Maswali magumu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Kuna mambo ambayo Rais Magufuli ana shangaza wengi. Kasema kila kiongozi afanye shughuli za kisiasa katika Jimbo lake, sasa tumuulize Rais Magufuli maswali yafuatayo:

1. Freeman Aikaeli Mbowe ni mbunge wa Hai lakini pia ni mwenyekiti wa Chadema taifa. Je, kwanini azuiwe kufanya mikutano ikiwa yeye ni mwenyekiti wa Chadema taifa na siyo kiongozi wa chama kwa Jimbo la Hai??

2. James Francis Mbatia ni mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI taifa na pia ni mbunge wa jimbo la Vunjo. Kwanini azuiwe kufanya mikutano ya kisiasa ngazi ya taifa??

3. Kinacho endesha vyama vya siasa ni RUZUKU. Sasa kwanini vyama vya upinzani vipewe Ruzuku wakati kazi ya Ruzuku ni kuimarisha vyama na kazi hizo zimepigwa marufuku??

4. Kwa hali ya kisiasa kwa sasa na hasa kwa vyama vya upinzani, kwanini tusibaki na Mfumo wa chama kimoja?? Kama kwa sasa tafsiri ya Upinzani ni vurugu, sasa kwanini tusibaki na Chama kimoja??

5. Ni lini na ni nani alifanya tathmini na kugundua kuwa mikutano ya kisiasa jukwaani inazuia shughuli za maendeleo??
Yakijibiwa haya maswali basi Charles nitaunga mkono agizo la Rais.

6. Cecilia Daniel Paresso ni mbunge na aliamua kufanya mikutano ya kutatua changamoto Jimboni kwake bila fujo wala vurugu yoyote ile lakini cha ajabu ni kwamba polisi walimuita kuhojiwa kwa kukiuka AMRI ya kutofanya mikutano ya kisiasa! Je, haki iko wapi hapo??

Lakini pia Rais jana alitoa kauli KALI akiwa kule IKUNGI-SINGIDA, kwamba atakaye mjaribu atamshughulikia BILA HURUMA!

Hii ni kauli CHUNGU na KALI sana, inaweza kuonekana kama ni sawa lakini inajenga hali fulani ya kuwaandaa watu kisaikolojia (nafikiri mmenielewa). Sasa tuendelee kusubiri tuone matokeo ya watu kuandaliwa kisaikolojia!

NB: Tuendelee kumuombea Rais awe na afya njema ili aendelee kuongoza vizuri kwa hekima na busara pia tusichoke kuomba juu ya amani ya taifa! Nchi kwanza!
 
Kwanza kabisa tofautisha mikutano ya kiserikali na ya kisiasa, then:-

1. Kweli kabisa Mbowe na Mbatia, Cheyo, Mrema etc hao ni wenyeviti wa kitaifa wa vyama vyao, wao wanawajibu wa kufanya vikao vya ndani vya vyama vyao - katika mikoa, wilaya na mashina (zingatia vikao vya ndani na si mikutano ya hadhara ya kutaka kutushikisha UKUTA).

2. Ruzuku, ni za chama na si za mwenyekiti wa chama na kakikundi kake, hivyo zinatakiwa kugawanywa katika ngazi ya taifa hadi ngazi ya shina ya chama husika ili kukijenga, ruzuku si ya kazi moja tu ya kutumiwa na mwenyekiti kuzunguka kwenye viwanja na majukwaa (kumbuka ugomvi wa chacha Wangwe na Mbowe ilikuwa ni ruzuku, wakati Wangwe akitaka fedha ziende mikoani na ngazi ya chini zikajenge chama, Mbowe na group lake wakagoma, kilichofuata kila mtu anafahamu).

3. Ujenzi wa vyama vya siasa si mikutano ya mwenyekiti tu, au mikutano pekee ila hata kununua diesel, shajara, bendera, viwanja, spear za magari, magwanda, scarf, miwani ya giza ya red brigade, etc.

4. Kwa kweli hata mimi namuunga mkono rais kuwa atakaye mjaribu amshughulikie maana hakuna namna.
 
Uzuri ni kwamba kwa sasa dunia ni kama ipo naked, pale mambo yatakapotibuka ICC haitawachukua muda kuhukumu kesi dhidi ya dikteta huyu.
 
Kwanza kabisa tofautisha mikutano ya kiserikali na ya kisiasa, then:-

1. Kweli kabisa Mbowe na Mbatia, Cheyo, Mrema etc hao ni wenyeviti wa kitaifa wa vyama vyao, wao wanawajibu wa kufanya vikao vya ndani vya vyama vyao - katika mikoa, wilaya na mashina (zingatia vikao vya ndani na si mikutano ya hadhara ya kutaka kutushikisha UKUTA).

2. Ruzuku, ni za chama na si za mwenyekiti wa chama na kakikundi kake, hivyo zinatakiwa kugawanywa katika ngazi ya taifa hadi ngazi ya shina ya chama husika ili kukijenga, ruzuku si ya kazi moja tu ya kutumiwa na mwenyekiti kuzunguka kwenye viwanja na majukwaa (kumbuka ugomvi wa chacha Wangwe na Mbowe ilikuwa ni ruzuku, wakati Wangwe akitaka fedha ziende mikoani na ngazi ya chini zikajenge chama, Mbowe na group lake wakagoma, kilichofuata kila mtu anafahamu).

