Maswali ninayojiuliza: Walimu wa Sanaa, Dilema hii inarudisha nyuma maendeleo

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Hadi sasa wanafunzi waliomaliza vyuo katika shahada ya elimu hasa sanaa kwa misimu miwili mfululizo hawajui ni lini na kwa vipi wataajiriwa. Yawezekana kweli kukawa na nia njema iliyonyuma ya ucheleweshwaji huu au zoezi zima la ukaguzi wa wafanyakazi hewa.

Katika asset zote duniani, MUDA ni asset ambayo imethibitika kuwa ya Thamani kuliko zote. Mtu,Kijiji,Nchi ambayo Muda haupewe kipaumbele ni hakika utaishia kuwa mtumwa wa wanaojali Muda.

Maswali haya yameniijia Asubuhi ya leo kabla sijaingia duniani kutimiza agizo sio la Rais tu bali pia ni la Mungu yaani KAZI (kwa wapenzi wa bibilia Kutoka 20:8-11).

1: Ni lini waalimu hasa wa Sanaa na wafanyakazi wengine walio pending watajua hatma yao? Hatuoni tunawaacha watanzania hawa katika dilema na kunarudisha nyuma maendeleo?pia hatuoni haja ya kubadili mifumo yetu ya iwe na kalenda za matukio na watu wajulishwe mapema?

2:Hatuoni kama Mtu akijua Hataajiriwa Miezi nane ijayo, Itamfanya afanye mradi wenye time frame ya miezi nane kuliko kuachwa kwenye dilema maana anaweza kuwekeza leo Dar million hata tatu kesho ukamwambia umepangiwa kufundisha tunduru na uwekezaji wako hauamishiki kirahisi?

3:Kama kuna mtu hafanyi kazi yake kwa wakati na kusababisha ucheleweshwaji wa hitimisho la ajira kwa waalimu hasa wa sanaa na wengine kwa nini asichukuliwe hatua?

4:Unapowaambia wajiajiri, Atajiajiri vipi ukiwa hujaonyesha kwamba Wito wa mtu huyo kulielimisha taifa hauna nafasi tena au ipo finyu ili aprogram upya akili yake kuwekeza kwenye Kujiajiri?

Mfano: Mtu kamaliza 2015 akiwa na uhakika wa kukaa nje bila kuajiriwa kwa mwaka mmoja na nusu siku anamaliza Chuo akili ya mtu huyu ni tofauti na ya mtu anayemaliza Chuo akiwa na uhakika wa kuajiriwa Ualimu muda mchache ujao kutokana na Upungufu bila kujua anamwaka na zaidi mbele yake. Watu hawa wawili ni Rahisi wa kwanza Kujiingiza kwenye shughuli za kimaendeleo kwa Dhati kuliko huyu mwenye Dilema.

Muda Muda Muda Muda Muda Muda Muda Muda Muda Muda
HILI Litafanikiwa kama mambo haya yakianza kuendeshwa kama miradi/Projects
 
Haijawahi kuwepo nchi yoyote inayoajiri wahitimu wake wote. Nadhani tuwe wakweli tu ingawa tunasema mfumo wa elimu ni mbaya tunapaswa kutumia akili zetu kukabiliana na changamoto za kila uchao.Hivi kweli degree holder anakaa kabisa nyumbani kusubiri majaaliwa ya ajira hata kwenye vichekechea hataki kufundisha ili achange kamtaji .Inaumiza sana kwa kweli.
 
yani umenena vema,ajira zitolewe au zisitolewe yote ni sawa tuu hata kama ambao mnatarajiwa kuajiriwa mtaumia vipi.Ila ni vema wenye mamlaka wawe wawazi why kudanganya watu kama watoto?wekeni watu wazi ili wajue moja ni lini zitato
ka au hazitatoka kabisa.Mtoa mada umeandika vema sana,
 
