Maswali kwa JK

Mensarum

Member
Apr 16, 2009
9
0
Wadau kuna jamaa wamenitonya hapa watakutana na JK mchana huu hapa DK. Mimi nipo mbali kidogo na Copenhagen so kama kuna maswali mnadhani
ni muhimu akaulizwa mnaweza kunipenyezea kabla ya 11:30am sawa´na 12:30pm East African time.

Nasubiria, then Mods mtaiondoa baada ya huo muda asante´ni
 
Naomba uumuulize Nini alichowafanyia waTz tangu awepo madarakani 2005??Umaskini wa waTz umekithiri ni nini matarajio yake kwa kipindi kijacho!
 
Akiulizwa kwa nini Rostam na wenzie (mafisadi) wake wako juu ya sheria ingekuwa vema sana
 
Tunaomba umuulize mchakato wa Dual Citizenship umefikia wapi? Swali la pili Watanzania walio Nje, watapiga kura Uchaguzi wa 2010? Swali la tatu , Atatoa nafasi mbili za ubunge kwa Diasporas? kama ilivyo kwa makundi mengine maalumu, kwa lengo la kuchota utaalamu wao, market knowledge, foreign policies, na FDI's?
 
nadhani hapa tumefikia mwisho
naenda kazini na hayo ndio maswali nitamtumia mkuu atakaenda kwenye hicho kikao
 
Alisema madini itakuwa win win situation kwa kurekebisha mikataba mbona kimya? mbona mapendekezo ya kamati zote za madini anayafungia kabatini?
 
Diaspora kupewa nafasi bungeni is a rather foolish idea. They are not a disadvantaged or less fortunate group.. Its just a minority, like the number of people with more than 1million dollars.. so on that argument they too should get representantion. Diaspora ya watu wasiotaka kwenda kujenga nchi... they would rather kaa-MBELE tuu...lol
 
Aulizwe safari ya kuja huko na ujumbe wake imegharimu kiasi gani? Na je mafanikio ya safari hiyo yanazidi gharama hizo?
 
Tafadhali Aulizwe kuwa kuna dalili tosha ya Wazanzibari wote hawataki Muungano pamoja na Karume jee ataendelea Kuulinda Kwa Nguvu au atakaa chini kuandaa utaratibu wa KURA YA MAONI YA KITAIFA JUU YA MUUNGANO.
 
Tafadhali aulizwe yale Majengo ya Kifahari anayoyajenga Chalinze pesa zake kazitowa wapi? ikieleweka kuwa CCM haina sera ya UBEPARI na aeleze alipoingia Madarakani mali alizo nazo alizioredhesha na zinalingana na alizo nazo sasa
 
Anyway kumuuliza ni sawa, ila ubongo wake wa kipanzi panzi unaweza kutoa jibu la kukera zaidi. Kimsingi JK hana majibu ya kuleta suluhu, ni chekacheka boy. Miaka 4ameulizwa maswali na amejibu na hakuna kilichobadilika saana. Nadhani kugoma kumuuliza maswali inaweza kuwa tiba ya majibu yake ya kisiasa
ninaota tuu ndugu zangu mnisameheeee.........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom