Maswali Kidogo

O

oloo

Guest
Nimekua nafuatilia mijadala ya computer kwa muda mrefu , lakini kuna vitu ambavyo naona watu haswa nyie mafundi hampendi kujadili au hata kama mkiulizwa basi mnakwepa na kuwaachia watu wengine wajichanganye wakati wataalamu wenyewe mumekaa kimya

Naomba kuanzisha mada hii kwa mara ya kwanza na samahanini kwa kuanzisha mada hii sitaki kugombanisha watu , mie ni mwanafunzi nahitaji kujua .

1 ) Jinsi ya kulinda komputa yangu

2 ) Njia za kuhakiki vitu vyangu ndani ya computer

3 ) Ulinzi wa Ziada katika computer yangu

4 ) njia za kusajili computer yangu

5 ) nikiibiwa computer nifanye nini ? au njia za kufuatia

6 ) mambo mengine mengine kuhusu computer na mitandao
 
Nimekua nafuatilia mijadala ya computer kwa muda mrefu , lakini kuna vitu ambavyo naona watu haswa nyie mafundi hampendi kujadili au hata kama mkiulizwa basi mnakwepa na kuwaachia watu wengine wajichanganye wakati wataalamu wenyewe mumekaa kimya

Naomba kuanzisha mada hii kwa mara ya kwanza na samahanini kwa kuanzisha mada hii sitaki kugombanisha watu , mie ni mwanafunzi nahitaji kujua .

1 ) Jinsi ya kulinda komputa yangu

2 ) Njia za kuhakiki vitu vyangu ndani ya computer

3 ) Ulinzi wa Ziada katika computer yangu

4 ) njia za kusajili computer yangu

5 ) nikiibiwa computer nifanye nini ? au njia za kufuatia

6 ) mambo mengine mengine kuhusu computer na mitandao

ndugu Oloo,

nadhani maswali yako ni mazuri sana na yako wazi kabisa...,nitajitahidi kuyajibu kwa kadri ya uwezo wangu.

swali la 1.jinsi ya kuilinda kompyuta yako..,

kwanza ni muhimu kujua unatakiwa kuilinda kompyuta kutokana na vitu gani hasa..,navyo ni:-

-wezi(wahalifu)
-hackers(software'attackers)
-viruses-(hardware and software)
-spyware's(software,advertising bots and malawares)
-Keyloggers and trojans(data miners and phishers)
-adawares and popups
-accidents(spills and accidental falls)
-matatizo mengine madogo madogo.

baada yakujaribu kutaja matatizo hayo ya kujilinda nayo nadhani itakuwa rahisi kidogo kujaribu kuelezea sasa jinsi ya kujilinda na matatizo hayo

-wezi(wahalifu)

hawa kwa kweli sio expert ya kuwaelezea sana,muhimu ni wewe tu kuwa makini.hasahasa katika matumizi ya komputer yako,kama ni laptop ya ofisi ni vizuri kuiacha ofisini mara baada ya kazi(ulinzi ni mkubwa zaidi),na kama una kazi za ziada ni vyema ukahakikisha iko katika upeo wako wa macho(hasa kwenye public transports).

hapa pia nitajibu swali lako la mwisho je iliibiwa je??ufanyeje??
wahenga husema preventation is better than cure.ni vema ukajilinda kwanza.kwa kuiweka laptop yako katika mazingira yasiyovutia wezi.kutumia laptop kwenye Bar downtown sio sehemu nzuri kabisa!!

njia rahisi ya kuweza kuipata tena laptop yako mara baada ya kuibiwa ni kui-preinstall with "hardware trackers"...,hii ndio njia bora zaidi ambayo ni rahisi zaidi kulocate hasahasa kama mwizi wako hajui mengi kuhusiana na laptop..,huduma kama hizi zinapatikana kwa large producers kama LENOVO au sony ukiwa una-customise executive laptop models..,sijui kwa upande wa Tanzania kama hilo lawezekana.

software tracker yaweza tumika pia lakini binafsi sishauri...,kwani it can easily be bypassed by well minded thief!!


