Masuala na Maswali kwa Ofisi ya Rais na Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Jana nilitoa "Tamko kwa Vyombo vya Habari kuhusu Taarifa ya Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma" ( Unaweza kulisoma tamko lote hapa: http://mnyika.blogspot.com/2010/03/tamko-la-mnyika-kuhusu-taarifa-ya-smvu.html). Kutoka katika tamko hilo naomba kuwapatia 'Masuala na Maswali kwa Ofisi ya Rais na Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma' tuyajadili.

Mosi; Watanzania wenzangu na mamlaka husika zizingatie kwamba msingi wa tuhuma nilizotoa tarehe 19 Februari 2010 kuhusu Mkapa kufanya biashara Ikulu, matumizi mabaya ya madaraka katika mchakato wa Kiwira na kutokutoa taarifa za mali zake zote na madeni yake baada ya kutoka madarakani ni kutolewa kwa tuhuma hizo mara kadhaa mwaka 2006, 2007, 2008 na 2009 bila kutolewa majibu kamili na Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma au Rais Mstaafu Mkapa mwenyewe. Tuhuma kuwa Rais Mstaafu hakutaja mali zake zilianza kutolewa bungeni na Fatma Maghimbi (Mb) wakati akichangia mjadala kuhusu Hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa tarehe 30 Disemba 2005 wakati akizundua bunge. Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma haikutoa tamko wakati huo. Viongozi wengine waliowahi kutoa tuhuma hiyo hadharani na kunukuliwa na vyombo vya habari ni pamoja na: Profesa Ibrahim Lipumba (Tanzania Daima-20/04/2008); Profesa Mwesiga Baregu (Mwananchi-21/11/2009). Aidha taarifa kwamba Rais Mstaafu Mkapa hajawahi kutangaza mali zake baada ya kutoka madarakani ziliandikwa pia na wanahabari kadhaa mathalani: Rai (12/1/2006); Tanzania Daima (01/04/2009) nk. Hivyo, Sekretariati ya Maadili ya Umma inapaswa kueleza Rais Mstaafu Mkapa alijaza lini hasa tamko juu ya mali zake? Na kwanini Sekretariati haikutoa taarifa katika kipindi chote toka mwaka 2006 pamoja na tuhuma hiyo kuandikwa na vyombo mbalimbali vya habari mpaka pale Gazeti la Jambo Leo lilipozirudia katika toleo lake la Jumapili tarehe 21 Februari 2010 ? Tamko la Sekretariati limekidhi sehemu ya matakwa ya sheria husika lakini halijakidhi mahitaji ya umma na misingi ya uwajibikaji hivyo, kupitia tamko hili natoa mwito wa Rais Mstaafu Mkapa mwenyewe kutaja mali zake hadharani kama sehemu ya ‘ukweli na uwazi’ ambao amekuwa akihimiza toka mwaka 1995 alipoingia madarakani katika kipindi chake cha kwanza cha Urais.

Pili; kwa kuwa Sekretariati ya Maadili ya Umma imejitokeza rasmi kutoa kauli ya kujibu kwa niaba ya Rais Mstaafu Mkapa, naiomba ijibu maswali yafuatayo ambayo umma umekuwa ukijiuliza na yako ndani ya mamlaka ya sekretariati husika kuyazungumzia: Je, Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma imehakiki mali zote na madeni ya Rais Mkapa ili kuthibitisha usahihi na ukweli wa taarifa zilizowasilishwa? Je, mali zilizotajwa zinajumuisha pia mali zinazotajwa kumilikiwa na Rais Mkapa na mkewe zikihusishwa na tuhuma mbalimbali za kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma mathalani kufanya biashara Ikulu kupitia kampuni ya ANBEN, kujiuzia bei chee mgodi wa umma katika kashfa ya Kiwira ambayo Rais Mkapa alitajwa kuwa mmoja wa wanahisa? Je, Sekretariati ilichukua hatua gani baada ya tuhuma hizo kutolewa hadharani na kwenye mamlaka mbalimbali ikiwemo bungeni zikihusisha pia kukiuka kifungu 12(1)(a) kinachokataza kiongozi kutumia taarifa zinazopatikana kwenye uongozi wa umma kwa manufaa binafsi? Suala hili linahusu pia tuhuma dhidi ya Andrew Chenge (Mb) katika kashfa ya Rada zinahusu pia kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa umma kifungu 12(e) kwa kupokea maslahi ya kiuchumi wakati wa manunuzi na mikataba. Sekretariati imepewa mamlaka kwa mujibu wa sheria husika kifungu 18(4) kuanzisha na kufanya uchunguzi wa tuhuma hata kama hakuna mtu aliyekwenda kuwasilisha malalamiko rasmi na pia inaweza kuchunguza tuhuma hata zilizotoka kwenye vyombo vya habari kwa mujibu wa kifungu 22(4). Hivyo, Sekretariati inapaswa kueleza umma toka tuhuma zitolewe hadharani kupitia Orodha ya Mafisadi (List of Shame) Septemba 15 mwaka 2007 uchunguzi gani imeukamilisha na hatua kuchukuliwa kwa watajwa wote? Izingatiwe kuwa pamoja na uchunguzi wa awali unaoweza kufanywa na Sekretariati kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 kifungu 22(2); uchunguzi kamili unafanywa na baraza ambalo kwa mujibu wa kifungu 26(5) linapaswa kufanya uchunguzi wake hadharani ili umma uweze kufahamu.

