Master j, madam rita na salama siku za kuaibishwa na kulia zaja

Mngejua wala msingeangaika na izi sanaa za wabongo..sikujua kama kuna great thinkers wanafatilia huu usanii.."umeimba vizuri sana nitakupa ofa ya kurekodi wimbo mmoja kwenye studio yangu"-Master Jay...watu eeeeeeh unaona mpaka masta jei kamkubali...waulize waliowai kupewa izo ahadi mpaka leo kama wameshawai kurekodi ngoma zao..

Kipanya nae akirudia usanii wake wa awali aliowafanyia washiriki wa MaishaPlus hakika kipindi kitakufa tena.
 
.... Master J akawa anawakataa akisema kuwa waimbe tena bila vyombo maana wanatafuta mwimbaji na si mpiga vyombo. Pili, majaji wote hata Madam Rita hamkuwa mnawahitaji watu waliokuwa wanakuja na nyimbo za kiutamaduni eti kwa kuwa hiyo si miziki au style mnayoitafuta. Ni aibu sana leo....
Bongo hakuna kinachofanyika bila Magumashi hivi hamjastuka tuu?waachieni mavipindi yao ili wapange matokeo vizuri.
 
Haijalishi Madam Rita ni nani
Kikubwa amejaribu kuchangia jamii na yeye mwenyewe kujikimu

Kwa nini tusikubali kazi za watu wengine wanapojitahidi??? I don't get it.
 
Tunazikubali lakini si kwa kiwango kikubwa cha uchakachuaji kama wanavyofanya. Hakuna mtu mwenye akili timamu asiye na masilahi yoyote na mshiriki yoyote anayeweza kukubali kwamba Norman alistahili kutolewa jana. Hata kwenye danger zone hajaingia then from no where wanamtoa.

Ndio maana nakubaliana na hoja ya Kibunango kwamba ni muhimu kuwepo na screen inayotuonyesha votes counts vinginevyo hakuna maana ya kusema wanatafuta vipaji kumbe wanawatafutia ulaji watu wao. Hii inawakatisha sana tamaa vijana ambao wana vipaji vya kuimba na wamekuwa wakipoteza muda wao mwingi kushiriki BSS.
 
Last edited by a moderator:
Norman anaweza kuwa anajua kuimba sana

Je ni aina ya mtu mwenye mvuto wa kupigiwa kura??? Kwangu hakuwa na mvuto kabisa, na nisingeweza mpigia kura japo anaimba vizuri.

Kwanza mie nilikuwa naona madam rita anampigia debe norman wazi wazi sababu anaonekana ana adabu au hali ngumu labda. Kuna siku kama wiki mbili zilizopita alimpigia debe wazi wazi hadi kidogo nizime tv cos he was not one of my favourate.

Na wiki iliyopita hakuna mshiriki aliyetoka hivyo washiriki wote walikuwa kwenye danger zone, sioni upendeleo ulipofanyika.

So sioni upendeleo wa kiasi hicho labda masimango kwa nshoma maana wanamlinganisha sana na Misoji

Hilo ndilo nililoliona mie Mkuu.. Kwamba Norman alikuwa anapigiwa debe na majaji wote.. Na huwezi kuniaminisha ati huyo Norman ana uwezo kuliko washiriki waliobaki..! Wapo wenye uwezo na mvuto kwa wapiga kura na ndio maana unaona Wababa anaongoza..! Inawezekana kuna mapungufu ambayo yaangaliwe kama changamoto ila haya-justify vapor ilitemwa hapa na mleta uzi.. Hii ni a reality show na so far kinaleta burudani kwangu..
 
Hivi kati yetu tunaolalamika kuhusu hii kitu tumepiga kura ngapi ngapi kwa washiriki tunaowapenda ili tuweze kujustify kwamba kweli kura zetu hazikutiliwa maanani?

