Maswali ninayojiuliza baada ya wabunge wa CUF kuvuliwa uanachama na wapya kuchukua nafasi zao

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Kwa ninavyofahamu,mtumishi wa umma akisimamishwa kazi analipwa mshahara nusu na baadae akija kuonekana hana makosa/hatia basi hurejeshwa kazini na kulipwa sehemu mishahara yake yote iliyobaki.

Si hivyo tu,hats mtumishi wa umma akifukuzwa kazi na mtumishi huyo kwenda mahakamani na baadae mahakama ikaamuru mtumishi huyo arejeshwe kazini,bila shaka mwajiri(serikali) itawajibika kumlipa mtumishi huyo mishahara ya miezi yote ambayo mtumishi husika hakulipwa kutokana na yeye kufukuzwa kazi kimakosa.

Sasa najiuliza iwapo wabunge wa CUF waliofukuzwa uanachama na kuvuliwa ubunge itathibitika mahakamani kuwa walifukuzwa kimakosa,hawatakuwa na haki ya kudai mishahara yao?

Kama watakuwa na haki hiyo, atakaepaswa kuwalipa ni nani?

Ni chama kilichowavua uanachama na kusababisha wao kupoteza ubunge au serikali inayowalipa mishahara?

Au ni chama ndio kitapaswa kuwalipa fidia?

Mikopo waliochukuwa wabunge hawa(kama ipo) nani atapaswa kuilipa kwa sasa wakati mshahara hawapati?

Kama kuna bima,je, mbunge anapofukuzwa uanachama na hivyo kupoteza ubunge wake,bima hapa inahusika?

Wabunge hawa waliokula kiapo leo hii na kuwa wabunge kamili,si wanastahili mikopo kwa mujibu wa sheria?

Kesho na keshokutwa mahakama ikawavua ubunge wabunge hawa walioapidhwa leo huku wameshachukua mikopo(iwapo watachukua) watairejesha kwa vipato gani?

Au wabunge mikopo yao hawairejeshi kupitia wao kukatwa mishahara?

Kwa mujibu wa sheria/taratibu,serikali hulipa sehemu ya mikopo hii wanayochukua wabunge, sasa ikitokea mahakama imewavua hawa ubunge,kisheria na hivyo wao kuwa si wabunge tena,sheria itaruhusu serikali kulipia mkopo wa mtu ambae si mbunge tena?

Baada ya wabunge hawa wa viti maalumu kuapishwa leo hii na mamlaka husika kuridhia wabunge waliovuliwa uanachama si wabunge halali,serikali inaendelea kulipia sehemu ya mikopo yao?

Au ndio watakatwa mafao yao?

Kwasababu wametumika Bunge kwa muda mfupi tu,mafao hayo yatatosha?

Hapa ndipo napoona hasara ya mahakama kutotoa zuio la wabunge hawa kuapishwa na pia kutoruhusu wabunge wa sasa kuendelea na ubunge wao mpaka pale kesi ya msingi itakapotolewa uamuzi.
 
Ulijiuliza hayo maswali wakati Lissu anamfukuza Zitto au wakati Maalimu Seif anamfukuza Hamad Rashid, hakuna kingine zaidi ya unafiki hapa.
 
Ukawa (kama bado ina exist) wamenasa kwenye mtego! Kitendo cha kuwasusia wabunge wenzao wa upinzani ni kutangaza kutohitaji nguvu yao. Kama hawa wabunge wana vinyongo basi watakuwa upande wa chama tawala. Aidha, kwa kuwakosa hao wabunge upinzani utakosa akidi inayotakiwa ili kuweza kupeleka hoja yoyote bungeni. Kwa hili niseme tu wapinzani wamejipa sifa ya mshumaa, kuwafurahisha watazamaji (wazungu) ilhali wanateketea kwa ndani.
 
Kama mahakama itaamua wabunge wa zamani ni wanachama halali wa cuf basi nila ya shaka watarudi kuwa wa bunge . Tena bila kula kiapo cha mara ya pili.
Na nina uhakika mahakimu wetu wamepata nguvu baada ya kuona wenzao wa Kenya walivo toa hukumu nzito ya uchaguzi bila ya hofu.
Nadhani lazima watataka kutuhakikishia Watanzania kuwa nao pia ni mhimili huru usio weza kuchezewa na mkubwa yoyote.
Hili walofanya. Ccm ni ujambazi wa kisiasa. Kutumia madaraka kimabavu kufanya watakavo....
Lakini tunaamini mahakama zetu hazitakuwa party ya ujambazi huu.
 
Wewe Salary slip usiandike vitu kutokana na hisia zako tuu. Mahakama itazuia wabunge kuapishwa kwa sheria ipi? Hapa Labda umlaumu spika kwa kutokua na subira lakini mahakama haina mamlaka ya kuzuia shughuli za bunge zisiendelee
 
Kama hukumu ya mahakama yaenda kuwa ya haki, basi tutegemee aibu ya aina yake kupata kutokea nchi kwa kitendo kilichofanywa na NEC na Spika wa Bunge. Nina uhakika kama sio shinikizo maafisa wa NEC wasingetoa maamuzi yale haraka na kwa kukurupuka namna ile, pia ofisi ya Bunge kama ingetumia wataalamu wake na sio spika anayesema "wameingia kwenye 18 zangu" mambo yasingekuwa hivi.
Tunaposema taifa linaharibiwa na siasa chafu ndio haya yatakayo jitokeza.
 
Back
Top Bottom