-hackers
jinsi ya kujilinda na hawa jamaa ni kutumia kifaa rahisi kijulikanacho kama router(configured with a firewall)--its the best option kwa mtu asiyejua mengi kuhusu computer..,

na kama watumia laptop i suggest u get a very capable firewall like agnitum post firewall.i have suggested to be extra carefull in laptop kwani its even easier for gifted hackers to monopolise wireless connection of your laptop to get in your computer..!!

other good firewalls include zone alarm jetico etc..!!

here also remember to do something about your evil ports and tcp bondage!!especially if its an office laptop,its easily done but needs an expert to do it well..,or unless you know what your doing!!(if havent figure out how to do this i will write a separate artcle on how to accomplish this important security step)

otherwise if you are using vista i suggest u dont use administrator account for simple tasks or commonly!!

-viruses
these are easily contained if u follow their rule of thumb!!never ignore them!!hahahaaa!!that simple!!

be very strict about the type of antivirus u use..,and make sure its compatible with your system flawlessly..,

a good antivirus not only will it remove viruses,but it will also proactively stop new viruses at a high rate!!and it will be light on resourses..,meaning it wont slow donw your system..,

my suggestion comes down to only three antiviruses so far i found satisfying

NOD32,KASPERSKY,BITDEFENDER.

-spywares

just as viruses..,spyware are todays most troublesome problem for computers and internet at large..,they are so serious that they are responsible for many bad behaviours in any infected computer today...,crashe,slowdowns,blue screens,sluggishness...,its all spywares..,

give them a knockdown with a regular scan..,with at least two engines and with an online scaner!!!

here i would suggest a combination of counterspy and spyware doctor..,also spysweeper can do!!and any online scanner will do!!

-keyloggers and trojans!!

here comes a problem that any executive used to face in daily basis...,spies!!people who wants to know your whereabouts and whatabouts!!
and now its becoming a problem for anyone owning a computer and connects with the internet!!

the best way is to have a keylogger monitor as well as frequent scanner of your activities..,

two softwares will prove priceless for you...,

spybot search and destroy and hijackthis(this needs help using!!)

-spams and popups

here i mean aggresive advertisement that frequently fills your inbox..,hundreds of mails that other date 2059!!

th secret is simple..,

have a toolbar installed and use an updated browser!!i suggest firefox or a very well tuned IE7..,

and if you realy hate spammers then consider having a spam blocker and filter..(i personally use superAd blocker-its very good)

-Accident & spills

if an accident is very serious,here there is nothing you can really do..,BUT..,there is the best hope for you!!especially for accidents that are not worthy loosing your datas for!!

consider a simple laptob slip from a table..,it will definatelly lead to a crack..,BUT with well engineered laptops like THINKPADS its not worthy loosing all your datas in the hard drive..,or loosing you harddrive at all!!

well engineered computers will keep you away from simple worries..,remember they might cost a bit more expensive..,BUT dont forget experts says costs of buying a new laptop is only 20% of its whole cost!!you will eventually spend 80% in maintenace and keeping well of that laptop!!

what expensive(well engineered) laptops do,is they make you spend like 30% in buying and even less in maintenace!!

so in 5 years you might find yourself spending more for your cheaply bought than if you had bought a lillte bot expensive machine!!

-matatizo mengine madogo kama betri na hard drives failure....,i suggest you use your computer(laptop) in a heat releasing area..,like a table or wood!!,avid using it in heat traping environment for longer times like pilllows or soft sofas!!since it will only lead to heat trapped which will lead to high operating frequencies of CPU and hence..,more deterioting of battery..

about hard drives i suggest u get yourself a drive with at least 2 year warrant..if its external,and also dont forget to have backup of all your harddrive!!!very important part of protecting your data!!and as a rule of thumb...,never forget to have windows restore on!!since it can sometimes save u big time!!

if u use lucrative laptop like THINKPADS you will find yourself with lots of a lot of management softwares namely THINKVANTAGE...,if u use these carefully u will be ok..,that says if your brand comes with rescue services make use of them!!


2 ) Njia za kuhakiki vitu vyangu ndani ya computer

hili swali sijalielewa mkuu!!

3) swali lako la tatu nadhani linaweza kupata majibu hapo juu!!

4) njia za zusajili komputa zipo nyingi..,cha kuangalia ni kuwa mara unapoinunua then dont forget to visit your vendors website..,i am sure there u will get an easier gateway to registering and support!!some vendors even offer further discounts for further parts for registered computers..,vitu kama antivirus..OS..,au even printers and other peripherals..,

sure there is a lot to write!!

what about hivyo hapo juu??kama kuna maswali zaid si vibaya yakawekwa wazi kabla hatujaenda mbali!!ili tuwe pamoja!!
 
Bwana oloo sio kweli kwamba watu wanakimbia kusaidia na kutoa ufafanuzi , ukweli ni kwamba wengi hawaaminiani wengi sio waaminifu na kadhalika , mfano unaweza kujitoa kumsaidia mtu kitu chake , badaye yake akakugeuka kwa sababu zake mwenyewe , wakati wewe umeshapata mateso makubwa manyanyaso na kudhalilishwa sehemu hizo siwezi kuendelea na hiyo badala yake nitajibu maswali yako uliyouliza lakini ujue mimi sio yesu kwahiyo siko kamilifu najibu kutokana na kile ninachojua mimi

1 ) Jinsi ya kulinda komputa yangu
Kuna njia mbali mbali za kulinda computer yako na vitu mbali mbali ndani yake , unachotakiwa uangelie ni wakati huo umenunua computer yako mfano kuna programu gani zimetoka mpya za mambo ya ulinzi na usalama na vitu vingine vingi vingi .

Zamani watu walikuwa wanategemea zaidi password katika CMOS sikuhizi watu wanaweza kuondoa hizo password , lakini katika laptop za dell ndio wengi wanashindwa kwa sababu nyingi zinazokuja pwd zake zimewekwa kwatika eprom .

Lakini ukisoma katika mitandao kuna wengine wanatoa ushuhuda kwamba wameweza kutoa pwd za eprom na kuweza kuendelea na shuguli zao lakini sijawahi kuhakikisha hizo habari kwa sababu zinasemwa na watu wa nje zaidi ambao ni ngumu kuonana nao .

La zaidi ni kutafuta kampuni ambazo zinasajili hizi computer na laptop mfano ikiibiwa ikichomekwa katika internet iweze kuwasiliana na database ya kampuni husika ndio waweze kujaribu kuitafuta hiyo laptop .

Mfano mzuri tazama tovuti ya www.hp.com ukiingia pale unatafuta drivers kuna sehemu ya kubonyeza unascan vitu vilivyoko katika computer yako , hiyo ina maanisha nini ? ina maanisha HP inaweza kusaidia wateja wake kutafuta laptop zao na computer zao kama walizisajili na kampuni yao siku za mbeleni

Mimi binafsi niliwahi kufanya jaribio hilo kutafuta laptop Fulani iliyokuwa sehemu nyingine lakini nilitumia programu maalumu na programu yenyewe sasa imeshapitwa na wakati ila suala hili ni gumu sana manake kama nilivyosema mwanzo unaweza kumsaidia mtu , yeye akaenda kukuripoti polisi na mambo kama hayo ni mpaka serikali ifanyie marekebisho sheria za mambo ya mawasiliano na tuwe na wataalamu zaidi wa mambo haya ili tueweze kwenda sawa .
2 ) Njia za kuhakiki vitu vyangu ndani ya computer
Kuna njia mbali mbali za kuhakiki , moja ni wakati unanunua hiyo computer kumwomba muuzaji akuorotheshee majina ya vitu na serial namba zake kwa ajili ya ref za baadaye lakini pia kuna programu maalumu za kufanya hivi kama BELARC ADVISOR programu hii unaweza kuiweka katika computer yako na ikakupa taarifa zake na unaweza kuzisave sehemu tofauti kwa ajili ya matumizi ya baadaye haswa katika inventory yako kama una computer nyingi na hii inasaidia sana wakati computer inashida .

