Maswali 11 yenye utata: BAKWATA ilianzishwa na nani?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Kwanza kabisa huu uzi sio wa nia mbaya yoyote ile nimeanza kulisema hili mapema waswahili wanasema kuuliza si ujinga tunauliza ili tujifunze na kwa nia ya kujipatia elimu na maarifa

Na mimi nimeona nijifanye sijuwi lolote ili nielimike.

Naombeni mnijibu maswali yafuatayo ambayo yananipa utata na yanawaacha watu na alama ulizo kichwani?

1. BAKWATA ilianzishwa na nani?

2. BAKWATA inafadhiliwa na nani?

3. Kwanini BAKWATA iwe ni baraza tu maana ya neno baraza navyoelewa ni kikundi cha watu wateuliwa kwajili ya jambo fulani na sio mamlaka kamili

4. Kwanini taasisi ya mwanzo ya waislam ya East Africa muslim welfare society ilipigwa marufuku nchini?

5. Ni nani aliye nyuma ya BAKWATA?

6. Kwanini ukiigusa BAKWATA umeigusa serikali na chama?

7. Je, ni kweli kwamba BAKWATA ni tawi la chama fulani?

8. Je, ni kweli kwamba Baba wa taifa alianzisha BAKWATA kwa kutumia usalama wa taifa

9. Miaka 50 ya BAKWATA kwanini hawajafanya maendeleo yoyote kwa waislam huku taasisi ndogo na changa kama islamic foundation tayari muda mfupi tu wana TVs na redio na mashule ya kisasa?

10. Kwanini BAKWATA mara nyingi husimamia upande wa serikali au chama fulani tu?

11. Kwanini BAKWATA ipo kama vile sio kwa ajili ya watu husika inayopaswa kuwasimamia ipo kama vile ipo kinyume nao?

MY TAKE: nimehoji hayo kama kujifunza wala sijahoji kwa nia mbaya, sote tupo hapa JF kujifunza na sio mengineyo
 
Waswahili wa pwani ndio wapigania uhuru nchi yetu!wazungu wakashtuka wakamwandaa kijana wao kambarage ashike hatamu chini ya kanisa katoliki!!Sasa waswahili walipogundua wameingizwa chaka wakaanzisha Bakwata yao!!Serikali-kanisa ikaiua Bakwata ile ikaleta Bakwata-kanisa-serikali hii iliyopo!!!
 
Waswahili wa pwani ndio wapigania uhuru nchi yetu!wazungu wakashtuka wakamwandaa kijana wao kambarage ashike hatamu chini ya kanisa katoliki!!Sasa waswahili walipogundua wameingizwa chaka wakaanzisha Bakwata yao!!Serikali-kanisa ikaiua Bakwata ile ikaleta Bakwata-kanisa-serikali hii iliyopo!!!
Aisee
 
Acheni kuliamsha jinamizi la udini, tena shikeni adabu kwa dude hilo. Ashukuriwe Mungu nchi haiongozwi kwa misingi ya dini fulani. Watu wana uhuru wa kuabudu imani waiaminiaye, kuchokonoa udini hauna tija kwa taifa la sasa
 
Mijadara ya udini mara nyingi hujadiliwa na Masikini sijui kwanini.

Iyo Bakwata haijengi barabara, haikupeleki mbinguni, haijengi hospital, haileti maji wala haiwezi kukuajili.
Kwanini sasa unapotaka bakwata iundwe upya kwa muundo wautakao waislam wenyewe huishia kutishiwa nakuitwa wanaleta chokochoko za kidini.Kwanini serikali inakataza waislam kujiundia chombo chao huru?Maana hii haijulikani iliundwa na nani hasa na kwa malengo gani.
 
navyojua kulikuwa na taasisi ya waislamu kabla ya Bakwata, ilivunjwa na awamu ya kwanza na kuzuka Bakwata kama political wing ya CCM ( kwa mtazamo wangu)...ilianzishwa Bakwata ili kuwacontain waislam kwa maana ya Bakwata ni kama mali ya serikali tu na waislam hawawezi kuwa huru kupanga mipango yao....
 
Back
Top Bottom