Maswali kadhaa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,193
25,504
Leo asubuhi, kupitia Kituo cha Runinga cha Clouds katika kipindi cha Clouds 360, nilimtazama na kumsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumzia mambo kadhaa yanayoihusu Wizara yake. Amezungumzia mambo mengi yakiwemo yatakayozungumzwa kwenye Bajeti ya Wizara yake itakayowasilishwa tarehe 19 mwezi huu.

Katika maelezo yake, aligusia zoezi linaloendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwasikiliza wanawake waliotelekezwa na waume zao wakiwa na watoto. Kimsingi, Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa zoezi hilo lipo ndani ya sheria, yaani lipo kisheria. Hii ni kwasababu, wanaowasikiliza wanawake hao ni Maafisa wa Ustawi wa Jamii ambao wana mamlaka ya kufanya hivyo.

Waziri Ummy Mwalimu ameongeza kuwa alichofanya Mkuu wa Mkoa Makonda ni kuwatia shime na ujasiri wanawake hao kwenda Ofisini kwake kusikilizwa badala ya wanawake hao kwenda kwenye Ofisi za Ustawi wa Jamii. Akasema kwa kusisitiza kuwa Maafisa Ustawi wa Jamii ndiyo wanaowasikiliza wanawake hao na ikibidi wanaume watakaotajwa nao wataitwa na kusikilizwa. Kama hakutakuwa na maridhiano, mambo hayo yatapelekwa mahakamani.

Waziri Ummy Mwalimu akasema pia kuwa anaungana na Naibu Waziri wake Dr. Faustine Ndugulile kukemea kuvunja faragha za watoto katika kusanyiko hilo. Akasema kuwa ameongea na Paul Makonda na kuahidi kutatua tatizo la faragha linalojitokeza hata mitandaoni kuwahusu watoto. Amewaasa wanawake na wanajamii kwa ujumla kutowaanika watoto katika mitandao kwakuwa kwa kufanya hivyo ni kuingilia faragha zao.

Sasa maswali:

1. Je, tamko au tangazo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda lililenga wanawake hao kusikilizwa na nani hasa- yeye Mkuu wa Mkoa wa Mkoa na Wasaidizi wake au na Maafisa Ustawi wa Jamii?

2. Je, Maafisa Ustawi wa Jamii wako chini ya Wizara au Mamlaka gani hadi iwezekane Mkuu wa Mkoa awakusanye Maafisa hao Ofisini kwake kuwasikiliza wanawake na changamoto zao?

3. Je, kwanini faragha iwahusu watoto tu na si wanawake na wanaume wanaohusika katika zoezi hilo?

4. Je, Maafisa wa Ustawi wa Jamii wanayo mamlaka kisheria kutoa amri ya kufanyika vipimo vya damu kumhusu 'mzazi' na mtoto?

5. Je, kama kazi za Wizara zinafanywa na Mkuu wa Mkoa, kuna uhalali wa zoezi zima?
 
Kwa sasa kuna moral panic kwa service users na providers pia, Sababu watendaji na viongozi wao wanachanganya madawa na kuvuka mipaka yao. Ktk case studies za harakaharaka zilizonikuta katika maofisi tofautitofauti yanayotoa huduma kwa wananchi nimekuta mifarakano ya taarifa tofauti za ushauri wa nini nahitajika kufanya au kufuatia katika uhitaji wangu wa services kutokea Kwao. hii inaonyesha lack of understanding katika professionalism nyingi nchini.
 
Mkuu Petro uko vizuri. HASA uliposema faragha haiwahusu watoto tu bali hata wanawake wenye watotot hao na wanaume ambao kila kukicha tunasikia mara wa Lowasa mara wa Petro mara yule wa Makonda na mara yule wa Mwanaulanzi nk.

Kumtaja mtu kwamba amemtelekeza mtoto ni kumvunjia heshima kabisa.

Sasa Rais inabidi aangalie tena kuteua labda mkurugenzi wa manyanyaso ya watoto na kina Mama Kama alivyofanya huyu mkuu wa jiji alipolikoroga kwenye madawa ya kulevya.

Kimsingi si kosa la mtu awaye yote ila ni KUKOSA ELIMU Kama viongozi wetu wangekuwa na Elimu na ufahamu makosa ya uzalilishaji ya namna hii yasinge kuwepo.
 
Kwani mzee mwenyenyumba kasemaje mpaka sasa? Manake twaona watoto wanajigonga gonga tu na kupigana vikumbo
 
Hili suala la Makonda na mengine aliyokwisha fanya yanadharirisha watendaji wengine wa serikali. Mtu mmoja anaingilia mamlaka zote za nchi, kiasi ambacho hata waziri mkuu hawezi kudiriki. Hili ni moja ya madhaifu ya serikali ya awamu ya 5 ya utawala. Wasipoangalia huyu "mwendawazimu" ataivua nguo serikali pamoja na maafisa wake waandamizi.