3. Ujenzi wa vyama vya siasa si mikutano ya mwenyekiti tu, au mikutano pekee ila hata kununua diesel, shajara, bendera, viwanja, spear za magari, magwanda, scarf, miwani ya giza ya red brigade, etc.

4. Kwa kweli hata mimi namuunga mkono rais kuwa atakaye mjaribu amshughulikie maana hakuna namna.
Kweli na hakika sasa nimeamini kuwa mmelaaniwa kwa kunyimwa akili na maarifa na Mungu pamoja na laana za Wazt. kwa kuwa nyima maendeleo na kusababisha vifo visivyo vya lazima kwa kukosa huduma za msingi na muhimu zaidi ya miaka 55 ya uhuru hadi leo ninapokujibu hivi ni vilio TU.
 
Hivi hii nchi hata wanasaikolojia wa nchi nao ni wanafiki kwa nini au wataalamu wa psychiatric kwa nini wasituambia kiongozi wa aina hii yukoje kwenye uwezo wake wa utu na akili yake
 
Kwanza kabisa tofautisha mikutano ya kiserikali na ya kisiasa, then:-

1. Kweli kabisa Mbowe na Mbatia, Cheyo, Mrema etc hao ni wenyeviti wa kitaifa wa vyama vyao, wao wanawajibu wa kufanya vikao vya ndani vya vyama vyao - katika mikoa, wilaya na mashina (zingatia vikao vya ndani na si mikutano ya hadhara ya kutaka kutushikisha UKUTA).

2. Ruzuku, ni za chama na si za mwenyekiti wa chama na kakikundi kake, hivyo zinatakiwa kugawanywa katika ngazi ya taifa hadi ngazi ya shina ya chama husika ili kukijenga, ruzuku si ya kazi moja tu ya kutumiwa na mwenyekiti kuzunguka kwenye viwanja na majukwaa (kumbuka ugomvi wa chacha Wangwe na Mbowe ilikuwa ni ruzuku, wakati Wangwe akitaka fedha ziende mikoani na ngazi ya chini zikajenge chama, Mbowe na group lake wakagoma, kilichofuata kila mtu anafahamu).

3. Ujenzi wa vyama vya siasa si mikutano ya mwenyekiti tu, au mikutano pekee ila hata kununua diesel, shajara, bendera, viwanja, spear za magari, magwanda, scarf, miwani ya giza ya red brigade, etc.

4. Kwa kweli hata mimi namuunga mkono rais kuwa atakaye mjaribu amshughulikie maana hakuna namna.
kwani wale wahitimu waliozuiliwa kufanya mahafali yao pale udom ulikuwa ni mkutano,kikao au nini
 
Majibu murua, na wakicheza 2020 itakuwa historia kwao
 
Nikuulize wewe ilikuwa ni nini kati ya hivyo ulivyotaja.
wewe umesema kuwa mikutano ya kisiasa ndio tu iliyozuiliwa na mikutano ya kiserikali ni sawa kufanyika....mimi kwa uelewa wangu haukuwa mkutano wa siasa wala kikao cha serikali bali ni shughuli tu ya kusheherekea kuhitimu mafunzo yao....but question is that "kwanini walizuiliwa au ni kwasabab walikuwa ni wanachama wa chadema"?
 
Usichanganye hoja
1. Mh Magufuli alipongea na wananchi huko Manyoni, Ikungi na Singida, alikuwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi, - alikuwa kwenye ziara ya kiserikali na hakusimama na kuongea yote yale kama mwenyekiti wa CCM.

2. Sherehe za kuhitimu hufanywa na chuo husika, hivi CHADEMA siku hizi ina chuo? Kinaitwaje?
 
umeninukuu tofauti mkuu sijamaanisha kama wewe ulivyofikilia, yale mahafali yalikuwa ni ya wana_member wa chadema
 
Nimekupata Boss wangu, napenda unisaidie sasa, umesema yale mahafali yalikuwa ni ya wana_member wa chadema.

Je wale wanamember wa chadema walikuwa wana graduate chuo gani?
 
wewe umesema kuwa mikutano ya kisiasa ndio tu iliyozuiliwa na mikutano ya kiserikali ni sawa kufanyika....mimi kwa uelewa wangu haukuwa mkutano wa siasa wala kikao cha serikali bali ni shughuli tu ya kusheherekea kuhitimu mafunzo yao....but question is that "kwanini walizuiliwa au ni kwasabab walikuwa ni wanachama wa chadema"?
Uyu mkuu wa kaya mbona anahofu sana na hawa wapinzani kwani akiwaachia wafanye iyo mikutano na vyombo vya usalama vikiwalinda kama ilivyo mwaka jana kwenye kampeni kunatatizo gani au kuna kitu hapa kinafichwa wananchi hatujui ili ni jambo la kujiuliza tusiwe washabiki kwakila jambo lisemwalo pia tutafakari
 
UMESEMA NENO MKUU
 
Back
Top Bottom