Tatu; Sekretariati itoe taarifa ya kueleza bayana imechukua hatua gani kwa viongozi wa umma ambao hawajataja mali na madeni yao au wametoa taarifa za uongo kama ilivyoelezwa kwa miaka kadhaa na sekretariati yenyewe pamoja na Ofisi ya Rais ( Rejea- Habari Leo 12/1/2007, 26/1/2007; 29/1/2007; Mwananchi 18/09/2007 na taarifa zingine zilitolewa kwenye vyombo vya habari mwaka 2008 na 2009). Aidha ikumbukwe kwamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia wakati akiwasilisha makadario ya bajeti ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2008/2009 alitoa ahadi kuwa Serikali ingewachukulia hatua za kisheria viongozi wa umma 3,186 kwa kuwa hawakurudisha fomu za tamko la mali. Pia, Taarifa ya Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne katika kipindi cha miaka mitatu iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais(Utawala Bora)-Sofia Simba mwaka 2008 ilisema kwamba serikali inachunguza baadhi ya viongozi baada ya kubaini wana mali zaidi ya walizotaja kwenye fomu baada ya kuhakiki mali za viongozi 260 tu kati ya viongozi zaidi ya 7000 ambao ilipaswa kuhakiki mali zao. Sekretariati ni muhimu pia ikatoa taarifa ya kuuleza umma kwanini haikagui mali za viongozi wote kama inavyohitajiwa kwani hapo kabla iliwahi kueleza kupitia kwa kamishna wake mkuu kwamba ina uhaba wa fedha za kuweza kutekeleza kwa wakati zoezi hilo la kisheria ( Habari Leo- 18/09/2007). Badala ya kutumia fedha nyingi za walipa kodi kwenye kutoa matangazo ya maneno ni muhimu kwa sekretariati kuwekeza katika kufanya vitendo vya uhakiki, uchunguzi na kuchukua hatua stahili kwa manufaa ya umma. Sekretariati ikumbuke kuwa Rais Kikwete aliagiza toka mwaka 2007 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM kwamba mali zote za viongozi wa umma zitahakikiwa na kuchunguzwa badala ya utaratibu wa zamani wa kuorodhesha tu kwenye daftari.