Tatizo la DAB ni ukurupukaji na kufanya kazi za kujionesha. Hili ni tatizo la mazero-brain, siku zote hawajiamini na kila wanachofanya wanataka kionekane ni bonge la deal hata kama ni cha kawaida ua hata kama hakikutakiwa kufanyika kabisa. Eti anasema wanayo mamlaka ya kupima DNA! Hivi makonda hajui hatua hii hufikiwa wakati upi na ni vigezo gani huangaliwa kabla ya upimajiji halali kufanyika? Ni mahakama ipi itapewa mzigo wa kusikiliza kesi za namna hii na zile za malezi ya watoto kwa maelekezo na shinikizo la watawala? Ifahamike kuwa akina mama hawa sikuzote wamezungukwa na madawati ya jinsia na ustawi wa jamii lakini hawakuchukua hatua ya kushitaki.

Mkuu wa mkoa anayo mamlaka yake kisheria. Hata hivo mamlaka yakitumiwa vibaya inakuwa ni shida. Kazi ya Mkuu wa mkoa ni kuhamasisha na kuelekeza sekta zingine za uma kufanya mambo flani, sio ofisi ya mkuu wa mkoa kujigeuza jeshi la polisi, ustawi wa jamii, wizara au hata mahakama.

Serikali ya Magufuli iangalie mara mbili utendaji kazi wa mtu huyu. Si kila anaetembea na jembe ni mkulima mzuri, na si kila anaevaa vazi jeupe ni daktari -anaweza kuwa muuza bucha tu. Kwa kweli ilikuwa ni mapema sana kumpromote huyu kichaa.
 
Dah, haya mambo kuna DER mmoja alikuwa na mtoto mahali na alipeleka mkaa na chochote apatacho akiwa safarini na kumpa Pesa kidogo. Dada kdanganywa jamaa anataka raha tena, kaenda ustawi eti asiende pale bali wakutane ustawi kumpa mahitaji. Hata mwezi hajamaliza kwanza kutusumbua tuliokuwa mashemeji zake eti jamaa hapitishi mkaaa. Tulichoka sana. Bahati Mbaya jamaa katumbuliwa lkn ilikuwa Mbaya sana.
 
Na ikitokea majibu y'all DNA yanaonyesha aliyetuhumiwa sio baba wa mtoto itakuwaje, ofisi ya mkuu wa mkoa inayoendesha zoezi itaweza kulipa fidia ya udhalilishaji?
 
Leo asubuhi, kupitia Kituo cha Runinga cha Clouds katika kipindi cha Clouds 360, nilimtazama na kumsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumzia mambo kadhaa yanayoihusu Wizara yake. Amezungumzia mambo mengi yakiwemo yatakayozungumzwa kwenye Bajeti ya Wizara yake itakayowasilishwa tarehe 19 mwezi huu.

Katika maelezo yake, aligusia zoezi linaloendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwasikiliza wanawake waliotelekezwa na waume zao wakiwa na watoto. Kimsingi, Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa zoezi hilo lipo ndani ya sheria, yaani lipo kisheria. Hii ni kwasababu, wanaowasikiliza wanawake hao ni Maafisa wa Ustawi wa Jamii ambao wana mamlaka ya kufanya hivyo.

Waziri Ummy Mwalimu ameongeza kuwa alichofanya Mkuu wa Mkoa Makonda ni kuwatia shime na ujasiri wanawake hao kwenda Ofisini kwake kusikilizwa badala ya wanawake hao kwenda kwenye Ofisi za Ustawi wa Jamii. Akasema kwa kusisitiza kuwa Maafisa Ustawi wa Jamii ndiyo wanaowasikiliza wanawake hao na ikibidi wanaume watakaotajwa nao wataitwa na kusikilizwa. Kama hakutakuwa na maridhiano, mambo hayo yatapelekwa mahakamani.

Waziri Ummy Mwalimu akasema pia kuwa anaungana na Naibu Waziri wake Dr. Faustine Ndugulile kukemea kuvunja faragha za watoto katika kusanyiko hilo. Akasema kuwa ameongea na Paul Makonda na kuahidi kutatua tatizo la faragha linalojitokeza hata mitandaoni kuwahusu watoto. Amewaasa wanawake na wanajamii kwa ujumla kutowaanika watoto katika mitandao kwakuwa kwa kufanya hivyo ni kuingilia faragha zao.

Sasa maswali:

1. Je, tamko au tangazo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda lililenga wanawake hao kusikilizwa na nani hasa- yeye Mkuu wa Mkoa wa Mkoa na Wasaidizi wake au na Maafisa Ustawi wa Jamii?

