Maswali magumu tume ya mchanga wa dhahabu

-Nani mkweli kati ya tume ya rais na wahusika?
-Je ni mtambo gani ulitumika kugundua kiwango cha madini yaliyomo kwenye makontena?
- Je huo mtambo tunao ama ulikodishwa?
-Kama ulikodishwa ni kutoka wapi?
-Kampuni gani ilipewa hiyo tenda?
-Je yalufunguliwa ama yalihamishwa hapo bandarini ama ilitumika technology gani kugundua KIASI cha madini?
-Kifaa gani kilitumika kufanya sorting?
-Kulikuwa na mizani maalum ya kupimia madini yaliyopatikana?
-Je mchanga na madini mpaka sasa bado vimetenganishwa ama vimerudishiwa kama zamani?
-Zoezi lilisimamiwa na nani?
-Je tume husika ina uwezo wa kupambana kisheria ikashinda ili kuepuka kutia taifa hasara kwa kulipa fidia?
MWISHO! Je tunaibiwa kwenye sheria na mikataba ama kwenye mchanga au kwenye vyote viwili?
Nawakilisha
Si profeseri kasema walifanya "sampling" kwa kuchota mchanga wa mbele kati na nyuma toka containers zote
 
Kwa hili hao wataalamu wetu hawana uzalendo wanatumikia matumbo yao tu, ni bora Mheshimiwa Rais aiambie hiyo tume au kamati ifanye tena uchunguzi wakiwashirikisha wataalamu wa hao ACACIA. Ila ninachojua mimi hata kama matokeo yake hayatkuwa tofauti sana kwa mfano haitapungua chini ya tani 4 za dhahabu kutoka kwenye wastani wa tani 7 hivyo bado watakuwa wanadanganya tu, kwa nini walitumia nguvu kubwa sana kulizima hili jambo na bado wanajaribu kutumia wataalamu mbalimbali kutuaminisha kuwa hiyo ripoti sio sahihi. Mimi nina imani kwa 70% ya ripoti hiyo ya majiologist wazalendo waliyotuletea, kilichobaki ni tusubiri hizi kamati (tume) za wanauchumi na wanasheria, tujue hali halisi na aina mikataba tuliyoingia ili tujue pa kuanzia. Hizo propaganda tumezichoka hasa za wanasiasa wa TANZANIA.
 
Hawa ACACIA na wengine wote ni wezi wakubwa hilo halina ubishi na wanawatumia wataalam na viongozi wetu hasa wa kisiasa kwakuwa huwa wanawapa makombo
Nilichotaka mimi ni kufanyanika kitu ambacho kingewabana kila kona kuanzia kisheria mikataba mpaka Mali ilyokamatwa..kisha unawapiga fine iliyotakata lakini kwa bahati mbaya sana kitulacho ki nguoni mwetu wenyewe
 
Kamati ilisema zoezi lilisimamiwa na vyombo vya ulinzi pia walichukua samples pekee hawakupima mchanga wote unapochukua sample ni kuchukua kiasi kidogo kuwakilisha namba kubwa sio rahisi kupima kiasi chote katika majaribio ni gharama na waste of resources..

Mkuu;
Umenifurahisha sana hapa. Ati, zoezi lilisimamiwa na vyombo vya ulinzi. Yaani walipewa polisi wenye magobore kuwalinda wasidhuriwe na walinzi wa kampuni au?? Sitaki uniambie kuwa walilindwa wasije punguza/ongeza viwango.
Tumechoshwa na wapiga dili. Hadi walinzi wa bank wanachora mission. Tz ni zaidi
 
Hii nchi ni yaaina yake. CCM imefilisi nchi kwa spidi ya ajabu. Ni aibu kuzungumzia nchi inavyopelekwa. Najisikia vibaya natamani watu wengine niwacharaze bakora hadharani. Marehemu mmoja aliwahi kusema wanatumia m.a.k...... kufikiri. Hakukosea hata. Nimeamini. Angalua watu wanapewa nyadhifa wanaenda kufanyia comedy au majaribio. AIBU. Acheni tu inauma si mchezo. EPA, ESCROW, BAE, VYOTE UJINGA UJINGA TU. MADINI, UTALII , ARDHI, MAMBO YA NDANI NI UOZO TENA WENYE UVUNDO. Mijitu inaendelea kutumbua tu as if nothing is here. Business as usual. Too bad so sad
 
Nadhani sote tunajua kwamba hawa wawekezaji wanatuibia sana, sio kwa namna wanavyochukua madini yetu kwao tu ila pia kwa sababu sisi wenyewe tumekubali mikataba ambayo ni feki kuliko maelezo yoyote. Haingii akilini kwamba sisi wenye ardhi yenye dhahabu tukubali tulipwe shilingi elfu arobaini tu kwenye kila shilingi milioni moja ambazo mchimbaji anapata. Mimi naona ni kama mikataba ya hovyo kabisa.