Njia nyingine ni kutengeneza Recovery Disk na Ghost Images , ukimaliza kufanya installation ya computer yako kila kitu unatengeneza recovery disk ambayo inaweza kutumika computer yako ikiwa na shida , sasa hii recovery inakuwa na kila kitu kuhusu hiyo computer yako au kifaa chako .

3 ) Ulinzi wa Ziada katika computer yangu
Unashauriwa uwe na account mbili katika computer moja administrator au ita jina lolote , na ingine guest , kuna wakati moja ya hizo accounrt inaweza kucorrupt ukalazimika kutumia ingine , na kama unavyojua katika windows xp ukishaweka pwd katika account yako hauwezi kuigusa tena mpaka labda utumie computer yenye windows 2000 au 2003 ambayo ina uwezo wa over write permissions kuchukuwa mamlaka ya hiyo windows xp wengi yamewakuta wanashangaa wanapoteza data zao .
4 ) Njia za kusajili computer yangu
Kuna baadhi ya sehemu niliona wanasajili computer zao na wanaweka software maalumu ambayo ukilogin inaweka rekodi katika database maalumu , nakumbuka zamani kampuni ya raha mfano ilikuwa inasajili network card za computer kwa ajili ya mtandao ukitumia kadi tofauti huwezi kutembelea mitandao ,ongea na raha.com ujue mpango wao huo kama unaweza kuendelezwa kwa vifaa vingine pia .
5 ) nikiibiwa computer nifanye nini ? au njia za kufuatia
Kwanza nenda kituo cha polisi ripoti tukio hilo wakati una ripoti tukio hilo waaambie vitu vifuatavyo .
1) Sehemu ya tukio , muda , siku
2) aina ya kifaa chako , serial namba , model yake .
3) vitu vilivyokwemo ndani vingine kama hdd ( ukubwa gani aina yake ) , ram ukubwa wake , mainboard , casing na kadhalika kwa sababu kuna wengine wanaweza kubadilisha baadhi ya vitu kama imeibiwa )
4 ) kama uliweka programu zozote , aina zake na version zake
Hivyo ndio vitu vinavyoweza kusaidia uchunguzi zaidi hapo mbeleni ingawa jeshi letu la polisi ni dhaifu katika vita hii na polisi wengi hawani uelewa mwingi kuhusu computer .

6 ) mambo mengine mengine kuhusu computer na mitandao
Kuna mambo mengi sana wewe kaa tu angalia hapo watu wanajadili nini na kuuliza nini pengine ndio utapata wasaa wa kuweza kujua na kujinufaisha zaidi , usisite kuuliza hata maswali ya kipuuzi na uchokozi huo ndio mwanzo wa kuelewa vitu na mambo mengi zaidi .

Yote haya tunayojadili na tutakayo kuja kujadili yanahusiana na data , kila mtu anataka alinde data zake na taarifa zake zingine

Ila ninachokushauri , usipende kucheza na data , kama unajua umuhimu wa data , unaweza ukapoteza data za watu na mali zao data ndio muhimu kuliko vyote inaonyesha wewe ni mwanafunzi .

Samahanini kwa kuwaingilia wakubwa .

Ahsante na wewe ukiwa na kingine uliza tu tunaweza kushiriki wote kwa namna moja au nyingine , wakati mwingine unaweza kuacha namba yako ya simu tuweze kuongea na wewe moja kwa moja kujua experience yako na mambo haya hapo ulipo au ulipokwepo .

SAFARI MOJA HUANZISHA INGINE
 
Jamani saa nyingine yaangalieni maswali ya hawa watu. wanakuja kutafuta desa la shule. ukiwa na assynment ya shule umiza kichwa usitegeshee watu wakufanyie wewe ukopi tu.
 
Back
Top Bottom