2. Je, Maafisa Ustawi wa Jamii wako chini ya Wizara au Mamlaka gani hadi iwezekane Mkuu wa Mkoa awakusanye Maafisa hao Ofisini kwake kuwasikiliza wanawake na changamoto zao?

3. Je, kwanini faragha iwahusu watoto tu na si wanawake na wanaume wanaohusika katika zoezi hilo?

4. Je, Maafisa wa Ustawi wa Jamii wanayo mamlaka kisheria kutoa amri ya kufanyika vipimo vya damu kumhusu 'mzazi' na mtoto?

5. Je, kama kazi za Wizara zinafanywa na Mkuu wa Mkoa, kuna uhalali wa zoezi zima?

Inawezekana leo watu wanaanza kumlaumu Paul Makonda kwa initiative hii lakini wanasahu taasisi ambazo kisheria zinapaswa kushughulikia jambo hili zimekuwa very dormant na hivyo kusababisha shida kubwa. Nafikiri mpaka hapa ilipofikia, Idara ya Ustawi wa Jamii itakuwa imeamka na kujua kuwa:

1. Shida hii ni kubwa
2. Watu hawana imani nao
3. They are not pro-active
4. Wanatumia sheria ya zamani kufanya kazi na hivyo watu kuwaona kama hawana msaada
 
Sasa maswali:
1. Je, tamko au tangazo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda lililenga wanawake hao kusikilizwa na nani hasa- yeye Mkuu wa Mkoa wa Mkoa na Wasaidizi wake au na Maafisa Ustawi wa Jamii?

2. Je, Maafisa Ustawi wa Jamii wako chini ya Wizara au Mamlaka gani hadi iwezekane Mkuu wa Mkoa awakusanye Maafisa hao Ofisini kwake kuwasikiliza wanawake na changamoto zao?

3. Je, kwanini faragha iwahusu watoto tu na si wanawake na wanaume wanaohusika katika zoezi hilo?

4. Je, Maafisa wa Ustawi wa Jamii wanayo mamlaka kisheria kutoa amri ya kufanyika vipimo vya damu kumhusu 'mzazi' na mtoto?

5. Je, kama kazi za Wizara zinafanywa na Mkuu wa Mkoa, kuna uhalali wa zoezi zima?
Mkuu Wakili Msomi, wewe ungekuwa mwandishi wa habari, ungekuwa ni bonge la mwandishi!.
Japo maswali yameelekezwa kwa Waziri Ummi, na sio member humu, labda naibu amjibie, ila naomba kuchangia.

1. Aliyewaita ni RC, RC ndiye rais wa DSM anaweza kumuita yoyote, popote, kwa ridhaa kama alivyofanya, au kwa summon, waliokuja wamekuja kwa ridhaa zao, alichofanya ni kuwakusanya tuu na kuwakabidhi kwa maofisa husika which is a good thing!. Amini usiamini hata knowledge tuu kuna ustawi wa jamii, hata mimi nakiri, nimezaliwa hapa na sipajui ustawi wa jamii!, hivyo wito huo wa Makonda ni ukombozi kwa wengi.

2. Kama ilivyo kwa rais wa nchi, rais wa mkoa pia mamlaka zote katika mkoa wake ziko chini yake!.

3. Hoja ya faragha kwa Watoto ipo kisheria kabisa as minors, ila faragha ya wahusika, kwa sababu they are over the age of the majority, wako free kutamka hadharani na kutawaja wenzi waliowapa ujauzito na kuwatekekeza, but behind the camera, yaani off the record. Zoezi ni zuri na limefanyika kwa nia njema ila media haikupaswa kuitwa, au kama ni kuitwa ili tuu kuonyesha extent na sio details.

4. DNA ni suala la kisheria, umeelezwa pale, zinatumika taratibu za reconciliation, wakishindwa ni mahakamani na huko ndiko DNA itapimwa kwa lazima, mfano wewe Mselewa umemtia mimba Lara1 au Miss Natafuta, kisha ukamkana mimba sii yako, mtoto amezaliwa copyright na wewe, lakini bado ukamkana, umeitwa ustawi wa jamii umekana, unaambiwa pima DNA kuthibitisha sio wewe, umekana, then hiyo inakwenda mahakamani, unapewa samansi, unalazimishwa kupima DNA kama ni wewe, unawajibika kwa lazima, utake usitake!.

5. Kama Katiba imeruhusu jambo Fulani kufanyika, halafu katokea mtu kazuia na hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, unaulizia uhalali gani kwa rais kivuli?. Kila kitu ni halali!.

P.
 
Back
Top Bottom