Konakali
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 1,533
- 263
Wewe kama waziri wa ujenzi umesimama mbele ya wana Igunga kumnadi mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM, na kuahidi kutenga bajeti maalum kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mbutu iwapo watamchagua Dr. Dalaly Kafumu...! Maswali yangu ni:
- Je, iwapo wana Igunga wakaamua kumchagua mgombea wa CUF, CHADEMA, au chama kingine chochote, hilo daraja halitajengwa?
- Je, kama watanzania wote tulishuhudia bajeti nzima ya serikali; ikiwepo ya wizara ya ujenzi, ikipitishwa na bunge kwa upungufu, hadi kubatizwa kwa jina la "kasungura kadogo", wewe hiyo bajeti utaitoa wapi?
- Kama mojawapo ya kazi za bunge letu ni kujadili, kupitisha na kuidhinisha bajeti ya taifa letu, hiyo bajeti yako mwenyewe itajadiliwa, kupitishwa, na kuidhinishwa na nani, lini na wapi?
- Kama umeahidi kuwa daraja litajengwa, je ni lini hasa daraja hilo litakuwa tayari, na unawashauri nini wana Igunga iwapo itafika muda huo bila daraja hilo?