Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Tunashuhudia Tundu Lissu akiendelea "kuisambaratisha" serikali hii ya awamu ya tano huko katika vyombo vya habari vya kimataifa
Tumeshuhudia namna ambavyo Tundu Lissu "alivyoichanachana" serikali hii ya awamu ya tano kwenye mahojiano yake katika kipindi maarufu cha Hardtalk cha BBC
Tumeshuhudia pia namna Tundu Lissu alivyomtoa "knockout" Balozi wa Tanzania huko Umoja wa Mataifa, Wilson Masilingi, katika mahojiano yao na chombo cha habari cha VoA
Yamekuwepo maswali mengi yakiulizwa hivi seriakali hii ya awamu ya tano hawana watu mahiri wa kuyajibu hayo maswali ya Tundu Lissu??
Jibu nitakalokupa hapo ni hakuna mwanasiasa yeyote kutoka nchini Tanzania ambaye ni Mcha Mungu wa ukweli mwenye ubavu wa kuyajibu maswali hayo ya Tundu Lissu
Hebu niyaweke baadhi ya maswali hayo:-
1. Ni kwanini eneo alilopigwa risasi Tundu Lissu, panapokuwepo na ulinzi wa masaa 24 ya kila siku wa walinzi wenye silaha, hapakuwa na walinzi, katika siku hiyo ya tukio tarehe 7/9/2017??
2. Ni kwanini vyombo vya ulinzi na usalama vya ndani, vimegoma kushirikisha vyombo vya nje vya uchunguzi katika tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu??
3.Je kama vyombo vya ulinzi na usalama vilitoa sababu kuwa hawawahitaji wachunguzi wa nje kuja kuchunguza tukio hilo/kwa madai kuwa wao wana uwezo wa kuwabaini wahalifu hao, ni kwanini hadi sasa, zaidi ya mwaka mmoja na nusu, tokea tukio hilo litokee, hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na Jeshi letu la Polisi na kufanyiwa mahojiano na kuburuzwa mahakamani??
4. Ni kwanini CCTV camera zilizokuwa kwenye nyumba ya Waziri Medard Kalimani, nyumba iliyoko jirani kabisa ya tukio la mashambulizi, zilionyofolewa na kupelekwa mahali kusikojulikana, mara tu baada ya shambulizi lile??
5. Ni kwanini Spika Ndugai amegoma kutoa stahiki za malipo ya matibabu, ambayo ni stahiki ya kila Mbunge anapopata na matatizo ya kuumwa, kwa mujibu wa kanuni za Bunge letu??
Hayo ndiyo maswali magumu kabisa ambayo naweza kudiriki hakuna mtendaji yeyote wa serikali hii ambaye atadiriki kujitia "kitanzi" na kuyajibu maswali hayo, kwa kuwa wahenga walisema PENYE UKWELI UWONGO HUJITENGA!
Nimalizie kwa kusema kuwa siyo KWELI kuwa Mbunge Tundu Lissu analichafua Taifa hili na kuwatukana viongozi wa serikali bila sababu za msingi, bali anataka mumjibie maswali yake anayoyauliza
Majibu SAHIHI yasiyo ya "kutunga" kutoka kwa watendaji wa serikali hii ya awamu ya tano tutayasubiri sana na pengine tutasubiri hadi Yesu Kristo arejee hapa dumiani, bila ya kupata majibu SAHIHI ya maswali hayo!
Tukumbuke msemo wa wahenga unaosema MWISHO WA UBAYA AIBU!