Maswali na Majibu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Bismillah Rahman Raheem..Mimi niwatakie ndugu zangu waislam woote duniani kheri na nema katika kipindi hiki cha mfungo mtakatifu,inshaAllah Allah awafanyie wepesi na dua zenu zikapokelewe na kufanyika baraka,amin!!!

Wabillah tawfiq,ahsalam aleykum.

Ramadan Kareem.

Mumu.
Waaleikum salaam ukhti, asante sana Allah atufanyie wepesi sote Allahu ameen
 
Neno 'Saumu' ki lugha ya Kiarabu lina maana ya kujizuia. Pia ni neno ambalo lilitumika kabla ya zama za Uislamu. Baadaye Uislamu ulipokuja ukalijaalia neno hili kuwa ni moja kati ya maneno yatumikayo kiibada.

Ama maana ya neno hili Kisheria, ni kujizuia kutokana na mambo yanayobatilisha Saumu yaitwayo 'al-Muftiraat'.

Kinyume cha watu wengi wanavyodhani kwamba Saumu hasa ni kujizuia kula na kunywa tu. La Hasha! Bali Saumu ni kukihifadhi kila kiungo chako kutokana na mambo yasiyotakikana.

Amesema lmam Ja'far As-sadiq (a.s.), "Kufunga siko kujilinda na kula na kunywa tu, bali utakapofunga hifadhi (chunga) macho yako, ulimi wako, tumbo lako, masikio yako na uchi wako. Vile vile ilinde mikono yako, pendelea sana kunyamaza ila katika heri tu (kama kusoma Qur'ani n.k.) na umhurumie mtumishi wako."

Naye Mtume (s.a.w.) amesema: "Mambo matano hutengua Saumu ya mtu: Uongo, kuseng'enya, kufitinisha, kula viapo vya uongo na (mwanamke) kumkazia macho mwanamume asiye maharimu wake au (mwanamume) kumkazia macho mwanamke asiye maharimu wake kimatamanio.”

Kuseng'enya kumekatazwa katika kauli hii ya Mtume (s.a.w.) na badala yake tunahimizwa na hadithi nyingi tujiepushe na lolote la kutuharibia Saumu zetu.

Mtume (s.a.w.) anasema: "Mwenye kufunga huwa ibadani wakati wowote hata kama analala madamu hajaitengua Saumu yake kwa kusengenya. Kwa hapa utaona kwamba, kule kutokula na mfano wake kama tulivyo yabaini hapo mbeleni siko kufunga hasa kunakotakikana, bali kufunga ni kujizuia na makatazo yote na mabaya.

Naam Maalim, na je kumkiss mkeo wakati wa kumuga kwenda kazini, yaani kumbusu kwenye shavu au paji la uso kama tufanyavyo wengi wetu kunafunguza swaumu? na kumkumbatia kimahaba bila kufanya tendo la ndo mchana kuna leta mushkir kwenye swaumu?
 
Nimekwambia hivi,TAHAJUD ni kitendo tu sio SWALA.
Hata meditation ya Mshana Jr ni TAHAJUDI.
Kwenye uislam hakuna swala ya TAHAJUDI.
Hata ukhti Madame S amekwambia hapo.
Sisi sote ni wanafunzi tunaelekezana tu hapa tusipotoshe.

Jana Kishki amewaambia waumini wapige makofi pale Taifa,pamoja na elimu yake kuuuubwa ila amechemka.So hata wewe au mimi tukikosea ni kurekebishana.
Ramadhan Kareem

Sheikh, si vibaya ukanitoa ujinga katika hili. Kwenye dini ninavyoelewa Mimi kwa vile yanatumika maneno ya kiarabu huwa yanatafsiriwa kwa namna 2. Ki'maana ya kilugha ya kiarabu(1) na kiistilahi(2). Kwa mfano swaumu ina tafsiriwa kilugha na pili ni sheria ya kidini/kiistilahi. Ila mhusika apate kufahamu zaidi.
 
