Maswali kuhusu matumizi ya stendi mpya ya mabasi Mbezi (so-called Magufuli)

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,174
73,616
Kuna tangazo linasema safari zote zitaanzia stend mpya Magufuli. Tangazo linazidi kusema mabasi makubwa wakodishe mini bus kuwasafirisha abiria kuwaleta stend mpya au wawaelekeze abiria kuja Mbezi.

Sasa swali:
1. Anayekwenda Mtwara na yuko Mbagala, naye aje Mbezi? maana tangazo linasema stend zote za Temeke etc zimefutwa

2. Anayekwenda Tanga/Moshi/Arusha na yuko Tegeta aje Mbezi if not so, mabasi yaliyokuwa yanapitia Bagamoyo niliyoyataja hapo juu, mtu wa Tegeta atayapandia wapi? Aje Mbezi?

3. Mabasi ya Tanga/Moshi/Arusha kupitia Bagamoyo yatachukua njia gani kukusanya watu wa Mwenge, Tegeta, Bunju then na kuendelea na safari ya kwenda mikoa hiyo via Bagamoyo? Au wa Mwenge aje Mbezi? Wa Bunju? au mabasi yatatoka Mbezi na kuja na Morogoro road, Ubungo, Mwenge na kuingia Bagamoyo road?

Msaada tafadhali wa maswali hayo.
 
Huu ujinga upo Tanga,

Mnashushwa Kange, mnapandishwa daladala had mjini, Bus linaenda tupu mjini. Na vice versa

Halafu mizigo mtachukua mjini.
Ndio ujinga mkubwa wanaofanyiwa watu. You incur double expenses maana kama una mizigo mikubwa unajuta! Ndiyo hiyo inakuja Mbezi na foleni hizi. Unashuka Mbezi, unakwendaje Kimara na foleni hizi za Dar na mizigo! Wameweka utaratibu gani wa shuttle buses kutoka Mbezi kwenda sehemu zingine za Jiji, say Mbezi Mbagala, Temeke, Kigamboni, Mwenge etc etc etc. Ilibidi kuwe na connection za city shuttle buses to various destinations in Dar!
 
Hili la Bagamoyo road nimeliwaza sana,
Mimi hua nachukua mizigo k.koo naipeleka mwenge, basi inakuja inabeba..

Sasa najaribu kuwaza kama hakutakua na basi inafika mwenge hili litakua ni pigo kwanguu,
Either kukodi cary mpk mbezi au nihamie kwenye transist za mafuso zinazoondoka usiku.
 
Hako kautaratibu kapo mikoa yote iliyijenga stendi Mpya. Kuna siku Nimeenda Iringa nako ni hivyo hivyo. Basi linaendana mjini na lina ofisi kubwa tu, lakini haliruhusiwi kwenda na abiria,mnashuka nje ya mji then mnapanda dalala.
Kuna tatizo hapo imagine unashuka saa sita usiku na daladala hakuna na una mizigo mingi mikubwa!!!
Wenye mabasi kushusha ofisi zao ilikuwa ni huduma nzuri ya kumsaidia abiria

Kinachotakiwa kitamkwe ni kuwa basi zote zipitie stendi kuu kuanzia safari au kumaliza safari ziwe na abiria au la lazima zipitie ila kusema marufuku kuwa na abiria haliko sawa

Pili kuua hivyo vituo vingine vilivyokuwepo ni kuua ajira za mamia ya watu waliokuwa wakipata riziki zao kupitia hizo stendi ndogo kuanzia maduka teksi bodaboda bajaj wabeba mizigo mama lishe nk zingeachwa tu kama sehemu ya Transit kama ilivyo ndege tu kuwa stendi kuu ubungo stendi ndogo temeke Au mbagala au tegeta au kariakoo au ofisi juu ya basi nk ili kuondoa usumbufu kwa abiria .Sipati picha mtu anaishi mbagala anaenda mtwara aende mbezi kupandia gari kule wakati mfano mwenye gari ana ofisi kuu hapo hapo mbagala na basi linaanzia hapo kwenda mbezi kubeba abiria!!!!

Chukulia mfano basi zima wamekata tiketi watani zangu wamakonde wanaoishi mbagala wanaenda kwao basi linaanzia hapo hapo mbagala ofisi kuu ya basi .Kwa hiyo hao makonde wanatakiwa wapande daladala kwenda mbezi na hilo basi liende tupu hadi mbezi lipakie hao makonde kwenda nao mtwara!!! ni kituko badi watakalopanda liko mbeke yao tupu na wao wako kwenye daladala kwenda mbezi

Haya maamuzi mengine hayako sahihi
 
Mbagala si watapandia mbagala. Ila magari yataanzia mbezi then watapita temeke mpaka mbagala then kimoja to mtwara.
The same to route ya moshi. Wanaanzia mbezi wanaikamata ubungo mwenge tegeta bunju bagamoyo then boom
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom