Maswali kwa Wiliam Malechela na Wagombea wengine wa Ubunge wa Afrika Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali kwa Wiliam Malechela na Wagombea wengine wa Ubunge wa Afrika Mashariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RabidDog, Apr 3, 2012.

 1. RabidDog

  RabidDog Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 25
  Wakuu JF, poleni na harakati za Arumeru Mashariki na hongereni sana wote kwa kazi kubwa na nzuri! CDM Milele! Pongezi nyingi kwa wana-Arumeru na (kwa wanaChadema) kwa kutumia sanduku la kura kuelezea mapenzi yao na RoadMap ya kulejiletea maendeleo yenu. Wakati tunaendelea na furaha hii, ni vema tuanze kuangalia hili la Afrika mashariki. Naomba kuuliza maswali machache kwa W. Malechela na wenzake wanaogombea nafasi hii! Je ni kutafuta nafasi baada ya Mjengoni kujaa au wanataka kufanya mazoezi kwanza Arusha (pamoja na ajira) kabla ya kuangalia barabara ya mjengoni?

  Willy na wagombea wengine tupe sababu za kufikiri kwamba wewe (na wengine) ndio mnastahili kupewa nafasi hii kati ya watanzania zaidi ya mill 40? Jumuia hii ina faida gani kwetu? Nini Uzoefu, uelewa na Elimu yako ambayo unafikiri itakufanya usiwe wakulala katika Bunge hilo la Afrika Mashariki ambalo viwango vya elimu miongoni mwa wanachama kuwa tofauti. Na utafanya nini katika kulinda masilahi ya Tz

  a) Tutarajie nini kutoka kwako katika kuhakikisha kwamba rasilimali za Tanzania zitaendela kunufaisha Watanzania na sio nchi zingine? Maliasili kama Wanyama hawana mipaka, utafanya nini kuchangia kupotea kwao au kutopotea kwao?

  b) Tayari tuna matatizo na baadhi ya nchi mipaka ya majirani waliowanachama, unafikiri wewe unamchango gani hapa kuakikisha kwamba hii miungano ya kiuchumi haileti matatizo kwa nchi yetu kama zilivyo kero za Muungano wetu TZ?

  c) Unafikiri nini kifanyike tusiwe dampo la bidhaa toka wanachama wengine?

  d) Kama utachaguliwa kwa nafasi hiyo, je kwako ni nchi zipi zinastahili kuwa wanachama wa jumuia hii - nchi kama Somalia, Msumbuji na zingine zinataka uanachama.

  WanaJF, haya ni baadhi tu ya maswali, naomba wengine waongeze na tupate maelezo ya wahusika pamoja na CV zao!

  Kwa heshima nawakilisha
   
 2. k

  kubenafrank Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  W. Malecela jibu maswali haya:-
  1. Kwanini ugombee ubunge wa afrika mashariki?
  2. Huu sio mwendelezo wa wewe kama mtoto wa kiongozi mstaafu wa umma kuminya demokrasia kwa watoto wa maskini?
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Ili kuonyesha kweli utakuwa makini kwenye kusimamia maslahi ya watz
  je umeshatoa ada yako hapa jf kwa mwaka huu wa 2012.
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Hakuna William Machela kwenye orodha ya wagombea,........bali nimeona kuna William John Malecela.
   
Loading...