Naam Maalim, na je kumkiss mkeo wakati wa kumuga kwenda kazini, yaani kumbusu kwenye shavu au paji la uso kama tufanyavyo wengi wetu kunafunguza swaumu? na kumkumbatia kimahaba bila kufanya tendo la ndo mchana kuna leta mushkir kwenye swaumu?
Wakati unasubiri Maalim aje atoe ufafanuzi, naomba nanmie nichangie kidogo.

Kumbusu mkeo inajuzu. Hakufunguzi.

Cha muhimu ni kuepuka michezo baina ya magoti na kitovu.

Allah ndiye mjuzi.
 
Assalaam Alaykum Warahmatullah

Ndg
Allah awabaarik sana popote mlipo

Napenda kutoa nasaha kwa ujumla
Hususan katika jambo la kuomba/kumuombea mtu Duaa kadhalika kuitikia

Haifai kusema
In sha Allah
Hili ametukataza Mtume ﷺ
Usiseme unapoomba Duaa,
mfano
Eee Allah niponye in sha Allah
au
kuitikia kwa kusema

Amiin in sha Allah/Allahumma Amiin in sha Allah

Haya ni makosa kisheria

بارك الله فيكم
 
Assalaam Alaykum Warahmatullah

Ndg
Allah awabaarik sana popote mlipo

Napenda kutoa nasaha kwa ujumla
Hususan katika jambo la kuomba/kumuombea mtu Duaa kadhalika kuitikia

Haifai kusema
In sha Allah
Hili ametukataza Mtume ﷺ
Usiseme unapoomba Duaa,
mfano
Eee Allah niponye in sha Allah
au
kuitikia kwa kusema

Amiin in sha Allah/Allahumma Amiin in sha Allah

Haya ni makosa kisheria

بارك الله فيكم
Malizia mkuu, badala yake tusemeje?
 
Ama neno TAHAJJUD na QIYAAMUL LLAYL

haya maneno,hutumika katika kuelezea ibada za usiku

Neno Tahajjud,hutumika hasa,baada ya mtu kuamka na kufanya ibada za usiku,kwamaana,alale kwanza kisha aamke usiku

na neno
Qiyaamul llayl,hili linakusanya yote,Awe amfanya kabla ya kulala usiku au baada ya kumka
 
Ama kusema
Sala ya Tahajjud,inaswaliwa kumi la mwisho tu katika Ramadhaan,hii si sahihi

Hakuna tofauti katika matumizi ya kisheria katika neno Qiyaamul Llayl,Tahajjud au Taraweeh

Sala za usiku wa Ramadhaan,zimeitwa Taraweeh,lkn ndio hizohizo Sala zinazopatikana katika masiku yasiyo Ramadhaan
 
Kadhalika
kuitwa kwake Taraweeh,ni kwasababu kunapatikana kila baada ya Rakaa 2 au 4 pumziko kidogo
 
Naam Maalim, na je kumkiss mkeo wakati wa kumuga kwenda kazini, yaani kumbusu kwenye shavu au paji la uso kama tufanyavyo wengi wetu kunafunguza swaumu? na kumkumbatia kimahaba bila kufanya tendo la ndo mchana kuna leta mushkir kwenye swaumu?

Kumbusu/ kumkumbatia mkeo hakufunguzi swaumu. Zipo hadithi zilizopokelewa na Bukhari na Muslim zinazoonesha Mtume s.a.w alikuwa akimbusu au kuwabusu wake zake.