Hao wawekezaji kwenye machimbo ya dhahabu wanatuibia kwa njia nyingi. Kuna watu ambao wamekuwa maeneo ya hao wawekezaji wanasema kuna helikopta zinakuja usiku kubeba dhahabu safi moja kwa moja kuipeleka nchi ya jirani na kuisafirisha kwao kutoka huko. Ndio maana baadhi ya watu waliokuwa wanahusika katika kuzuia wizi kwenye migodi wana mali nyingi sana na Takururu na vyombo vingine vya usalama wameshagundua mali zao zenye thamani kubwa kuliko mishahara yao.

Tena, watu ambao wamekuwa kwenye machimbo wanaamini kwamba kuna dhahabu inafichwa kwenye huo mchanga. Mchanga ukipimwa hauna dhahabu lakini mawe yenye dhahabu yanafichwa ndani. Ndio maana miaka kadhaa iliyopita (awamu ya nne) mabehewa yenye mchanga yalipoanguka kuna watu waliyakimbilia wakawa wanachukua mchanga. Wenye migodi walivyoona hivyo, wakaweka ulinzi kwenye huo mchanga. Kama udongo una dhahabu kidogo sana kwa nini hao wenye migodi waliulinda?

Siku chache tu baada ya ripoti ya wataalamu kutoka, ACACIA wameandika barua kadhaa za kujitetea. Wanahaha. Kuna kitu ambacho hawakuwa wanakifanya sawa. Lakini, bado kwa upande wa sheria nadhani tumejiweka mahali pabaya. Kuna mambo mawili: a) Namna upimaji wa huo mchanga ulivyofanywa na maprofesa wetu na b) Kuzuia huo mchanga ambao kwenye mkataba si mali yetu bali ya ACACIA.

- Je, kwa nini wakati wa upimaji wawikilishi wa ACACIA pamoja na mwakilishi wa kimataifa, (yaani SGS) hawakuwepo ili baadaye ACACIA wasije kukana matokeo? Wangepaswa wasaini ripoti ya kila container, na kuthibitisha kwamba sampuli ilichukuliwa vizuri, na upimaji kwenye mashine ulifanyika vizuri. Navyoona, mahakamani ACACIA wanaweza kutushinda kirahisi kwa kusema kwamba upimaji haukufanywa kwa uwazi wala usahihi. Ndio maana wameshasema kwamba wanataka wapimaji wa kimataifa waletwe. Tena kuna barua yao moja inasema kwamba sampuli za kupima udongo zilichukuliwa kwenye container 44 tu kati ya hizo 277.

ACACIA pia watatushinda kwa vile mchanga ni mali yao (kulingana na mkataba). Watadai mahakamani kwamba kwa kuchelewesha huo mchanga, tumewasababishia hasara kubwa sana. Kwa vile mchanga ni mali yao, kama huo mchanga una madini ya thamani ya shilingi
trilioni moja, basi pesa zetu sisi Watanzania kwenye huo mchanga ni shilingi bilioni 40 tu, na zao ni bilioni 960 !

Na kama itatokea kwamba(kwa bahati mbaya sana) hao wapimaji wa kimataifa watakuja wapime huo mchanga na wakute kwamba hauna kiasi hicho cha madini kilichosema, ACACIA wanaweza kutushitaki kwa kuwaharibia jina maana tayari thamani ya hisa zao kwenye soko la hisa Ulaya zimeshuka sana tangu hili sakata lianze. Tutatakiwa tulipe pesa nyingi sana.

TUSUIRI TUONE (while keeping our fingers crossed).

Naamini KUNA HAJA YA KUVUNJA MIKATABA YOTE YA MADINI. Ni heri tulipe fidia ya kuvunja hii mikataba kuliko kuendelea kupata elfu 40 kwenye kila milioni.

