Maswali kwa mkurugenzi wa HESLB ndugu Badru

Afrikasana

JF-Expert Member
Oct 27, 2021
320
283
Mpaka kufikia leo January 9/2022 baadhi ya wanachuo hawajapewa mikopo tangia wamefungua vyuo yani wengine wanakaribia kusaini awamu ya pili wapewe fedha,wengine walisha saini ila hawajapewa fedha zao za awamu ya kwanza mpaka sasa. Je wewe mzee unataka nini hasa kwa watoto wa wanaume wenzio?
Je kama unawatoto au wajukuu waliopo masomoni hujawapa pia hela za kujikimu kwa miezi miwili sasa?

Hivi hizo hela kama zingekua za kwako siungetaka kusujudiwa kabisa?

Naomba kukuuliza hivi nikwanini unampangia mtu mkopo,unamsainisha kisha humpatii haki yake?
Hivi nikwanini wanachuo ambao hamkuwapa mkopo mwaka wa kwanza na mkaanza kuwapa mkopo mwaka wa pili hamtaki kuwapa malimbikizo ya mwaka wa kwanza?

Au wewe mzee ni mwanasiasa unapenda sana kuona maandamano ya watoto maskini hapo kwenye ofisi za bodi?
Hivi mzee unadhani wewe utaishi milele hapo bodi?
Au una maagano gani na mamlaka iliyo kuteua?
Kama huogopi mamlaka ya uteuzi umeiweka mkononi je Mungu humuogopi?
Mzee unakera sana,nielewe nikisema unakera. Wewe mzee ni jipu haiwezekani unakaa na fedha za wanachuo karibia miezi miwili huwapi.
Au hata wewe hujala na kunywa muda wote huo?
Hivi hiyo ni roho ya mzazi wa kitanzania kweli ambaye ameenda shule?
Tofauti yako msomi wewe na asiyesoma au asiyejua umuhimu wa elimu ni ipi?
Mzee ninayo maswali mengi lakini ngoja nikuache uendelee kuyatafakari hayo.

Jambo la ajabu huyo mama anayejiita Veronica Nyahende nae anasema eti bodi itaanza kutoa mikopo ndani ya masaa 24. Hivi huyo anafanya watu ni mazuzu?
Miezi miwili hutoi hela leo unahadaa watu na habari za masaa 24? Masaa 24 unayajua au unayasikia?
Miezi miwili umeshindwa masaa 24 utayaweza?
Wewe mama huwezi kuwa serious

Hiyo bodi imejaa majipu matupu kuanzia makao makuu mpaka wasimamizi wa kanda hadi vyuoni. Simu hampokei mkipigiwa

Mmejaa harufu za rushwa hata yatima na maskini pia mnatamani wawape rushwa ndio mtimize wajibu

MAMLAKA HUSIKA ONDOENI HAO WAZEMBE WAMEVIMBIWA VIYOYOZI
 
Wanauhakika hamna wa kuwababaisha,,nchi hii watu wengi hatuwezi kutimiza majukumu yetu kiuzalendo
 
Mpaka kufikia leo January 9/2022 baadhi ya wanachuo hawajapewa mikopo tangia wamefungua vyuo yani wengine wanakaribia kusaini awamu ya pili wapewe fedha,wengine walisha saini ila hawajapewa fedha zao za awamu ya kwanza mpaka sasa. Je wewe mzee unataka nini hasa kwa watoto wa wanaume wenzio?
Je kama unawatoto au wajukuu waliopo masomoni hujawapa pia hela za kujikimu kwa miezi miwili sasa?
Hivi Watanzania ni nani aliyewaloga maana mimi simo,unapewa dhamana kubwa kama hii halafu unajifanya mungu mtu,hivi hiyo mkurungezi anajua machungu wanayopitia watoto wa maskini kwa kuwacheleweshea mkopo?
 
Hiyo bodi ingebaki kwa wanafunzi waliodahiliwa vyuo vya binafsi na badala yake imeharibu kabisa elimu hadi kwenye vyuo vikuu vyetu vya umma ambako watoto wa wanyonge wanapata elimu huko. Wizara kupitia idara ya elimu ya juu irudishe utaratibu wa zamani wa kutoa ufadhili wa masomo kwenye vyuo vikuu vya umma, badala ya kuiacha loan board kuvuruga elimu ya vijana wa kitanzania...
 
Ukifika HESLB ndio utasikitika zaidi maana majibu yao wanaonesha wamelogwa kweli na wamezoea ofisi wala hawajali
 
Hiyo bodi ingebaki kwa wanafunzi waliodahiliwa vyuo vya binafsi na badala yake imeharibu kabisa elimu hadi kwenye vyuo vikuu vyetu vya umma ambako watoto wa wanyonge wanapata elimu huko. Wizara kupitia idara ya elimu ya juu irudishe utaratibu wa zamani wa kutoa ufadhili wa masomo kwenye vyuo vikuu vya umma, badala ya kuiacha loan board kuvuruga elimu ya vijana wa kitanzania...
Asante kwa maoni wanaohusika waone na kuyafanyia kazi
 
Especially continues walio pata kwenye batch ya mwisho hamna alie pewa pesa zake.sasa nashangaa kutoka mwezi wa 11 hadi leo Office kama iyo ina shindwa vipi kuwahisha mambo ..hili ni jipu kweli

Hivi hamna mfanyakazi wa bodi humu ajibu
 
Wenye madeni tumalizie mapema muda si meingi tutasikia value retensio imerudi...hisia zangu lakini
 
Dawa ya majipu ni kuyatumbua tu, hakuna namna. Tatizo sasa hakuna mtumbuaji na anayeweza kufanya hivyo anayaangalia tu. Ile wetu usaha ukianza kuvuja!
 
Back
Top Bottom