Maswali na Majibu Bungeni: Kwanini Mawaziri baadhi wanajibia sehemu walipo wengine wananenda mbele?

mhuni

JF-Expert Member
May 30, 2015
955
592
Habari ndugu zangu

Naomba kufahamishwa ingawa sijasoma sheria najiuliza sana kuuliza kuhusu suala hili la Mawaziri na Manaibu Waziri katika kipindi cha maswali na majibu mbunge akiuliza swali.

Kuna baadhi ya Manaibu waziri na Mawaziri wanaenda pale mbele karibu na Spika na kujibu lakini baadhi ya Mawaziri wanajibu wakiwa kwenye viti vyao wanasimama na kujibu.

Sasa naomba kujua sheria inasemaje kuhusu kujibu maswali bungeni?

Nawasilisha.
 
Mkuu kwa ufafanuzi ni kama ifuatavyo. Kila kikao cha Bunge, kunakuwa na orodha ya shughuli za bunge kwa siku husika. Miongoni mwa orodha hiyo kuna kipindi cha Maswali na Majibu. Maswali hayo hayaulizwi kiholela bali yanapangwa kwa kila wizara. Wizara moja inaweza kuulizwa maswali kadhaa ya msingi kabla ya kuhamia wizara nyingine. Kunakuwa pia na maswali ya nyongeza yanayoulizwa baaada ya swali la msingi kujibiwa.

Nikirudi kwenye hoja zako, ni kwamba, Mawaziri wenyewe wanajipanga nani ajibu swali gani. Mathalan, kama wamekubaliana kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ndiye atakayejibu swali la msingi na nyongeza litakalohusu wizara yake kwa siku husika, ni yeye pekee ndiye atakayeruhusiwa kwenda pale mbele nadhani jina halisi la mahala pale ni Podium. Ikitokea kuwa kuna waziri mwingine ama majinu ya ziada baada ya yale ya Naibu Waziri kutolewa, Waziri huyo hataenda pale Mbele na badala yake atawasha kipaza sauti chake na kujibu hapo hapo alipo. Huo ndo utaratibu wa mabunge yote duniani kote.

Kwa kifupi ni kwamba, Waziri ama Naibu Waziri anayeenda kujibu pale mbele ni yule tu aliyeteuliwa kujibu swali la msingi na maswali ya nyongeza kwa wizara husika kwa siku husika. Wale ambao hawajayeuliwa kujibu maswali siku hiyo wanapokuwa na majibu ya ziada wanatakiwa kujibu pale pale walipokaa. Hizo ndo protokali za kujibu maswali bungeni
 
Asante kwa ufafanuzi!
 
Back
Top Bottom