Master j, madam rita na salama siku za kuaibishwa na kulia zaja

Kiukweli hiyo BSS ni magumashi tu! Sijaona hata mmoja aliyetoka kimaisha baada ya kuwa mshindi!
Usanii tu!
 
. Kwa nini usiwe unahusisha majaji wengine wataalamu wa muziki toka Bagamoyo ili kuwa objective & transparent? why always rafiki zako akina master J na Salama ambaye hana sifa yoyote na muziki isipokuwa kuwashushua watu walivyovaa au kuwambia watafute kazi nyingine lugha za kihuni sana kwa vijana wanaotafuta kujiendeleza kimziki.
Kuna jaji alikuwepo kabla ya Kitine, miaka ile inaanza anza, yule jamaa alikuwa mhindi na kwa kutokea kwenye namna alivyokuwa akisahili alionyesha kuwa mjuaji sana wa music.
Ye ndiye alimgundua na kumtetea Reah Moudy kipindi kile wakati wakina Madam Rita wamemkataa.

Yule Mhindi sijui yupo wapi, naamini alikuwa jaji mzuri sana japo inaonekana alikuwa yupo tofauti sana na hao wengine ambao wapo mpaka sasa....

BSS haionekani kama ni watu wanaojua sana wanachokitaka kwanzia majaji mpaka mpangilio wa kiutawala wa hiyo biashara...
Kitu cha kujiuliza ni kimoja tu, Cocacola walifanya Popstar search moja tu na cheki mpka leo hii vile vipaji vinang'ara afrika mashariki yote ila hawa ndugu zetu wanakuja na hii kitu yao mwaka wa tano sasa na hamna kinachoeleweka zaidi ya kuona kuwa watu wanaimba-imba tu!!
 
Hawa wameshaandaa mshindi toka kitambo, kura ni kuzuga tu!! siwezi poteza credit yangu kwa upuuzi huu!
 
Ila siku alipotoka Norman niliumia sana, lakini siwezi kulalamika kwa sababu sikupiga kura. Hata hivo kati ya wote waliobaki, hakuna anayemfikia yule dogo hata kwa mbali tu. Utabaki kuwa ukweli hata kama ametoka.
 
Mimi tangu mwaka juzi sijaweza kuangalia hiyo Bss kwani ninaona kelele na fujo tu,kulinganisha na Tusker Project Fame wale wako organised,na mshiriki anapimwa katika nyimbo zote na unakuta anafiti, na kura zinahesabiwa na kampuni .hamna wabana pua sio hii Bss mtu anajiimbia kwaya au taarab tu mpaka anafika top 10 au 5,najitahidi kujaribu kuwa mzalendo lakini yaani siwezi angalia vituko.
 
Tunazikubali lakini si kwa kiwango kikubwa cha uchakachuaji kama wanavyofanya. Hakuna mtu mwenye akili timamu asiye na masilahi yoyote na mshiriki yoyote anayeweza kukubali kwamba Norman alistahili kutolewa jana. Hata kwenye danger zone hajaingia then from no where wanamtoa.

Ndio maana nakubaliana na hoja ya Kibunango kwamba ni muhimu kuwepo na screen inayotuonyesha votes counts vinginevyo hakuna maana ya kusema wanatafuta vipaji kumbe wanawatafutia ulaji watu wao. Hii inawakatisha sana tamaa vijana ambao wana vipaji vya kuimba na wamekuwa wakipoteza muda wao mwingi kushiriki BSS.

wabongo bwana kwa kulalamika au na huku mtatuambia mnataka tume huru na daftari jipya la wapiga kura???!
 
Huyu madam Rita asiye na hata mume mnampa kichwa. Huyu ni chakula ya wakubwa na kuwadi wao kama Rahma Kharoos "rais' wa kampuni la mafuta la mkuu ambaye amemgeuza nyumba ndogo. Siku ya mambo yao kuwekwa hadharani mtashangaa. Kwani Bongo kuna wafanya biashara au wasanii tu? Ipo siku mtajua uchafu wao na mtashangaa waliwezaje kuwazuga muda wote huo.

Wewe bwana kisa kuishi nje ishakuwa tabu, sijawahi kuona post hata 1 unasifia kitu kinachofanyika huko home wewe nikuponda tu, box limekuathiri nadhani
 
Ila siku alipotoka Norman niliumia sana, lakini siwezi kulalamika kwa sababu sikupiga kura. Hata hivo kati ya wote waliobaki, hakuna anayemfikia yule dogo hata kwa mbali tu. Utabaki kuwa ukweli hata kama ametoka.

Mkuu pole sana kwa kuumia juu ya Norman, nami niliumia lkn sikushangaa sababu niliuelewa mchezo uliochezwa. Kimsingi dogo alitolewa kafara hili kuamasisha wadau wapige kura kwa wingi yaani wametuaminisha kuwa tusipopiga kura ata mtu akiwa mzuri vipi atatolewa tu, angalia jinsi Salama alivyojifanya kukimbia eti ataki lawama au Master J alivyofinyanga karatasi kuwa amekasirika mno lkn Rita akafikisha ujumbe uliokusudiwa kuwa bila ya kupigiwa kura yeyote atatolewa. Lkn watambue kuwa wanapoonesha ubabaishaji kwa kutoa washiriki wenye mvuto wanapoteza pia uhalisia wa shindano.
 
Back
Top Bottom