Mikataba yetu iwepo kwa msingi kwamba wawekezaji wa madini wawe wanatulipa asilimia 55, na wao wachukue 45 tu ya kiasi cha madini yaliyochimbwa, lakini wasilipishwe kodi.
Sisi nchi tugawane nao hao wachimbaji gharama zao za uendeshaji kwa asilimia hizo hizo. Kama wawekezaji hawataki, ni heri madini yetu yasichimbwe. Nina imani, makampuni ya kuchimba kwa kugawana 55/45 yatakuwepo mengi tu. Utetezi wa mrabaha wa asilimia 4 tu eti kwa sababu wanalipa kodi ya asilimia 30 ni hafifu kwa sababu hiyo kodi inalipwa baada ya kuondoa gharama (ambazo wenye kampuni wanahakikisha ni juu sana ili kodi inayolipwa iwe kidogo). Kampuni yauchimbaji ikifanya 'mambo yake' na mwisho wa mwaka mahesabu yakionyesha hasara maana yake ni kwamba sasi Watanzania hatupati chochote zaidi ya ile asilimia 4. Kwa hiyo, tunatakiwa tulipwe kwa kiasi cha madini yaliyotoka sio kwa faida au hasara ya kampuni.

Mwisho wa yote, kwa nini sisi kama Tanzania tushindwe kununua hizo mashine za kuchimbia na kuajiri wataalamu wa kimataifa? Kwa nini?

Mkuu mbona maswali yako mepesi sana hata mimi pia naweza kukujibu.

Leo mshana jr kiukweli umeuliza vitu ambavyo hata havifikilishi na namashaka makubwa hukusikiliza siku ile wakati tume inasoma ripoti yake mbele ya raisi.

Pale walifanya uchunguzi kwa kuchukua sample za mchanga katika makontena machache na kwenda nayo maabala kupima.

Na kumbuka yale majibu ni makadilio kwa wastani.
Wewe ndio umefikilia kirahisi sana, maswali kama haya yanahitaji akili nyingi kupita kiasi. Na kama ww ni muhitimu wa shahada au uzamili au uzamivu ungefeli kama ni mtihani.
 
Watu wanavichwa vizito kuelewa,Hebu fikiria kichekechea kidogo ukienda shambani kunakuwa na ndizi za kijan lakini zimeiva, ukazipita ukafikiri mbichi, Ndio mfano wa huu mchanga wa makinikia.
 
Nadhani sote tunajua kwamba hawa wawekezaji wanatuibia sana, sio kwa namna wanavyochukua madini yetu kwao tu ila pia kwa sababu sisi wenyewe tumekubali mikataba ambayo ni feki kuliko maelezo yoyote. Haingii akilini kwamba sisi wenye ardhi yenye dhahabu tukubali tulipwe shilingi elfu arobaini tu kwenye kila shilingi milioni moja ambazo mchimbaji anapata. Mimi naona ni kama mikataba ya hovyo kabisa.

Hao wawekezaji kwenye machimbo ya dhahabu wanatuibia kwa njia nyingi. Kuna watu ambao wamekuwa maeneo ya hao wawekezaji wanasema kuna helikopta zinakuja usiku kubeba dhahabu safi moja kwa moja kuipeleka nchi ya jirani na kuisafirisha kwao kutoka huko. Ndio maana baadhi ya watu waliokuwa wanahusika katika kuzuia wizi kwenye migodi wana mali nyingi sana na Takururu na vyombo vingine vya usalama wameshagundua mali zao zenye thamani kubwa kuliko mishahara yao.

Tena, watu ambao wamekuwa kwenye machimbo wanaamini kwamba kuna dhahabu inafichwa kwenye huo mchanga. Mchanga ukipimwa hauna dhahabu lakini mawe yenye dhahabu yanafichwa ndani. Ndio maana miaka kadhaa iliyopita (awamu ya nne) mabehewa yenye mchanga yalipoanguka kuna watu waliyakimbilia wakawa wanachukua mchanga. Wenye migodi walivyoona hivyo, wakaweka ulinzi kwenye huo mchanga. Kama udongo una dhahabu kidogo sana kwa nini hao wenye migodi waliulinda?

Siku chache tu baada ya ripoti ya wataalamu kutoka, ACACIA wameandika barua kadhaa za kujitetea. Wanahaha. Kuna kitu ambacho hawakuwa wanakifanya sawa. Lakini, bado kwa upande wa sheria nadhani tumejiweka mahali pabaya. Kuna mambo mawili: a) Namna upimaji wa huo mchanga ulivyofanywa na maprofesa wetu na b) Kuzuia huo mchanga ambao kwenye mkataba si mali yetu bali ya ACACIA.

