Maswali matano usiyopaswa kuyadharau

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
1. Wale wahujumu uchumi waliokamatwa kwa mbwembwe za ngazi ya PhD kuwa ati wameficha sukari maelfu ya tani na tena watu wakashangilia sana kuwa "walikuwa wanamhujumu na kuzikwamisha juhudi za rais", waliishia wapi?

2. Ni mahakama ipi wamefikishwa hao wahujumu wakubwa?

3. Na yale maelfu ya tani za sukari yaliyotaifishwa yako wapi?

4. Na yale malaki ya tani za sukari yaliyoagizwa yako wapi?

5. Na ile bei elekezi ya Shs 1,800 kwa kilo ni lini itatekelezeka?

Ukiwa mwongo lazima uwe na kumbukumbu nzuri. Jifunzeni kusikiliza na kutafakari ili muhoji na kubaki salama kuliko kusikiliza na kupiga makofi ili muumie muda huo na baadaye. Wale wanaoshangilia matamko ya propaganda za serikali ya sasa hawana wanachomsaidia mjenzi wa nyumba yetu. Wanampeleka porini, wengine tutaendelea kumkumbusha.

Mtatiro J
 
Umemkumbusha nini hapo, mbona povu tu ndio limekujaa. Yaani akili za nyumbu za nyumbu tu. Sukari tunaijua tunaokaa mtaani siyo nyie mnaishi uzunguni huko. Uko masaki utajuaje bei za sukari Missungwi?
 
1. Wale wahujumu uchumi waliokamatwa kwa mbwembwe za ngazi ya PhD kuwa ati wameficha sukari maelfu ya tani na tena watu wakashangilia sana kuwa "walikuwa wanamhujumu na kuzikwamisha juhudi za rais", waliishia wapi?

2. Ni mahakama ipi wamefikishwa hao wahujumu wakubwa?

3. Na yale maelfu ya tani za sukari yaliyotaifishwa yako wapi?

4. Na yale malaki ya tani za sukari yaliyoagizwa yako wapi?

5. Na ile bei elekezi ya Shs 1,800 kwa kilo ni lini itatekelezeka?

Ukiwa mwongo lazima uwe na kumbukumbu nzuri. Jifunzeni kusikiliza na kutafakari ili muhoji na kubaki salama kuliko kusikiliza na kupiga makofi ili muumie muda huo na baadaye. Wale wanaoshangilia matamko ya propaganda za serikali ya sasa hawana wanachomsaidia mjenzi wa nyumba yetu. Wanampeleka porini, wengine tutaendelea kumkumbusha.

Mtatiro J
scripted stunts don't need remembrance just cramming. Yale yalikuwa ni maigizo na yalidhamiriwa kwa muda ule tu yaliposemwa/fanywa baada ya hapo subirini maigizo mengine.
 
Back
Top Bottom