Tusiwe ndani ya mioyo ya watu jamani, kwamba flani wewe unampenda ukaamini kwamba watu watampigia kura. Wote watkuwa kama wewe, wanampenda ila hawampigii kura hivyo anatoka.

Kibongo bongo hata kwenye siasa ni hivi hivi, mtu umekaa na PC yako unasubiria mtu unayempenda ashinde uchaguzi wakati hata kura hukwenda kupiga!!!!

Mashindano yenyewe majaji wote wako single, na ni watu ambao katika jamii yetu tunawaona wa ajabu ajabu kuanzia mavazi yao, ongea yao, matendo yao ukilinganisha na umri wao haviendani! Mara utasikia huyu ni mboga ya huyu, huyu ni msagaji, huyu anatembea na wasanii wa lebo yake huyu vile, aaagh!!!!

Mzee Kitine yuko wapi? Aliona anachafuka akaacha? Au wao waliona kuwa hawaendani naye? Sijui. Angalia kupoteza muda wako tu!
 
BSS iko kibiashara na sio NGO isiyotaka faida. Faida yao na maslahi kwanza halafu vipaji vya mdundiko baadae.
 
Norman anaweza kuwa anajua kuimba sana

Je ni aina ya mtu mwenye mvuto wa kupigiwa kura??? Kwangu hakuwa na mvuto kabisa, na nisingeweza mpigia kura japo anaimba vizuri.

Kwanza mie nilikuwa naona madam rita anampigia debe norman wazi wazi sababu anaonekana ana adabu au hali ngumu labda. Kuna siku kama wiki mbili zilizopita alimpigia debe wazi wazi hadi kidogo nizime tv cos he was not one of my favourate.

Na wiki iliyopita hakuna mshiriki aliyetoka hivyo washiriki wote walikuwa kwenye danger zone, sioni upendeleo ulipofanyika.

So sioni upendeleo wa kiasi hicho labda masimango kwa nshoma maana wanamlinganisha sana na Misoji

Kama unadhani kumtoa Norman ilikuwa sahihi, umeshajiuliza ni kwanini majaji waliamua kukimbia jukwaa wakati Norman anatangazwa kutolewa? hukumuona hata Master J alivyosema anajua watu hawatoamini kilichokuwa kinatokea?

Ni ukweli kwamba walijua mtu wanayemtoa hakustahili kutolewa. Mtu kama Menynar wamembeba sana hadi baadae wakaona habebeki wakaamua kumtoa.
 
Mkuu kuna vipindi zaidi ya milioni kwenye tv stations.. Kama vipi wewe kipotezee sio unamwaga povu hapa..

Usiponde sana mkuu, tunapishana sana kwenye hobbie, ndo sbabu wakati wewe unaangalia basketball, kuna wenzako wanaangalia cycling, swimming, football, baseball n.k. Ni mtazamo tu, ambapo mleta mada katoa hisia zake kwa kuwa ni mfuatiliaji wa mambo ya EBSS.
 
kwanza BSS haina tija kwa mustakabali wa muziki wa hapa bongo kwa sababu hawatafuti wanamuziki,bali wanatafuta watu wanaoweza na kujua kuiga kuimba(MAKASUKU) na ndio maana hadi leo hii hakuna mshindi wa BSS anayesikika au kufahamika katika ramani ya MUZIKI WA TANZANIA
my take
waanze upya wabadilishe na pia majaji hao lazima wawe na na terms of refference katika kutoa judgment zao coz kina SALAMA wanamjaji mtu kwa upeo wao finyu na kwa mapenzi binafsi au chuki binafsi,kwa mfano kuna dada mmoja wa kihindi SIMJUI JINA NA SITAKI KUMJUA alichukuliwa wakati hata kuiga tu sauti hajui.....huu ni upuuzi na kuendelea kuushusha chini mziki wetu

naomba kutoa hoja
 
Hivi kati yetu tunaolalamika kuhusu hii kitu tumepiga kura ngapi ngapi kwa washiriki tunaowapenda ili tuweze kujustify kwamba kweli kura zetu hazikutiliwa maanani?

