Maswali kuhusu mawimbi ya teknolojia ya mawasiliano

Africa Tanzania

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
1,504
2,261
Habari za muda huu wataalam.
Bila shaka kila mtu anaujuzi katika eneo fulani na kaupata kutoka sehemu fulani.....Kupitia ujuzi huo naomba kufahamishwa machache kati ya haya nisiyoyafahamu!

1.Tunafahamu kuwa kwa sasa sayansi na teknolojia vinakuwa kwa kasi sana sote tunashuhudia, Katika kasi hii hii kuna kitu kinachosafirisha taarifa kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine (sikijui sina utaalamu) sasa basi, Haya mawimbi ambayo hayaonekani yanayozalishwa na wanadamu wenzetu yana madhara gani katika suala zima la afya ya viumbe hai?

2.Maana kila siku redio mpya zinazaliwa, visimbuzi vipya vinazaliwa, artificial satellite mpya zinarushwa kila kukicha anga za juu, internate inapanda viwango kutoka 2G, 3G, na sasa 4G, minara mipya kila kata kijiji inawekwa......Je, ni mamlaka gani Inayopima kasi ya mawimbi haya na udhibiti wake kwa viumbe hai?

3.Je, mimi kama binadamu wa kawaida nitajuaje kama eneo ninaloishi lina mionzi mikali inayozalishwa katika mifumo hii ya teknolojia ili niweze kuhama?

4.Je Nchi kama Yetu Tanzania, ina uwezo kiasi gani kuzuia mionzi inayoletwa au inayowekwa na mataifa mengine angani kwa manufaa yao ikiwa yanatuletea madhara bila manufaa kwa viumbe hai vyote vya nchi hii?

5.Simu ninayotumia, au iwe computer nitajuaje kama kwa sasa mionzi inayoingia ni mikali mno inaweza kunisababishia madhara nikiwa naitumia?

Nimewaza sana, naombeni majibu hapo! Maana kuuliza si ujinga.....Nitarudi kwa maswali ya nyongeza
 
Kuna Tume ya Sayansi na Teknolojia
na Tume ya Nguvu za Atomiki na Nyuklia

naona kama maswali yako yanawalenga wao moja kwa moja...

ila kwa kuwa elimu zaidi hawaitoi, tunaamini wataalam zaid huku JF watatusaidia kujibu
 
Back
Top Bottom