Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,110
Mods msiunganishe uzi. Mhe.Lukuvi awali ya yote nakupongeza kwa kutoa tamko la 'serikali' kuhusu tukio la bomu lilitokea Soweto, Arusha tar.15/06/2013 ambapo CHADEMA walikuwa wakihitimisha kampeni. Mheshimiwa; Kauli uliyoitoa leo bungeni imeniacha na maswali 6 kama ifuatavyo: Umesema tukio la Soweto ni sawa na lile la kanisani Olasiti, umejuaje? Unawaambia nini waumini wa kanisa Katoriki waliokuwa wanasubiri uchunguzi rasmi ukamilike na kutolewa? Umesema wananchi waliwazuia Askari kumkamata mhalifu je, walikula njama ili awadhuru ama kuwaua kabisa? Umesema unajua tukio la Soweto ni mwendelezo wa kuchochea ukabila,ukanda,udini,uchama na rangi.Sasa kwanini unatangaza 100/= mln kwa atakayetoa taarifa unazozijua? Umetutaka Watanzania tujiulize kwanini Arusha, je tusijiulize yaliyotokea Nyololo,Iringa mwaka jana alipouwawa Mwangosi? Ulipotuhumiwa na Mhe.Chiku Abwao ulibisha, umepataje taarifa ambazo IGP Mwema hana?