Maswali kwa Mwanakijiji na wengine wenye kufanana naye katika mtazamo wa siasa...

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Baada yakuzisoma makala zake tano zenye udhui la kulandana kwa jicho la tatu zaidi, imenilazimu kumuuliza maswali machache ili kujua zaidi msingi wa makala zake na yatarajiwayo KESHO.

1. Mkuu Mwanakijiji, maamuzi ya kamati kuu yalikuwa halali ama haramu kwamjibu wa katiba ya Chadema ya mwaka 2006?

2. Kutokana na maamuzi hayo, kuna haja ya chama kuacha katiba na kusaka kinachoitwa suluhu kwenye meza ya mduara?

3. Ipi nafasi ya Chadema katika uzingatiaji wa katiba yake na miiko ya chama katika mfumo huu wa vyama vingi nchini?

4. Wewe umekuwepo katika anga za siasa za Tanzania kwa mda mrefu sana, na umekuwa karibu kisiasa na wanasiasa wengi akiwemo Zitto Kabwe, je ipi nafasi ya Zitto Kabwe wa leo katika siasa za Chadema zinazotembea na kuishi katika katiba yake?

5. Vyama vya CUF, CCM na NCCR MAGEUZI vimeshaadhibu wanachama wake tena kwakuwavua uanachama kabisa huko nyuma, naomba uwathibitishie makutano wa jf ama popote pale kama uliwahi kutumia nguvu inayoshahabiana na hii unayotumia leo katika kubatilisha maamuzi ya cc ya Chadema,

Majadiliano ya hoja ni msingi wa ujenzi wa taifa lenye tija katika nyanja zote,

NB

Mods nawaomba msiunganishe uzi huu na zingine,
 
Mwanakijiji namkumbuka post yake ilikuwa ya pili katika thread ya kuwavua akina Zitto vyeo.
Tena alisema cc walichelewa kufanya maamuzi. I would be amazed if I come to realize Mzee Mwanakijiji has deferent colors

Ndio maana nimeomba ajibu maswali hayo ili kupata msingi thabiti wa ujenzi wa hoja mpya dhidi yake
 
Mimi huwa siwaamini wapambanaji wanaokula kuku na watoto wao wanasoma kwa raha huko,huku wakituma silaha kwa waafrika wauane wenyewe!ushindi ukipatikana ndio wanakanyaga ardhi husika kutaka vyeo

Ni kweli. Mzee Mwanakijiji ni wakuangaliwa kwa macho mawili mawili. Ana unafiki wa ajabu ajabu hasa linapokuja suala linalomgusa Zitto
 
mimi huwa namuona mzee mwanakijiji ni mnafiki kama pasco ingawa nilianza kufatilia siasa kwasababu ya hoja zake hapa JF, ila ninacho kiona ni kuwa huyu hajui hsli halisi ya tanzania na bahasha zina muumiza..
 
Mwanakijiji namkumbuka post yake ilikuwa ya pili katika thread ya kuwavua akina Zitto vyeo.
Tena alisema cc walichelewa kufanya maamuzi. I would be amazed if I come to realize Mzee Mwanakijiji has deferent colors

Ninaamini bado msimamo wa Mwanakijiji ni ule ule kwamba wasaliti watafutiwe mlango wa kutokea!
 
Kingine tofauti na kuwavua akina Zitto vyeo na uanachama wao itakuwa ni chaos
Watakuja watu na chambuzi zao tata but the bottom line is kwa mujibu wa Katiba ya Chama na kwa mwenendo wa watu hawa ni kwamba wanahatarisha mustakabali wa chama kwa kushiriki mbinu chafu za kutaka kuua uwepo wa CHADEMA
Nimeona kwenye muendelezo wa makala ya Mwanakijiji anaimba nidhamu nidhamu nidhamu nitashangaa kweli akipendekeza watovu hawa wa nidhamu wakae kwenye meza ya majadiliano na wasamehewe, sababu kwa ujeuri wa kiwango cha juu their demeanor inaonyesha kuwa hawaitaji msamaha huo bali kutupiliwa mbali kabisa
 
Ni kweli. Mzee Mwanakijiji ni wakuangaliwa kwa macho mawili mawili. Ana unafiki wa ajabu ajabu hasa linapokuja suala linalomgusa Zitto

Nina Taarifa kwamba Mzee Mwanakijiji anaandaa anachoita Mapendekezo na Suluhisho lake dhidi ya Waasi.

