Maswali kwa Waziri Mkuu Hayana Tija Tena

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475

Masuala nyeti yanayohitaji ufumbuzi wa haraka na ufafanuzi wa serikali yalitegemewa kufanyiwa kazi katika siku hii, kwa sasa hilo halipo tena ni bora muda huo ukatumiwa kwa shuguli nyingine za Bunge

ADIOS
 
maswali ya papo kwa papo kwa mtoto wa mkulima yalipangwa ili yatoe mwanya kwa serikali kutoa mawazo ya nini kinaendelea Arusha,
yule mbunge mwanjelwa aliyeshutumiwa kuiba mataulo Hotelini Arusha ndiye aliyepewa kazi ya kuuliza kuhusu mwafaka na nini kifate baada ya hali hii'
ccm mmechoka kwelikweli
 
Nimeona amewaruka cdm kuhusu kutafuta muafaka wa Arusha na kuwashauri madiwani waliotimuliwa waende mahakamani. Kwakuwa nipo Arusha na leo kuna mkutano wa cdm, nadhani watajibu hilo swala.
Hata hivyo, kumbukumbu zinaonesha aliyeuliza swali ni yule mbunge aliyekamatwa na wahudumu wa hotel ya Arusha Tulip jijini Arusha akiwa ameiba taulo hapo hotelini, Bi Mary Mwanjelwa!
Ni historia tu inamuhukumu...!
 
Wakati waziri mkuu akijibu maswali ya papo kwa pap leo bungeni aliulizwa swali juu ya mazungumzo yake na Mh. Mbowe . Katika uvumi ambao Mbowe na CDM waliueneza kuwa wamekubaliana na waziri mkuu kuwa uchaguzi wa Meya wa Arusha urudiwe. Jambo hili kumbe si kweli na mazungumzo ndio kwanza yamepelekwa kwa msajili wa vyama ili kuundiwa utaratibu. My take : Viongozi wa CDM kuweni na kauli thabiti acheni uzushi
 
a NAMI NIMEMUONA YULE MWIZI WA MATAULO HOTELINI ARUSHA AKIULIZA MASWALI AMBAYO KWA TUNAOMJUA ATAKUWA KAPEWA KABLA ILI AYAULIZE. MWIZI WA MATAULO HANA GUTS ZA KUULIZA SWALI KAMA LILE UNLESS KAPEWA TU AULIZE ILI AONGEZE CV YAKE. MASWALI YALIPANGWA MAKUSUDI ILI KUTAKA KUUA NGUVU YA MKUTANO WA CDM ARUSHA LEO. MAGAMBA MMECHEMKA. ARUSHA HAWADANGANYIKI KWA MAGAMBA YENU NG'O. WANAJUA WANACHOKIFANYA WANAARUSHA.

NAE NDUGAI AKACHOMEKEA KUWA MADIWANI WALICHAGULIWA KWA NGUVU YA UMMA NA WAMEONDOLEWA KWA NGUVU YA VIKAO VYA CHAMA. KWAKE ANAONA WALITAKIWA WAONDOLEWE KWA NGUVU YA WANANCHI, LABDA. KWA SHERIA IPI HAPA TANZANIA? LABDA TUNGEKUWA NA SHERIA YA 'RECALL'. MTOTO WA MKULIMA AT LAST KAWAAMBIA WALE MADIWANI WALIOFUKUZWA WAENDE KORTINI NA AMEKANA YALE MAZUNGUMZO ALIYOFANYA NA MBOWE NA DR WA UKWELI.
 
a NAMI NIMEMUONA YULE MWIZI WA MATAULO HOTELINI ARUSHA. MASWALI YALIPANGWA MAKUSUDI ILI KUTAKA KUUA NGUVU YA MKUTANO WA CDM ARUSHA LEO. MAGAMBA MMECHEMKA. ARUSHA HAWADANGANYIKI KWA MAGAMBA YENU NG'O. WANAJUA WANACHOKIFANYA WANAARUSHA.

NAE NDUGAI AKACHOMEKEA KUWA MADIWANI WALICHAGULIWA KWA NGUVU YA UMMA NA WAMEONDOLEWA KWA NGUVU YA VIKAO VYA CHAMA. KWAKE ANAONA WALITAKIWA WAONDOLEWE KWA NGUVU YA WANANCHI, LABDA. KWA SHERIA IPI HAPA TANZANIA? LABDA TUNGEKUWA NA SHERIA YA 'RECALL'. MTOTO WA MKULIMA AT LAST KAWAAMBIA WALE MADIWANI WALIOFUKUZWA WAENDE KORTINI NA AMEKANA YALE MAZUNGUMZO ALIYOFANYA NA MBOWE NA DR WA UKWELI.


yule ndugai ni mnafiki sana
 
hayana tija kabisa,hajibu alichoulizwa,spika anamkingia kifua.alikubali nin kuwepo kwa kipindi cha maswali ilihali hana uwezo wa kujibu?
 
Katika tamko la chadema kuna sehemu walisema wameongea na pinda uchaguz urudiwe? Wazir mkuu kachoka na ndomana Mnyika alivosema kuwa hana iman nae akatoka nje huku kamenyong'onyea hadi kanatia huruma
 
Jambo moja mi sijalielewa kwa Mh. Pinda, mbona akiulizwa swali au akiwa anajibu swali huwa anachezea chezea vidole?
 
tupeni ratiba ya mikutano ya hapa a town unajua wengine bado tupo ofisini.
wadau tunataka tuombe ruhusa tukaungane na nguvu ya wananchi.
 
Yan had anatia huruma hasa pale Mnyika aliposema hana iman nae akaamua kutoka nje huku kanyong'onyea cjui anaumwa..kila cku maswal yanamshnda iv cku hz maswal ni magumu au Pinda kachoka
 
Nipe tano, Kwan kamati kuu imedanganya nn? Kwamba hawajakutana na pinda au hawajapanga kuundwa kamat na tendwa..achen kupotosha kwa masikio na macho yangu nilimuona Mbowe anasema hvo..kuhusu uchaguz kurudiwa au la wala hakugusia hyo mmesema nyie na kwa maana hyo nyie ndo waongo
 
Mi pia naamini kuwa maswali ya leo yalipangwa kabla. Mh. Pinda alipokuwa akijibu swali la Mh. Hokororo kuhusu pembejeo za kilimo cha korosho ameonyesha viashiria vya kuwepo kwa upangaji wa maswali kabla. Inasikitisha kweli jamani... loh! Kipindi cha maswali kwa Waziri mkuu kitakosa mvuto punde tu kikianza kutumiwa kwa maslahi ya chama fulani.
 
Back
Top Bottom