Mkuu hebu tumia akili ni wapi na nilini hii serikali iliwahi kuajiri watu wote?? Msifanye vijana wakawadharau na kuwaona punguani,tunachohoji ni kwanini tumeshindwa kuwa na serikali ya uwazi na ukweli,mfumo wa ajira unajulikana Siku zote,kuna kada ambazo huwa wanawekwa pending kwa ajili ya kuchukuliwa na serikali ikiwemo ualimu na Afya,ni vipi huo utaratibu usitishwe ghafla baada ya kuingia serikali hii ,,?? Walishindwa nn kuandaa watu kisaikolojia mapema ili wakajiandaa toka wakiwa chuoni,tuachane na hayo,vipi kuhusu wale walioajiriwa na kupewa mikataba kisha wakarudishwa nyumbani bila maelezo yoyote?? Unajenga taifa la aina gani ?? Unahitaji hawa watumishi unaowadhalilisha Leo kesho waje kuwa wazalendo,wasaidie taifa lao kwa upendo??na mtakao athilika ni nyie raia mnaofurahia vitendo vya kionevu,sababu wao viongozi watoto wao hawasomi shule zenu wala hawatibiwi hospitali zenu,nyie ndo mtajiandaa kutibiwa na madaktari waliothiriwa kisakolojia na serikali,na tutawapasua vichwa badala ya miguu ,au uletwe mahakamani na kesi ya kuku ni kifungo miaka 10,na kazi ngumu bila Huruma,,jiandaeni tu..watunyanyase sisi na sisi tutadeal na raia wao
 
Uko sahihi mkuu. Lakini changamoto haiji bali kusudi itatuliwe.Hebu fikiri tutalia mpaka lini?ni lazima maisha yako yaendelee tu ije mvua lije jua.Sioni haja ya kukumbatia kisasi. Chukua mf wa rushwa ukipokea mahakamani unatoa hospitali hesabu inabaki ziro.Sawa ni tatizo tunalo je tulitazame tu?au tufurukute!
 
yani umenena vema,ajira zitolewe au zisitolewe yote ni sawa tuu hata kama ambao mnatarajiwa kuajiriwa mtaumia vipi.Ila ni vema wenye mamlaka wawe wawazi why kudanganya watu kama watoto?wekeni watu wazi ili wajue moja ni lini zitato
ka au hazitatoka kabisa.Mtoa mada umeandika vema sana,
Wahusika wanapewa resource nyingi ili wawatumikie wananchi. kuwaweka watu katika suspension mode sio sawa. hakuna ambaye hataki kujiajiri maana hata usipotoa ajira lazima kama mwanadamu akomae ili maisha yaende. Lazima wawe wazi
 
Hasa wa sayansi na Hisabati! Ndo wamewaua kabisaaaa! Maana wamewapa moyo halafu wamepotea!
 
Mods inabidi waanzishe Jukwaa la Kilio cha Walimu, maana hawa jamaa kama ajira zimesitishwa kwao peke yao kila siku wapo hapa wanalia. Waandaliwe jukwaa lao mbona fani zingine hawaji kupost kilio kila siku, wao hawaisomi au.
 
Haijawahi kuwepo nchi yoyote inayoajiri wahitimu wake wote. Nadhani tuwe wakweli tu ingawa tunasema mfumo wa elimu ni mbaya tunapaswa kutumia akili zetu kukabiliana na changamoto za kila uchao.Hivi kweli degree holder anakaa kabisa nyumbani kusubiri majaaliwa ya ajira hata kwenye vichekechea hataki kufundisha ili achange kamtaji .Inaumiza sana kwa kweli.
Hakuna anayelilia ajira mkuu. Hilo linajulikana. Hapa ni suala la Tanzania, Jinsi inavyoendesha taratibu za kumuajiri mwalimu. Ikiwa kuna mabadiliko mawasiliano kwa wakati ni suala la msingi kuliko yote uliyoandika hapo juu.
hata bila elimu wala kutegemea ajira mwanadamu yoyote anaweza kubuni mbinu halali na akaishi.Ndio maana mambo haya ya kutgemea ajira yameshamiri baada ya First industrial revolution. kabla ya hapo ajira haikuwa habari kwa mwanadamu. wanadamu aliishi kwa kufikiri na kubadili mazingira yanayomzunguka ili yamsaidie kuexist.
 
Back
Top Bottom