Sidhani kama anaweza kujidhalilisha kusema Wasaliti na Waasi wasamehewe!! Sidhani..

Kwa sababu kwa mtu makini kuwaacha Wasaliti na Waasi ni kuichimbia Rasmi Kaburi Chadema.
 
Kwa hivi sasa kila anayeitakia mema Chadema ni lazima akubali Kufukuzwa kabisa uanachama Zitto na Wasaliti wenzie ndiyo njia pekee ya kuiingiza Chadema Ikulu 2015

Zitto asipofukuzwa nitawashangaa chadema.
Nitawashangaa chadema kwa Zitto aliyeamua kuvaa roho ya usaliti, akaamua kuwasaliti wapigania haki wa kweli wa chadema, nitawashangaa chadema hasa ninapokumbuka mauaji ya Daudi Mwangosi, Ally Zona, Mauaji ya Soweto, Mauaji ya January tano, Kufukuzwa kwa madiwani wa Arusha, kupigwa mapanga kwa wabunge wetu Kiwia na Machemli kwakuwa alikuwa nyuma ya yote haya. Nitawashangaa chadema kama hawatamfukuza Zitto ambaye ameamua kupigania maslahi yake badala ya maslahi ya wengi
 
Kingine tofauti na kuwavua akina Zitto vyeo na uanachama wao itakuwa ni chaos
Watakuja watu na chambuzi zao tata but the bottom line is kwa mujibu wa Katiba ya Chama na kwa mwenendo wa watu hawa ni kwamba wanahatarisha mustakabali wa chama kwa kushiriki mbinu chafu za kutaka kuua uwepo wa CHADEMA
Nimeona kwenye muendelezo wa makala ya Mwanakijiji anaimba nidhamu nidhamu nidhamu nitashangaa kweli akipendekeza watovu hawa wa nidhamu wakae kwenye meza ya majadiliano na wasamehewe, sababu kwa ujeuri wa kiwango cha juu their demeanor inaonyesha kuwa hawaitaji msamaha huo bali kutupiliwa mbali kabisa

Chadema kusamehe Waasi itakuwa ni Pigo Takatifu kwao.

Chadema watakuwa wameprove Failure kabisa na wananchi wataogopa kuwakabidhi Dola.
 
Nina Taarifa kwamba Mzee Mwanakijiji anaandaa anachoita Mapendekezo na Suluhisho lake dhidi ya Waasi.

Sidhani kama anaweza kujidhalilisha kusema Wasaliti na Waasi wasamehewe!! Sidhani..

Kwa sababu kwa mtu makini kuwaacha Wasaliti na Waasi ni kuichimbia Rasmi Kaburi Chadema.

umjui mwanakijiji wewe,hana rangi moja uyo mkuu.
 
mimi huwa namuona mzee mwanakijiji ni mnafiki kama pasco ingawa nilianza kufatilia siasa kwasababu ya hoja zake hapa JF, ila ninacho kiona ni kuwa huyu hajui hsli halisi ya tanzania na bahasha zina muumiza..

Ooh .... Hapana Crashwise!... Hilo la bahasha umenistua sana.. Ukisema Pasco ndie mzee wa vibahasha nitakubali ila kwa mwanakijiji sitaki kuamini..... Mimi huwa namfuatilia sana mwanakijiji jf na makala zake kabla mwanahalisi haijafungiwa na kwenye magazeti mengine!... Lini ameanza kuwa mnafiki??
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuwa maswali yameelekezwa kwa MMM basi ngoja tumsubiri aje kujibu hoja hizo...

Otherwise ya Chadema tuwaachie Chadema...
 
Back
Top Bottom