Nne; Natambua kwamba Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewaelekeza wahariri na wanasiasa wa aina ya “Mnyika” kuwasiliana na uongozi wa sekretariati ili kupata taarifa za mali na madeni ya viongozi. Kabla sijatoa tamko la kukataa ama kukubali maelekezo hayo kuna masuala ambayo wahariri na wanasiasa ambao Sekretariati imewabatiza jina la ‘aina ya Mnyika’ ni lazima tukapatiwa ufafanuzi. Sekretariati ituhakikishie kwamba hata baada ya kupitia taarifa za kumbukumbu hizo za mali na madeni ya viongozi tutaendelea kutumia uhuru wetu wa kikatiba wa haki ya kupata na kutoa taarifa kama ulivyotolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 18 vipengele (a) (b) (c) (d) badala ya kuzibwa mdomo kutoendelea kuzungumzia mali hizo baada ya kukagua daftari. Izingatiwe kuwa Waziri mwenye dhamana kwa mamlaka aliyopewa na Sheria kifungu 20(3) alishatunga kanuni zenye vipengele 6(1) (2) na 7(2) (c) vinavyokataza mwananchi kuzizungumzia popote taarifa hizo baada ya kuzikagua . Kwa upande mwingine, sekretariati ituhakikishie kwamba itatoa taarifa zote kwa wakati kwa kadiri ya tukavyohitaji kwa sababu kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kifungu 20(1)(2) taarifa zote zinapaswa kuingizwa kwenye daftari ambalo linaweza kukaguliwa na umma kwa nyakati zote zinazofaa. Hivyo Sekretariati itoe kwanza tamko kuwa imefikia wapi kuwaruhusu Viongozi wa Vyama vya Upinzani ambao kwa barua yenye kumbukumbu CCTN/TC/DSM/UF/2008/002 ya mwezi Aprili 2008 waliomba kukagua matamko ya mali za viongozi hususani waliotuhumiwa kwa ufisadi lakini mpaka sasa inakaribia miaka miwili sekretariati haijaruhusu daftari la mali husika kukaguliwa likiwemo tamko la Rais Mstaafu Mkapa . Ikumbukwe kwamba viongozi wa vyama walikwenda kwenye Sekretariati na kutimiza masharti yote ikiwemo kujaza fomu na kufanya malipo ya ada ya ukaguzi; Sasa Sekretariati inawahakikishia kwa kiasi gani wahariri na wanasiasa ‘aina ya Mnyika’ kwamba tukienda hivi sasa tutapatiwa taarifa kuhusu Mkapa na wengine ama utakuwa ni mwendelezo mwingine wa kufunika mijadala ya umma kwa kisingizio cha kusubiria ‘taarifa sahihi’ kutoka kwenye sekretariati hiyo?. Wakati tukisubiria maelezo na maelekezo ya ziada toka Sekretariati ya Maadili ya Uongozi wa Umma tutaendelea kuandika na kuzungumza kuhusu suala hili kama sehemu ya kuhamasisha uwajibikaji wa viongozi na kutetea rasilimali za taifa.

JJ
 
What next kama wakikataa? John let be serious, hatuwezi kusikia kila siku unaandika tuuuu. We need the way forward.
 
What next kama wakikataa? John let be serious, hatuwezi kusikia kila siku unaandika tuuuu. We need the way forward.

Selous,

Hili sio suala binafsi la "Mnyika" dhidi ya "Mkapa", ni suala la "Umma" dhidi ya "Viongozi wa Umma"; baada ya kusema hapa naamini hata wewe Selous unaweza kupendekeza nini kifanywe na watanzania kama ishara ya kuwa serious kama ulivyoelekeza. Ukisoma vizuri tamko langu unaona nimegusia kuhusu way forward, wakati naelezea malengo ya muda mfupi na malengo ya muda mrefu. Nilizungumza kwa kirefu zaidi kwenye kipindi cha Kipamajoto ITV; mengine sijaweka hapa kwenye kipindi cha kuwa nilichukua tu yaliyohusiana na kujibu Taarifa ya Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

JJ
 
JJ,
Naelewa kabisa kuwa hili ndo letu lakini tumelia weeee pasipo kwenda mbele. labda niulize, sheria inasemaje kama hujibiwi? Dr Slaa amesema suala la richmond tutalipeleka kwa wananchi, mnajua operation sangara imeishia wapi? Je, tabora na shy si ndio maeneo yaliolala kifikra (samahanini sana watakaojisikia vby)? hamuoni is better to go there, change them. Halafu waamke hata siku tukisema tunaandamawataandama kwa wingi tu. Show me the way, will be ther to help as usual.
 
JJ,
Naelewa kabisa kuwa hili ndo letu lakini tumelia weeee pasipo kwenda mbele. labda niulize, sheria inasemaje kama hujibiwi? Dr Slaa amesema suala la richmond tutalipeleka kwa richmond, mmnajua operation sangara imeishia wapi? Je, tabora na shy ndo maeneo yaliolala kifikra (samahanini sana watakaojisikia vby)? hamuoni is better to go there, change them. Halafu waamke hata siku tukisema tunaandama tutaandamana tu. Show me the way, will be ther to help as usual.

Selous

Asante kwa maoni yako. Dr Slaa alisema tunapeleka mashtaka kwa wananchi kwa kuwa ndio wenye mali. Kama ilivyofanyika wakati ule walipoiwekea mizengwe hoja ya BOT bungeni na kumsimamisha Zitto wakati wa hoja ya Buzwagi. Tulipeleka mashtaka kwa umma kupitia ziara iliyoishia Septemba 15 Mwembeyanga ambapo Orodha ya Mafisadi ilisomwa. Naamini unajua matokeo ya tendo lile kwenye medani nzima ya utawala katika taifa letu.

