Masuali mawili muhimu kuhusu muungano wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masuali mawili muhimu kuhusu muungano wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Macos, Jun 1, 2012.

 1. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  nataka niulize masuali mawili kuhusu huu muungano wa nchi huru mbili zilizoungana "kwa hiari"
  naoma kila mtu ajaribu kujibu bila ya jazba wala chuki, tujaribu kuwa great thinkers wa sawa sawa.

  1. suali la kwanza-jee kama watanaganyika kwa wingi wao na umoja wao wakisema na kuamua kwamba hatutaki kuendelea na muungano tunataka tanganyika yetu na bunge dodoma lipitishe azimio hili jee wazanzibar watakua na uwezo,nguvu,na haki ya kisheria kuzuia jaribio hili?
  2. suali la pili -jee wazanzibari kwa wingi wao na umoja wao wakisema muungano basi na baraza la wakilishi likapitisha hoja hii na kura ya maoni ikaamua ijitoe , jee tanganyika itakubali zanzibar ijitoe? Jee itaridhia bila ya kutumia nguvu kwa kupeleka jeshi huko zanzibar kuzuia jaribio hilo?

  naomba mjadala wa kina bila jazba kwani naamini jawabu zitatupa picha kamili ya aina ya muungano tulio nao
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ili Muungano uvunjike/usivunjike ni lazima wale walioungana kwa pamoja wajadili kuhusu huo muungano wao,
  Lakini kama mmoja kati ya wawili walioungana haridhiki na muungano wao si dhambi kujiengua la pasitokee yule anaeridhika akamzuia asieridhika kuondoka,
  kama ilivyokuwa hiyari wakati wa kuungana vivo hivyo ni hiyari pia kutengana,kwa kesi ya Tanganyika na Zanzibar katika kuungana majority wa pande zote mbili hawakuhusishwa hivyo basi wakati na zamu ya majority kuhusika juu ya Muungano unaowahusu kwa 100% Umefika , yangu ndo hayo Comrade Macos.

  1/Zanzibar watakuwa na haki ya kuuzuia lakini nguvu sina hakika sana kama watakuwa nayo.

  2/Kwa utamaduni ulioko hapa Bara wa kutumia mabavu ni dhahili watapeleka jeshi kuzima hilo jaribio
   
Loading...