Maswali 10 jk aliyoulizwa kwenye acount yake fb but hajatolea majibu mpk sasa!

NYAGI DRY

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
368
155
Jakaya Kikwete Baadhi ya ujumbe/maoni toka
kwenu: 1."Hello Rais wangu. Serikali
kwa sasa sio sikivu tu bali
imekuwa na upole uliopitiliza
kiasi kwamba wanasiasa
uchwara na wanaharakati
uchwara wanaitumia nafasi hiyo vibaya.Serikali ikiendelea
kuwa kimya katika hili ni
hatari kwa mustakabali wa
Taifa letu. Freedom of speech ni
kubwa mno. Mungu ibariki
Tanzania. Kazi njema." (Max) 2."Sometime people talk
without thinking critically but I
belive you are the best may God
help you and our
nation." (Mathew) 3."Posho za Wabunge toka
70,000 TZS hadi 200,000TZS ni
mzigo kwa wananchi, tafadhali
simamia jambo hili mapema.
Tuangalie na sisi waalimu pia.
Hali yetu ni mbaya sana." (Salim) 4."Ajira baba, ajira. Elimu zetu
hazitufundishi ujasiriamali.
Tunamaliza masomo na kukosa
ajira. Tumejazana mitaani.
Tumia miaka iliyobaki
kututatulia tatizo hili." (Gratian) 5."Hivi suala la umeme
limefikia wapi? Ki ukweli
naona wizara imeshindwa
kupata ufumbuzi wa kudumu.
Mbona tuko nyuma sana?
Hakuna vyanzo vingine?" (Mabula) 6. "Mr. President, I am an
engineer, have some ideas that
can help in solving the
electricity problem. How do I
reach you?" (Sameer) 7."Mheshimiwa Rais pole na
kazi. Hivi suala la Katiba
limefikia wapi? Kwa nini
tunahitaji Katiba mpya?
Naomba usimamie utoaji wa
elimu kuhusu Katiba. Nina wasiwasi wananchi
tutaburuzwa na ninyi
wachache, wanasiasa na
wasomi katika suala la katiba,
wengi hatujui nini kinaendelea.
Asante." (Ibrahim) 8. "Tafadhali dhibiti uhuru wa
kutoa maoni. Imekuwa too
much sasa. Watu wanautumia
vibaya. Ni hilo tu kwa
leo." (Halima) 9."Mpango wa shule za kata
unakosa waalimu makini na
vifaa bora Mheshimiwa Rais,
shule zipo sawa lakini je hizi
changamoto za waalimu na
vifaa zinakabiliwa kwa wakati?" (Sandra) 10. "Hallow Mr President, I
should first congratulate you for
using Facebook media, for this
enables people to interact with
you freely. The Legal and
Human Rights centre have posted a video, depicting
actions of police brutality in
Iringa. I think the police
involved should be brought to
justice." (Abdallah)
 
nasikia account sio yake bali kuna mtu anatumia alama ya kikwete kujitambulisha FB
 
Mambo ya teknolojia lolote linawezekana. kuna jamaa yangu mwingine wa huko huko Ikulu aliniambia Rais alifungua account FB lakini hana muda wa kuingia huko hivyo kuna watu wanacheza na akaunti yake pasipo yeye kufahamu kwa hiyo hata kinachoandikwa huko hakijui. wasiliana na invisible akupe namba ya JK ya mkononi inayotumika kwa wananchi au peleka maswali pale getini Ikulu wanapokea.
 
thread yako inachosha kuisoma haina mpangilio wa maswali kuanzia swali la kwanza na la mwisho huwezi kujua wapi swali moja linaanza na kuishia pengine ndio sababu hata majibu hayajapatikana kutoka kwa JK.
 
Huyo Halima anayemwambia adhibiti uhuru wa kuongea nae ndio walewale ambao wanasababisha hii nchi haiendelei!
 
Back
Top Bottom