Nashukuru umependekeza mikoa ya kwenda Sangara. Pamoja na kuwa tungependa kwenda Shinyanga kwa sasa, zingatia kuwa kuna mvua nyingi huko kwa sasa. Hivyo, tija ya ziara inaweza isiwe kwa kiwango kinachokusudiwa. Naamini vikao vya chama vitatoa mwelekeo wa wapi tunakwenda na tunakwenda lini. Lakini ni dhamira yetu kufika maeneo mengi kadiri iwezekanavyo hususani yale ya vijijini kabisa ili kufikisha elimu ya uraia, kuhamasisha uwajibikaji na kutetea rasilimali za taifa wakati huo huo tukitoa sera mbadala na kujenga oganizesheni ya chama mbadala.

Tunachoomba ni mchango wako na wa wengine wa hali na mali katika kufanikisha harakati hizi. Pamoja Tutashinda.

JJ
 
JJ,

Hebu weka tena hapa ile namba ya simu KUCHANGIA CHADEMA ili tuwezee kushirikii...

Ningependaa kuchangiaa leooo....
 
JJ,

Hebu weka tena hapa ile namba ya simu KUCHANGIA CHADEMA ili tuwezee kushirikii...

Ningependaa kuchangiaa leooo....

Nyauba,

Tuma neno CHADEMA kwenda namba 15710 iwapo una mtandao wa Zain au Vodacom kwa sasa. Asante kwa kuchukua hatua kuwa wakala wa mabadiliko unayotaka kuyaona.

JJ
 
Nyauba,

Tuma neno CHADEMA kwenda namba 15710 iwapo una mtandao wa Zain au Vodacom kwa sasa. Asante kwa kuchukua hatua kuwa wakala wa mabadiliko unayotaka kuyaona.

JJ

Kila ninapotuma naambie wewe ni mwanachama namba xyxyx. Hamuwezi kudesign maneno hata nukuu za Mwl J.K sio wa CCM huyu ni Baba wa Taifa au hata maneno yenye kuchochea. Hii itasaidia watu kuchangia zaidi. Nimewasikia watu kama kumi hivi wanalalamika kuwa "yale yale".
 

Tuma neno CHADEMA kwenda namba 15710 iwapo una mtandao wa Zain au Vodacom kwa sasa. Asante kwa...


JJ

Na ndo maana hatuendelei; hata kwenye dirisha la kukusanya ada mbali mbali kama TRA, DAWASCO, mahakama, Luku, n.k. unakuta hakuna mtu dirishani. Ndio vyanzo vya mishahara yao halafu wanaringa kupokea.

Mtu anaomba contacts za kuchangia CHADEMA, anaambiwa lazima awe na simu ya Voda au Zain!
 
Na ndo maana hatuendelei; hata kwenye dirisha la kukusanya ada mbali mbali kama TRA, DAWASCO, mahakama, Luku, n.k. unakuta hakuna mtu dirishani. Ndio vyanzo vya mishahara yao halafu wanaringa kupokea.

Mtu anaomba contacts za kuchangia CHADEMA, anaambiwa lazima awe na simu ya Voda au Zain!

Asante. Ameomba namba ya kuchangia CHADEMA, naamini alimaanisha 15710 kwa wateja wa Zain na Vodacoma kama nilivyompa. Angeomba contacts ningempatia contacts, angeomba account number ningempatia pia. Na wewe unaomba nini?

Turejee kwenye mjadala kuhusu tamko husika.

Siku njema

JJ
 
Selous

Asante kwa maoni yako. Dr Slaa alisema tunapeleka mashtaka kwa wananchi kwa kuwa ndio wenye mali. Kama ilivyofanyika wakati ule walipoiwekea mizengwe hoja ya BOT bungeni na kumsimamisha Zitto wakati wa hoja ya Buzwagi. Tulipeleka mashtaka kwa umma kupitia ziara iliyoishia Septemba 15 Mwembeyanga ambapo Orodha ya Mafisadi ilisomwa. Naamini unajua matokeo ya tendo lile kwenye medani nzima ya utawala katika taifa letu.