Tusiwe ndani ya mioyo ya watu jamani, kwamba flani wewe unampenda ukaamini kwamba watu watampigia kura. Wote watkuwa kama wewe, wanampenda ila hawampigii kura hivyo anatoka.

Kibongo bongo hata kwenye siasa ni hivi hivi, mtu umekaa na PC yako unasubiria mtu unayempenda ashinde uchaguzi wakati hata kura hukwenda kupiga!!!!

Mashindano yenyewe majaji wote wako single, na ni watu ambao katika jamii yetu tunawaona wa ajabu ajabu kuanzia mavazi yao, ongea yao, matendo yao ukilinganisha na umri wao haviendani! Mara utasikia huyu ni mboga ya huyu, huyu ni msagaji, huyu anatembea na wasanii wa lebo yake huyu vile, aaagh!!!!

Mzee Kitine yuko wapi? Aliona anachafuka akaacha? Au wao waliona kuwa hawaendani naye? Sijui. Angalia kupoteza muda wako tu!

true dat! Sijawahi kupiga kura na wala sitarajii kufanya hivyo mie naichukulia bss kama ze comedy!
 
kwanza BSS haina tija kwa mustakabali wa muziki wa hapa bongo kwa sababu hawatafuti wanamuziki,bali wanatafuta watu wanaoweza na kujua kuiga kuimba(MAKASUKU) na ndio maana hadi leo hii hakuna mshindi wa BSS anayesikika au kufahamika katika ramani ya MUZIKI WA TANZANIA
my take
waanze upya wabadilishe na pia majaji hao lazima wawe na na terms of refference katika kutoa judgment zao coz kina SALAMA wanamjaji mtu kwa upeo wao finyu na kwa mapenzi binafsi au chuki binafsi,kwa mfano kuna dada mmoja wa kihindi SIMJUI JINA NA SITAKI KUMJUA alichukuliwa wakati hata kuiga tu sauti hajui.....huu ni upuuzi na kuendelea kuushusha chini mziki wetu

naomba kutoa hoja

Mkuu huu ni muendelezo wa uozo kwa kila kila nyanja.. iwe siasa.. uchumi.. michezo na burudani.. Kwa hiyo for the time being acha tu tufurahie na mapungufu yote yaliopo..
 
Rita katia kibindoni tsh 2bn toka zantel kwa ajili ya hiyo BSS!swali TRA wamemtembelea kuchukua kodi?
 
Ni hivi..., Mbali na washiriki au Mshiriki kuwa na uwezo wa kuimba na kumiliki jukwaa lazima awe na kitu wao wanaita "Ex-factor" yaani Mvuto wa Nje wa Mshiriki katika Minaji ya Muonekano wake Mzuri kwa Audience, na hili ni kubwa sana katika Tasini nyingi mfano.Tasinia ya Filamu na Musiki wa kizazi kipya ( Bongo Flavour) ambao washiriki hao wanapigania kutoka nao...Ex-factor ni Mtaji mkubwa sana kwa vijana washiriki katika Mashindano hayo.

Mbali na ivyo..., husisahau jambo la Nidhamu, hakuna jambo lolote Duniani utakaloweza fanikiwa kama hakuna Nidhamu..., ivyo washiriki wote wanatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote wa Mashindano.Mfano, Nidhamu ya kuwasikiliza washauri wao wakati wa Mazoezi, ushirikiano wa Mshiriki na wenzake, Pia swala lile la pale Mezani yule kijana ( Norman ) alionyesha utovu wa nidhamu kwenda nje ya protokali ya mezani, tusemege ukweli jamani sio kukalia na kuonyesha mapenzi ya Mshiriki fulani kama wale wa UVCCM.!!!
 
Nakumbuka mambo ya Gidion Chimbungaelo aka CHIPS mratibu wa shindano la Miss Utalii.
 
Back
Top Bottom