Kuna kisa mashhuri kilichotokea kipindi cha mtume s.a.w kinacho nasibiana na swali lako. Alikuja kijana mmoja kwa Mtume kwa kuuliza kama anaweza kumbusu mkewe huku akiwa amefunga Mtume akamjibu hapana. Akaja MTU mzima sana(mzee) kwa mtume akauliza swali hilohilo mtume akamjibu unaweza kumbusu mkeo. Maswahaba wakashangaa swali moja majibu tofauti. Mtume akawaambia yule wa mwanzo ambaye ni kijana shahwa(matamanio yapo karibu sababu damu bado inachemka) anaweza akapndwa na hisia za kujimai na mkewe. Kuhusiana na mzee yule umri umeshaenda kwake inaweza athari za kuwa na mataminio ni ndogo.

Sasa hapo kazi ni kwako, kama unaona matamanio yako hayatoweza kupanda basi kheri. Kama yanaweza kupanda bila shaka unajua ni nini cha kufanya.

Allahu wa rasuuluh aaalam.
 
Malizia mkuu, badala yake tusemeje?

Alichokuwa anakusudia sheikh Abu Dharri ni hivi, inshaallah maana yake Mungu akipenda au kama Mungu akipenda. Kwenye Aamin maana yake tukubalie. Hebu tuyaunganishe haya maneno sasa "Mungu akufanyie wepesi kwenye mambo yako" wengi wetu huwa "inshaallah" yani Mungu akipenda. "Mungu akubariki bhana" hapa napo tunajibu Mungu akipenda(inshaallah).

Tafsiri yake ni kwamba, kwa lugha ya mtaani tunasema "vyovyote poa tu, akipenda asipopenda fresh tu". Hapa Mungu akichelewesha au asipojibu maombi yako usimaindi kwa sababu umempa option ya kutekeleza maombi yako. Ndiyo maana Sheikh Abuu Dharri akatukumbusha Mtume s.a.w amesema utakapoomba dua usiseme Inshaallah, sema Aamin kwa maana Mungu ni(tu)kubalie.
 
Amani iwe nanyi wadau.

Tupo ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mwenye swali kuhusu ibada hii adhim ya swaum anaweza kuuliza hapa ili wajuzi wa Elimu ya Dini watujuze.

Pia tukumbuke kuwa kuuliza haimaanishi kuwa hujui (tu), bali yawezekena wataka kutukumbusha kupitia atakaye jibu.

Mwenye kuuliza anaweza kuwa hajui na anataka kujuwa, au anajuwa lakini anataka kujuwa kama nasi twajuwa ama tu anataka kuuliza kwa kushangaa au kuuliza kwa namna ya kuleta utani.

Tuepuke kuleta utani ili wadau wafaidike na majibu yatakayo tolewa na wenye elimu husika.

Mwenye swali aliweke na tuwe na subira katika kungojea majibu.

Karibuni sana wadau.

Kwa kuanzia naomba kuuliza, NINI MAANA YA SWAUM?


1. Baada ya Kifo chake Mtume Muhammad (SAW) ametuachia Waislam mambo gani muhimu mawili? (a) Kur an na Hadithi AMA (b) Kur an na ahlul bait?
 
Tahajud sio sala.
Taraweh na witiri ni sala 2 tofaut.
Swaum njema

nimekufaham mkuu.
Kutokana na ueleo wangu japo kua sikua nauhakika nikua hakuna sala ya Taraweh wala Tahajud, bali kuna Qiyam lail kwa maana hiyo hayo majina ya tahjud na Taraweh ni wakati tu wakuswali iyo swala ya Qiyam lail au sivo mkuu?
wengi wetu tumekua tukienda ovyo sana kuhusu hili mpaka baadhi ya masheikh kuwashudia wakiteleza kusema kama sala ya Taraweh inapatikanwa ndani ya mwezi wa ramadhani tu.

Sasa je sala ya Qiyam lail (Taraweh na Tahajud) na sala ya witri je nayo nimoja au tafauti?
 
Mtume wa Allah ﷺ
ametuusia kushikamana na Kitabu na Sunna Sahihi

ama jambo la Ahli Bayti wake,
ametukumbusha katika kuwapa heshima yao,kuanzia Ndg zake wanae wake zake
 
Back
Top Bottom