Nashukuru umependekeza mikoa ya kwenda Sangara. Pamoja na kuwa tungependa kwenda Shinyanga kwa sasa, zingatia kuwa kuna mvua nyingi huko kwa sasa. Hivyo, tija ya ziara inaweza isiwe kwa kiwango kinachokusudiwa. Naamini vikao vya chama vitatoa mwelekeo wa wapi tunakwenda na tunakwenda lini. Lakini ni dhamira yetu kufika maeneo mengi kadiri iwezekanavyo hususani yale ya vijijini kabisa ili kufikisha elimu ya uraia, kuhamasisha uwajibikaji na kutetea rasilimali za taifa wakati huo huo tukitoa sera mbadala na kujenga oganizesheni ya chama mbadala.

Tunachoomba ni mchango wako na wa wengine wa hali na mali katika kufanikisha harakati hizi. Pamoja Tutashinda.

JJ


Mvua mwaka huu ni kidogo sana kulingalisha na miaka mingine. Kule hakuna mafuriko, na pia hazinyeshi mvua kama kule milima ya tanga, bukoba na mbeya. Plz hii sio sababu ya mshiko.
 
Mvua mwaka huu ni kidogo sana kulingalisha na miaka mingine. Kule hakuna mafuriko, na pia hazinyeshi mvua kama kule milima ya tanga, bukoba na mbeya. Plz hii sio sababu ya mshiko.

Selous,

Kabla ya kwenda mahali huwa tunawasiliana na viongozi wetu wa ngazi za chini kwa ajili ya maandalizi. Hiyo ndio hali halisi waliyotuambia. Lakini zingatia kuwa sizungumzii kwenda Mkoa au makao makuu ya wilaya, nazungumzia kwenda vijijini kabisa ambao barabara ni shida. Maeneo kama hayo kwenda wakati wa mvua kwa ajili ya kwenda ziara ya kijiji kwa kijiji huwezi kupata tija inayokusudiwa; mvua ikinyesha watu hawaji mikutanoni lakini pia magari hukwama na tija hupungua. Nimewahi kufanya ziara wakati wa mvua, ratiba huwa zinavurugika sana. Kwa hiyo unless uniambie wewe sasa hivi uko kwenye vijiji vyote vya wilaya zote za Shinyanga unisibitishie kuwa hakuna mvua!. Pamoja na hayo, nimekwambia kuwa vikao vya chama ndio vinaamua Sangara iende wapi; na mamlaka husika zitatangaza tutakwenda wapi very soon. Ila jambo moja ni kuhakikishie Sangara itaendelea karibuni, na lengo letu ni kwenda maeneo mengi ya nchi yetu kadiri iwezekanavyo ikiwemo Shinyanga uliyoitaja.

NB: Turejee kwenye mjadala wa thread hii, ambao unahusu Tamko kuhusu Taarifa ya Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa umma.

JJ
 
Nadhani serikali kulifumbia macho hili suala litaendelea kuwa kawaida.Kuna uwezekano hata JK mwenyewe akitoka hataweza kuifuata hii sheria

Sasa serikali aidha iamue kulitolea tamko hili suala,kuchukua hatua au kutangaza na kuia hii sheria.Hakuna maana ya kuwa na sheria ambayo haifuatwi,leo hii mtu ukifikiria mbali unaweza ona hata sheria zingine hazina maana simply kwa kuwa wamepuuza na wamekua comfortable kuona sheria fulani haifuatwi

Sijui hata ni kwa nini wanaendelea kutunga sheria nyingine kama hii ya matumizi ya pesa kwenye chaguzi,nina mashaka na dhamira yao njema
 
Hivyo, Sekretariati ya Maadili ya Umma inapaswa kueleza Rais Mstaafu Mkapa alijaza lini hasa tamko juu ya mali zake? Na kwanini Sekretariati haikutoa taarifa katika kipindi chote toka mwaka 2006 pamoja na tuhuma hiyo kuandikwa na vyombo mbalimbali vya habari mpaka pale Gazeti la Jambo Leo lilipozirudia katika toleo lake la Jumapili tarehe 21 Februari 2010 ? Tamko la Sekretariati limekidhi sehemu ya matakwa ya sheria husika lakini halijakidhi mahitaji ya umma na misingi ya uwajibikaji hivyo, kupitia tamko hili natoa mwito wa Rais Mstaafu Mkapa mwenyewe kutaja mali zake hadharani kama sehemu ya ‘ukweli na uwazi’ ambao amekuwa akihimiza toka mwaka 1995 alipoingia madarakani katika kipindi chake cha kwanza cha Urais.
wanapenda kusafisha visivyosafishika, ili umsafishe mkapa inabidi nawe ukubali kuchafuliwa na takataka alizonazo....kaazi kwelikweli
 
Back
Top Bottom