Maswali Muhimu kuelekea mchezo wa Yanga baadae

Tariqfinest

Member
Jul 13, 2021
16
23
1, Aina ya sajiri walizofanya kikosini na muda wa maandalizi watawapa mashabiki wao kile walichokimiss kwa muda mrefu ?

2, Kuwakosa Khalid Aucho, Djuna na Mayele kunaenda kuiathiri vipi Yanga ?

3, Kupoteza mchezo wa siku ya wananchi kunaenda kuwapa maswali gani wachezaji ?

4, Uongozi tuka uhukumu kwa matokeo ya mchezo wa leo ?

5, Tabiri ?
 
1: Ni kweli muda wa maandalizi kwa kuchanganya waliokuwepo na waliosajiliwa kupata timu tofauti ulikua mchache, walichokimiss yanga ni uwakilishi wa nchi kwa muda mrefu ambao ulitokana zaidi na matatizo yao wenyewe.

2:Kuwakosa hao wachezaji uliowasema haiwezi kuwa sababu ya kupoteza mechi, msimu uliopita yanga haikua mbovu kiasi hicho, labda ungesema kuwakosa walioondoka ndio ingeweza kuwa pengo kama Kisinda.

3: Kama yanga ilipoteza mchezo wa siku ya mwananchi, ile ilikua ni mechi ya kuangalia zaidi wachezaji kuliko mechi yenyewe ,na leo inaingia kwenye mechi ya mashindano ni mechi tofauti kabisa.

4: Uongozi hauwezi kuhukumiwa kwa mechi ya leo, hata kama muda wa preseason ungetosha,mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote kama hao wachezaji waliosajiliwa na yanga watakua wazuri kama huko walikotoka, na kufungwa ni matokeo ya mpira.
 
Nasimama na benchi la ufundi la mwalimu Nabi,timu ili iwe na muunganiko inabidi ipate muda wa kuwa pamoja angalau 3 mornth na mechi za kutosha.
Mashabiki wa Yanga wawe wapole wakubaliane na matokeo yoyote watakayopata.
 
Timu yetu ni nzuri. Hata ikitokea tukatolewa, bado nitabakia kuwa na imani na kikosi hiki mpaka mwisho.

Muhimu viongozi wa timu na wadhamini waachane na uswahili kwenye malipo ya mishahara na posho za wachezaji.
 
Back
Top Bottom