Maswali juu ya Kiswahili

Mbiya

Member
Apr 4, 2008
7
1
Mimi ni mwanafunzi wa Kiswahili na nina maswali juu ya lugha.
"Bwana Amri Abedi aliandika mashairi yanayokuwa magumu."
Kwa nini sentensi hii si sawa? Nataka kuandika "Bwana Amri Abedi aliandika mashairi ambayo ni magumu", lakini ninahitaji kuiandika vingine. Unaisemaje?

II. Ninajaribu kuunga sentensi hizi kwa kutumia -ki-.
Niliwaona. Waliondoka ofisini.
> Jibu langu: Nikiwaona waliondoka ofisini.
Kwa nini sentensi hii si sawa? Labda ninaweza kuandika pia "Niliwaona wakiondoka ofisini", lakini sijui.

Asante sana!
 
Mbiya,

"Bwana Amri Abeid aliandika mashairi magumu" aliandika inaonyesha kuwa mashairi yaliandikwa katika wakati uliopita, magumu inaonyesha ugumu wa mashairi, usichanganye ali- na magumu ukafikiri ukisema ".. aliandika mashairi magumu" ugumu utakuwa katika wakati uliopita, hasha.

Ya pili,

"Niliwaona wakiondoka ofisini" yaani niliwaona wakifanya tendo la kuondoka ofisini.

Ninavyojua mimi.
 
Mimi ni mwanafunzi wa Kiswahili na nina maswali juu ya lugha.
"Bwana Amri Abedi aliandika mashairi yanayokuwa magumu."
Kwa nini sentensi hii si sawa? Nataka kuandika "Bwana Amri Abedi aliandika mashairi ambayo ni magumu", lakini ninahitaji kuiandika vingine. Unaisemaje?

katika sentensi yako ya awali (kwanza) unakabiriwa na tatizo ambalo ni rahisi sana kufanywa na anayejifunza kiswahili kama lugha ya pili lakini si rahisi kufanywa na mzungumzaji wa asili wa lugha hii. Hata katika sahihisho la sentensi hiyo bado kwa mbali unaweza kuona tatizo hilo.

Bwana Amri Abedi/ aliandika mashairi/ yanayokuwa/ magumu

Bwana Amri Abedi.. aliandika (kitendo hiki kilishafanywa) kwa hiyo msingi wa kauli hii ni tukio lililokwisha tokea. SI jambo linalotokea sasa.

aliandika mashairi yanayokuwa (Kitendo kinachotokea sasa, yaani wakati huu.

Hapa kuna tatizo la kwanza nalo ni la muda; je mashairi haya yanakuwa magumu sasa, au yalikuwa magumu alipoyaandika. Kama unachotaka kusema ni kutoa kauli ya uhakika kuwa mashairi yaliyoandikwa na Bw. Amri Abedi yalikuwa magumu basi neno "yanayokuwa" linaleta tafsiri tofauti. Kwamba mashairi yaliyoandikwa zamani (aliandika) yanakuwa magumu sasa. Kwa maneno mengine; wakati yalipoandikwa yawezekana yalikuwa rahisi, lakini siku hizi yanakuwa magumu. Hivyo hapa kosa si la mtunzi bali aidha la msomaji, mtafsiri, au kama nitakavyoonesha kwenye sehemu ya pili.

Tatizo la pili, ni tatizo la kutokukamilika kwa wazo (unconcluded idea).

Kwamba, tukichukulia kuwa ulichotaka kusema ndicho hicho kwamba haya mashairi yaliyoandikwa zamani yanayokuwa magumu basi hatuna budi kuuliza..

Magumu kwanini, magumu kwa namna gani, magumu kwa vipi, na magumu kinamna gani?

Hivyo, tukiacha neno "yanayokuwa" magumu litumike, basi kauli yako hiyo ingeweza kuwa sawa kabisa endapo wazo lingekamilishwa.

Kwa mfano, Bw. Amiri aliandika mashairi yanayokuwa magumu kueleweka na wasomaji, au yanayokuwa magumu kutafsirika; au yanayokuwa magumu kuimbika n.k n.k

Hivyo basi kusahihisha tatizo la kwanza, ungeliweza kabisa kusema hivi bila kumalizia wazo na watu wakakuelewa.

"Bw. Amri Abeid aliandika mashairi yaliyokuwa magumu." (bila ya shaka wazo litaendelezwa) au Bw. Amri Abeid aliandika mashairi magumu (hivyo "yaliyokuwa" haina ulazima kutumika.

II. Ninajaribu kuunga sentensi hizi kwa kutumia -ki-.
Niliwaona. Waliondoka ofisini.
> Jibu langu: Nikiwaona waliondoka ofisini.
Kwa nini sentensi hii si sawa? Labda ninaweza kuandika pia "Niliwaona wakiondoka ofisini", lakini sijui.

Asante sana!

Kwenye sentensi yako ya pili, unakabiriwa na tatizo la muda kidogo lakini pia la hali (situational).

Matumizi ya "ki" kama unavyotaka yanakutana na mambo mawili.

- Moja huashiria muda ujao. Km. Nikifika, nikienda, nikimaliza nikirudi n.k Hilo ni rahisi kuliona.
- Pili matumizi hayo ya "ki" huashiria pia shuku, hisia au jambo ambalo laweza kutokea au kutotokea. Km. nikimaliza hili nitafanya kile. Kwa maneno mengine, nisipomaliza hiki sitofanya kile. Hivyo kauli yako ya "nikiwaona wakiondoka ofisini" inaweza kuwa sawa lakini inahitaji kumaliziwa na kujenga wazo kamili kwa mfano, "nikiwaona wanatoka kazini, nitawafuata".

Sasa, nimesema hapo juu kuwa "ki" inaashiria muda ujao hivyo kauli yako ya awali inakinzana na wazo hilo pale unapotumia muda wa aina mbili:

"Nikiwaona (wakati ujao) waliondoka (wakati uliopita) hivyo kauli hiyo ni rahisi kusikika kwa makosa kwani huwezi kuwaona in the future wakifanya tendo la wakati uliopita.

Hivyo ulivyoisahihisha sentensi yako kwa kuondoa "ki" na kuweka "li" umeoanisha muda na hivyo unaposema "niliwaona wakiondoka". Na hapa kuna matumizi mengine ya "ki" katika madaraja yake saba.
Natumaini itakusaidia kidogo.
 
Walimu wa umu ndani..dogo kaniuliza maana ya aya maneno na methali moja..pls msaada.
*Kupwa*
*Birashi*
*Upepo wa miujiza*
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom