Maswali kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu Royal Tour ya Rais Samia Suluhu

maiyanga1

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
1,317
1,790
Kwa sasa hivi rais Samia yuko kwenye Royal Tour akitengeneza filam ili kutangaza vivutio vya utalii kwa lengo la kuvutia watalii wa nje. Ni jambo jema sana.

Maswali kwenu:

1. Gharama za kutengeneza filamu hiyo ni kiasi gani?

2. Je, gharama hizo zilipangwa kwenye bajeti ya 21/22?

3. Rais ndiye mhusika mkuu, ina maana timu kubwa kutoka Ikulu inahusika, bado ni ya Wizara au na Ikulu pia?

4. Huko nyuma Wizara ilishawahi kuandaa kitu kinachoshabiana na hiki, nakumbuka mwaka fulani kwenye ligi kuu ya Uingereza kulikuwa na matangazo katika uwanja wa moja ya timu zilizokuwa zinashiriki, kulikuwa na mafanikio gani?
 
Acheni kujiabisha kwa ushamba wenu na kutofuatilia mambo ya nchi yenu

Rais alishasema kuwa Kuna hii program ataifanya kuanzia mwezi huu na alisema sekta binafsi wachangie na sekta binafsi wakachangia

Unavyouliza bajeti ya hili swala ilipangwa lini unaonesha ni kwa jinsi gani sio kilaza tu bali ni mtu ambaye kazi yako si kufuatilia mambo ya nchi ila kulalamika tu.

Pili fanya kwanza utafiti Royal Tour ni nini? Sio unakuja Kwa great thinkers alafu unafananisha Royal Tour na kutangaza kwenye club ya Sunderland sijui???
 
Back
Top Bottom