Uchaguzi 2020 Maswali ya Bernard Membe kwa Mgombea Magufuli. Kusini wana jambo lao

Membe ni mpinzani anayepiga kampeni zilizopevuka, amegusia gesi na watu waliopotea Kama miongono mwa Mambo ambayo hayakushughulikwa kwenye serikali ya Jpm, Pia akaahidi kuwaunga mkono ktk shuguli zao za kiuchumi kulingana na eneo husika, Lakini pamoja na hayo yote ukweli unabaki palepale kwamba watanzania ni wengi na mahitaji ni makubwa zaidi, hata Kama ukitokea muujiza Membe akapewa nchi, hatatimiza matakwa yote ya watanzania.
 
Lakini pamoja na hayo yote ukweli unabaki palepale kwamba watanzania ni wengi na mahitaji ni makubwa zaidi, hata Kama ukitokea muujiza Membe akapewa nchi, hatatimiza matakwa yote ya watanzania.

Tatizo la wana-ccm ni kumjenga Jpm kana kwamba amemaliza changamoto zote za nchi hii.

Kwa miaka 4+ ilijengwa taswira kwamba Jpm ametatua kila tatizo linalowasibu waTz na hakuna anayepaswa kufikiria tofauti.

Kila aliyejaribu kusema jambo tofauti, au kuonyesha kwamba eneo fulani lina changamoto, alipewa majina mabaya, alichafuliwa, na hata kusumbuliwa na vyombo vyetu.

Hakuna nchi isiyokuwa na changamoto. hakuna utawala usiokuwa na kasoro, na usioweza kukosolewa, au kuwa-challenged.

Kama nchi zenye ma-flyover, na zinazounda ndege achilia mbali kununua, wanabadilisha watawala wao, kwanini Jpm ajione yeye ni special sana kiasi kwamba ukimkosoa inalazimishwa uonekane kama umekufuru?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom