Master j, madam rita na salama siku za kuaibishwa na kulia zaja

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Tunawezaje kuwaamini majaji wa Epic Bongo Stars search hususani kuhusu upigaji wa kura. Kwa nini kusingekuwa na screen counts tuone vividly jinsi watu walivyopiga kura ngapi kwa nani. Nimehisi hujuma ya wazi kwa kijana Norman aliyeondolewa leo. Kuna mazingira matatu ambayo ni ya wazi ambayo hatuyapendi nayo ni:

1. Mtangazaji wa kike anapowaita na kuwatambulisha waimbaji yuko biased sana mfano anatoa sifa kibao kwa Salma Yusuf eti gitaa girl, Nshama na Wababa n.k Ukweli huyu guitar girl hana sauti (vocal) yeyote ya maana kuliko Norman. Nasema anaweza kuwa mpiga chombo na mjuzi wa muziki (nota) kama somo lakini talent ya kuimba wala kuperform jukwaani ni chini ya kiwango sana kuliko Norman na wengine wote. Anapoimba anabana sauti na anatoa sauti ya mwikwaruzo!

2. Majaji wanavyombeba Salma na Nshama pia ni bayana kwa kuonesha double stds. Wakati wa kutafuta washiriki mikoani kuna watu kibao waliingia katika mashindano toka huko Mwanza, Dodoma, hata Dar walikuwa wakali sana wa matumizi ya vyombo vya muziki na kuimba, Master J akawa anawakataa akisema kuwa waimbe tena bila vyombo maana wanatafuta mwimbaji na si mpiga vyombo. Pili, majaji wote hata Madam Rita hamkuwa mnawahitaji watu waliokuwa wanakuja na nyimbo za kiutamaduni eti kwa kuwa hiyo si miziki au style mnayoitafuta. Ni aibu sana leo tunashuhudia mkiwabeba na kuwapigia saluti akina Nshama na mwenzake yule mrefu (sikumbuki jina lake) ambaye sauti yake naye iko chini na anaimba nje ya key kila wakati anapenda kuimba nyimbo za utamaduni za Afrika kusini au za akina Helen Kijo. Je, mnataka kutuambia kuwa utamaduni wa mwafrika nje ya Tanzania ni bora kuliko ule wa wa Msukuma au Mnyamwezi, Mzigua n.k ambao uliwasilishwa kwa kiwango cha juu sana na washiriki mwazoni. Pitieni kimya kimya zile video zenu za mwanzoni huko Mwanza, Tanga muone. Majaji, mnaaibisha sana na double standards zenu halafu eti wakati wa kutoa matokeo kumfukuza Norman ili kumuandalia ‘guitar girl njia na ushindi’mnajifanya kukimbia toka jukwaani kuwa mmesikitika au kuwalaumu wapiga kura! Kila mtu anawaona kuwa mnajihuzunisha mbele ya screen kama ze comedy wanavyoweza kuamua kulia wakati hakika hawana huzuni wowote!

3. Uchunguzi zaidi ni kuwa hawa vijana washiriki walipopelekwa katika moja ya Stars Hotel nchini eti kameraman wa BSS akawa anamtafuta yeye Norman kwa karibu kuonyesha vituko au ushamba wake mezani (unbecoming table manners) mfano kumuonyesha Norman akinyanyua bakuli lake la supu toka mezani au alipojikuna kichwani akiwa mezani. This is such a very poor way of looking for a way to discredit a talented participant. Kwa jina la wote wapenda haki duniani chukueni video ya siku kijana huyu ameimba wimbo wa Lionel Richie; nasema haijatokea katika BSS, hata Richie mwenyewe hakufikia hapo kama huyu kijana alivyoimba siku hiyo maana nilitokwa na machozi ya furaha kumuangalia. Nimesikitika sana.

Madam Rita kumbuka kuwa kufanya biashara za dhuruma ni dhabi na ni kosa la jinai. Juzi tu Lance Amstrong kavuliwa medali zake zote za ubingwa wa dunia za miaka ya nyuma yote katika kuendesha baiskeli kwa kasi kwa sababu ya udanganyifu. Hizo siku za kuaibishwa na kulia zaja kwa BSS hata kama ni baada ya miaka mitano maana tutapitia video zote polepole na kudemand kura zilivyopigwa maana record zipo kwenye servers na ndipo tutawavua ubingwa wote mnaowabeba na kukulazimisha wewe Rita urudishe fedha za ufadhili na zile ambazo zinapatikana tokana na waliopiga simu kuwapa faida makampuni ya simu ambayo mnapanga nao matokeo toka mwanzo. Kwa nini usiwe unahusisha majaji wengine wataalamu wa muziki toka Bagamoyo ili kuwa objective & transparent? why always rafiki zako akina master J na Salama ambaye hana sifa yoyote na muziki isipokuwa kuwashushua watu walivyovaa au kuwambia watafute kazi nyingine lugha za kihuni sana kwa vijana wanaotafuta kujiendeleza kimziki.
 
Achana nao hao,angalia maisha plus sa 4 hdi 5 ucku tbc kpndi cha ukwl kinoma.
 
Kibunago ulichoandika hapo juu kina ukweli tena zaidi ya ukweli. Tatizo ni serikali yako imeshindwa kuwekeza na kusimamia vipaji vya vijana badala yake inamwachia mtu binafsi ambaye anaweza hata kunichagua mie niwe winner while mimi sina kipaji.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja tuone top 5 wataingia nani?!.
Yule menynah sijui nini kimempata leo hakuwa normal kabisa
 
Hivi hizo milioni 50 kwa age zao hizo ambazo zipo kati ya 16, 19, 20, 17 ,23 ukiachilia wababa. Je imewaandaa hawa vijana incase imagine 16 yrz anakuwa milionea?! Wasije kuchanganyikiwa na kuingia kwenye mambo ya madawa na anasa..
 
Ni burudani kama mpira wa miguu walah sijambo la kushangaza sana ndio maana binadamu tunatofautina
 
Huyu madam Rita asiye na hata mume mnampa kichwa. Huyu ni chakula ya wakubwa na kuwadi wao kama Rahma Kharoos "rais' wa kampuni la mafuta la mkuu ambaye amemgeuza nyumba ndogo. Siku ya mambo yao kuwekwa hadharani mtashangaa. Kwani Bongo kuna wafanya biashara au wasanii tu? Ipo siku mtajua uchafu wao na mtashangaa waliwezaje kuwazuga muda wote huo.
 
Huyu madam Rita asiye na hata mume mnampa kichwa. Huyu ni chakula ya wakubwa na kuwadi wao kama Rahma Kharoos "rais' wa kampuni la mafuta la mkuu ambaye amemgeuza nyumba ndogo. Siku ya mambo yao kuwekwa hadharani mtashangaa. Kwani Bongo kuna wafanya biashara au wasanii tu? Ipo siku mtajua uchafu wao na mtashangaa waliwezaje kuwazuga muda wote huo.


Kwanini usimwage sasa kama una data za kweli na sio uzushi?
 
nimeumia xana norman kutoka,cz mpaka jana nimempigia c chin ya kura 15,bt leo frm no where eti wanamtoa kwa lipi hasa?hakuna ukwl katika bss hzo kula 2napiga nidanganya toto 2,
 
Back
Top Bottom