Maswa: Wakazi elfu 10 kunufaika na mradi wa maji wa Rais Samia wa Isulilo

Ze Bulldozer

JF-Expert Member
Jun 12, 2020
998
520
MRADI wa Maji ya bomba wa kijiji cha Isulilo katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kuwanufaisha wananchi wapatao 10,497.

Mradi huo unatekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) kwa ufadhili wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan,

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Maswa,Mhandisi William Boniphace alisoma taarifa ya mradi huo kwa wajunbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Simiyu amesema kuwa wananchi watakaonufaika ni wa vijiji vya Isulilo,Mwamihanza na Ngingwa.

Mhandisi Boniphace amesema kuwa hadi sasa kazi zilizofanyika katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa Lita 90,000 katika mnara wa mita 15,Ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji,Ununuzi wa pampu za kusukuma maji na Ulazaji wa bomba umbali wa Kilomita 15.426

Akielezea gharama za Mradi huo amesema kiasi cha Sh 462,813,735 zimetumika katika mradi huo na tayari chombo cha watoa huduma ya maji ngazibya jamii kimeundwa na kusajiliwa kwa lengo la kuufanya mradi huo kuwa endelevu.

Aidha Mhandisi Boniphace ameeleza kuwa mpango mkakati wa Ruwasa ni kuongeza huduma ya maji kwa kupeleka katika kijiji cha Kidema na hiyo imewekwa kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoa wa Simiyu,Emanuel Gungu Silanga ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa kamati hiyo iliyotembelea mradi huo aliipongeza Ruwasa kwa utekelezaji wa mradi huo.

Sambamba na pongezi hizo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walitoa ushauri kwa Ruwasa kuangalia gharama za kuwauzia wananchi maji kwa ndoo moja ziwe za chini ili wananchi wengi waweze kunufaika na mradi huo ambao tayari umeanza kutumika.

photo_2021-12-22_10-49-18.jpg
 
Upuuzi mtupu, mradi wa mama Samia katoa wapi pesa? Acheni siasa za kiupambe, ndio maana viongozi wanavimba vichwa na kuishia kuiba kuiba kwa ajili ya hizi sifa za kijinga.
 
Mkuu tatizo ni nini? Rais Samia ndio kiongozi mkuu wa Serikali tukisema kafanya yeye tunakosea nini?
 
Wakati wao walikuwa busy kwenda Dubai kutafuna ruzuku za chama, makato ya wabunge wao waliokuwa wakiwakata kila mwisho wa mwezi, kula mamilioni ya Sabodo na wengineo, kutafuna michango ya wanachama wao bila kujali umasikini wao.

Kwa upande wa serikali hali ni tofauti. Neema imetamalaki kila kona shule zinajengwa na kuboreshwa, hospitali zinaongezwa, barabara zinasogezwa mpaka vijijini, tatizo la umeme na maji linazidi kutokomezwa nk.

Huu ndio uongozi wa kweli na sio ule wa changa la macho. Sisi kama watanzania wenye maono, hatuwezi kukubali kutawaliwa kwa njia ya "Wajinga Ndio Waliwao"

2528007_20200919_173148.jpg
 
Mkuu tatizo ni nini? Rais Samia ndio kiongozi mkuu wa Serikali tukisema kafanya yeye tunakosea nini?
Unakosea ze bulldozier, angalau sema sirikali, ingeleta mantiki, huo ni upambe uchawa, unaa Kwa lugha nyingine kupaka mafuta Kwa mgongo wa chupa.
 
We mama unatuchosha na nyuzi zako za kujitukuza kwa kutumia majina mbalimbali, tumeishakugundua
 
MRADI wa Maji ya bomba wa kijiji cha Isulilo katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu kuwanufaisha wananchi wapatao 10,497.

Mradi huo unatekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) kwa ufadhili wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan,

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Maswa,Mhandisi William Boniphace alisoma taarifa ya mradi huo kwa wajunbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Simiyu amesema kuwa wananchi watakaonufaika ni wa vijiji vya Isulilo,Mwamihanza na Ngingwa.

Mhandisi Boniphace amesema kuwa hadi sasa kazi zilizofanyika katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa Lita 90,000 katika mnara wa mita 15,Ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji,Ununuzi wa pampu za kusukuma maji na Ulazaji wa bomba umbali wa Kilomita 15.426

Akielezea gharama za Mradi huo amesema kiasi cha Sh 462,813,735 zimetumika katika mradi huo na tayari chombo cha watoa huduma ya maji ngazibya jamii kimeundwa na kusajiliwa kwa lengo la kuufanya mradi huo kuwa endelevu.

Aidha Mhandisi Boniphace ameeleza kuwa mpango mkakati wa Ruwasa ni kuongeza huduma ya maji kwa kupeleka katika kijiji cha Kidema na hiyo imewekwa kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoa wa Simiyu,Emanuel Gungu Silanga ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa kamati hiyo iliyotembelea mradi huo aliipongeza Ruwasa kwa utekelezaji wa mradi huo.

Sambamba na pongezi hizo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walitoa ushauri kwa Ruwasa kuangalia gharama za kuwauzia wananchi maji kwa ndoo moja ziwe za chini ili wananchi wengi waweze kunufaika na mradi huo ambao tayari umeanza kutumika.

View attachment 2053248
Safi Sana Rais Samia, Hakuna kama wewe, Chapa kazi mama yetu,
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom