CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,065
- Ndugu mheshimiwa rais wapo wenzako wengi tu wanapita humu na wengine wana akaunti humu mfano rais wa TFF kwahiyo sitaamini iwapo utasema eti maswali yangu hujayaona.
- Swali la kwanza: Umekuwa rais kwa muda mrefu (pengine kuliko marais wote tukimtoa Mugabe) je ni kitu gani cha kukumbukwa ulichowafanyia hadi sisi walimu tuliopo huku kijijini tujivunie kuwa wanachama wa CWT?
- Swali la pili: chama kimekata 2% ya mishahara yetu tangu kuanzishwa kwake hadi Leo chama kina miradi mikubwa (a) ni faida gani wanachama wanapata kutokana na miradi hiyo zaidi ya kofia na tisheti za mei mosi? (b) ni lini sasa mtaacha kukata hizo 2% kwakuwa chama kina miradi tayari?
- Nashukuru sana naomba unijibu au hata unipm mimi ni mwalimu Allan.