- Je, kwa nini wakati wa upimaji wawikilishi wa ACACIA pamoja na mwakilishi wa kimataifa, (yaani SGS) hawakuwepo ili baadaye ACACIA wasije kukana matokeo? Wangepaswa wasaini ripoti ya kila container, na kuthibitisha kwamba sampuli ilichukuliwa vizuri, na upimaji kwenye mashine ulifanyika vizuri. Navyoona, mahakamani ACACIA wanaweza kutushinda kirahisi kwa kusema kwamba upimaji haukufanywa kwa uwazi wala usahihi. Ndio maana wameshasema kwamba wanataka wapimaji wa kimataifa waletwe. Tena kuna barua yao moja inasema kwamba sampuli za kupima udongo zilichukuliwa kwenye container 44 tu kati ya hizo 277.

ACACIA pia watatushinda kwa vile mchanga ni mali yao (kulingana na mkataba). Watadai mahakamani kwamba kwa kuchelewesha huo mchanga, tumewasababishia hasara kubwa sana. Kwa vile mchanga ni mali yao, kama huo mchanga una madini ya thamani ya shilingi
trilioni moja, basi pesa zetu sisi Watanzania kwenye huo mchanga ni shilingi bilioni 40 tu, na zao ni bilioni 960 !

Na kama itatokea kwamba(kwa bahati mbaya sana) hao wapimaji wa kimataifa watakuja wapime huo mchanga na wakute kwamba hauna kiasi hicho cha madini kilichosema, ACACIA wanaweza kutushitaki kwa kuwaharibia jina maana tayari thamani ya hisa zao kwenye soko la hisa Ulaya zimeshuka sana tangu hili sakata lianze. Tutatakiwa tulipe pesa nyingi sana.

TUSUIRI TUONE (while keeping our fingers crossed).

Naamini KUNA HAJA YA KUVUNJA MIKATABA YOTE YA MADINI. Ni heri tulipe fidia ya kuvunja hii mikataba kuliko kuendelea kupata elfu 40 kwenye kila milioni.

Mikataba yetu iwepo kwa msingi kwamba wawekezaji wa madini wawe wanatulipa asilimia 55, na wao wachukue 45 tu ya kiasi cha madini yaliyochimbwa, lakini wasilipishwe kodi.
Sisi nchi tugawane nao hao wachimbaji gharama zao za uendeshaji kwa asilimia hizo hizo. Kama wawekezaji hawataki, ni heri madini yetu yasichimbwe. Nina imani, makampuni ya kuchimba kwa kugawana 55/45 yatakuwepo mengi tu. Utetezi wa mrabaha wa asilimia 4 tu eti kwa sababu wanalipa kodi ya asilimia 30 ni hafifu kwa sababu hiyo kodi inalipwa baada ya kuondoa gharama (ambazo wenye kampuni wanahakikisha ni juu sana ili kodi inayolipwa iwe kidogo). Kampuni yauchimbaji ikifanya 'mambo yake' na mwisho wa mwaka mahesabu yakionyesha hasara maana yake ni kwamba sasi Watanzania hatupati chochote zaidi ya ile asilimia 4. Kwa hiyo, tunatakiwa tulipwe kwa kiasi cha madini yaliyotoka sio kwa faida au hasara ya kampuni.

Mwisho wa yote, kwa nini sisi kama Tanzania tushindwe kununua hizo mashine za kuchimbia na kuajiri wataalamu wa kimataifa? Kwa nini?

csm_LZY_FourGreatThinkers2_df934172ff.jpg
 
-Nani mkweli kati ya tume ya rais na wahusika?
-Je ni mtambo gani ulitumika kugundua kiwango cha madini yaliyomo kwenye makontena?
- Je huo mtambo tunao ama ulikodishwa?
-Kama ulikodishwa ni kutoka wapi?
-Kampuni gani ilipewa hiyo tenda?
-Je yalufunguliwa ama yalihamishwa hapo bandarini ama ilitumika technology gani kugundua KIASI cha madini?
-Kifaa gani kilitumika kufanya sorting?
-Kulikuwa na mizani maalum ya kupimia madini yaliyopatikana?
-Je mchanga na madini mpaka sasa bado vimetenganishwa ama vimerudishiwa kama zamani?
-Zoezi lilisimamiwa na nani?
-Je tume husika ina uwezo wa kupambana kisheria ikashinda ili kuepuka kutia taifa hasara kwa kulipa fidia?

MWISHO! Je tunaibiwa kwenye sheria na mikataba ama kwenye mchanga au kwenye vyote viwili?

Nawasilisha
Pumba tupu! ila mjue Rais hajakurupuka kama mnvyodhani. Mtaumbuka kama mlivyokuwa mnataka Rais atangaze baa la njaa kumbe nchi ilikuwa na upungufu wa chakula baadhi ya miko, hadi Leo kimya.
 
Back
Top Bottom