigania ajenda za huko, lakini tulizungukwa na wanafiki, waongo, madikteta, walioweka vyama mifukoni na wenye kutafuta fedha kuliko wanachokiita "ukombozi", mbaya zaidi watu hao ndio wenye mamlaka makubwa ya maamuzi!. .
.
Wakati watanzania wachache wanashangaa kurudi kwako nyumbani, mimi nawashangaa watanzania hao kwa kutojiuliza vizuri kwa nini watu kama mimi tuliokulia upinzani tulijiridhisha pasi na shaka kuwa tunapoteza muda wetu kwenye siasa za "upinzani".
.
.
Najua wako baadhi ya "makamanda" watakuja hapa kusema kuwa hata nani akiondoka upinzani wao wataendelea kuujenga. Nawakumbusha makamanda hao kuwa "upinzani imara utajengwa na viongozi wenye mamlaka ya juu ambao ni wema, wakweli, waadilifu, wenye kusikiliza wenzao na kuamulia masuala vikaoni, wenye kuamini katika ukombozi bila kupata pesa". .
.
Nimekaa upinzani huko miaka 10, viongozi wenye sifa hizi wapo wachache, kwa bahati mbaya hawana mamlaka kwenye vyama, wanapigwa vita usiku na mchana huko huko. Nadhani baada ya miaka 50 hivi upinzani ukiwapa nafasi watu hao (sisi tutakuwa marehemu), ndipo nchi itaanza kuwa na upinzani imara. .
.
Kwa sasa nataka niwaeleze wazi, kuwa upinzani wa Tanzania unadhoofishwa mno, na unadhoofishwa na hao hao waliopewa dhamana ya kuuimarisha, ukiwa nje unaweza kudhani kuwa upinzani unashambuliwa na CCM zaidi, lakini ukiwa mzoefu kama mimi utasema upinzani unajishambulia wenyewe kwa asilimia 70, unashambuliwa na CCM kwa asilimia 30. .
.
CCM inaendelea kuwa chama imara, chama chenye nguvu kubwa, maono ya nchi. Ukitafuta chama mbadala kwa CCM utaitaja CCM yenyewe. Mimi niliona, ni bora niijenge CCM na Tanzania, na naendelea kutumia nguvu kubwa sana kuijenga CCM na kuwasaidia niliowakuta kuifanya izidi kuwa imara. It was a GOLDEN decision!
.
.
Najua mmekuwa mkinitafutia uteuzi kwelikweli, hamnijui! Nataka kuwaambia, niacheni niijenge CCM kwanza, mimi ni mwanasiasa mzoefu, kijana....nina visheni kubwa kwa nchi yangu kuliko uteuzi. Niacheni nichape kazi. Karibu nyumbani mzee Edward Lowassa.
.
.
MtatiroJ"


Nasisitizia kuwa moja nyenzo muhimu ndani ya chadema na mtu aliyekuwa ana nia ya dhati kulijenga taifa hili alikuwa Dr. Slaa lakini alitusiwa, alidhalilishwa sasa mutapambana na hali zenu maana nilichogundua yule Dude wa Bongo Dar es Salaam yuko Chadema na Mzee wa watu mumempiga teyari nasasa tusubiri propaganda mutakazo tulisha.
1551477563598.png
 
Huyu Jamaa anajitahidi sana sema teuzi zinampita kushoto kama dr bana, alihadiwa jimbo la Segerea 2020 na wana Segerea angekuwa mvumilivu,asubiri 2020 ndio atajua kuwa kwake ccm ni asset au liability.
 
Najua mmekuwa mkinitafutia uteuzi kwelikweli, hamnijui! Nataka kuwaambia, niacheni niijenge CCM kwanza, mimi ni mwanasiasa mzoefu, kijana....nina visheni kubwa kwa nchi yangu kuliko uteuzi. Niacheni nichape kazi. Karibu nyumbani mzee Edward Lowassa.
Haha naona anakumbushia teuzi kwa Wanasiasa tu ndiyo watamuelewa.. Eti Kijana haha 😂
 
Sababu kuu iliyopelekea Dr. Slaa kujiondoa CHADEMA ulikuwa ni ujio wa Edward Lowassa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Dr. Slaa alikaririwa akisema kwamba asingeweza kukaa meza moja na mtu aliyemnanga kwa miaka mingi kama fisadi.


Dr. Slaa akakimbia CHADEMA na kutangaza kustaafu siasa ingawa wataalamu wa masuala ya siasa watakubaliana nami kuwa Dr. Slaa alihama kambi akarejea CCM chama chake cha zamani.


Kwa nini Dr. Slaa yuko CCM? Kuna majawabu matatu moja ni juhudi alizofanya kumpigia kampeni Rais Magufuli kampeni za mwaka 2015. Pili kukubali ubalozi na alioteuliwa na Rais Magufuli huko nje na tatu ni kukaa kwake kimya licha ya ukandamizaji mkubwa unaofanywa na Rais katika demokrasia suala ambalo kalipigania muda mwingi.

Tutarajie nini? Ni wazi kwamba jana Edward Lowassa katangaza kurejea CCM kule kule aliko Dr. Slaa na ni imani yangu muda wowote kuanzia jana tutarajie Dr. Slaa kujiuzulu nafasi yake ya ubalozi kwa kuwa "watakaa meza moja" na Lowassa mara kwa mara.


Akitangaza Press Conference au akitoa Press Release naombeni mnijuze!. Wasaalam.
 
Back
Top Bottom