Mastaa hawa kutoka South Korea hawatumii social media

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
653
1,097
Bila kupoteza muda naomba niwataje mastaa watano kutokea korea ambao hawana account rasmi kwenye mitandao ya kijamii.



Ukiingia instagram kwa mfano unakuta mashabiki wameanzisha Fan pages tu na kupost picha za wasanii hawa au kuna muda Music label au agencies huanzisha accounts za wasanii hawa lakini msanii hausiki nayo kabisa.




Sasa wafuatao ni wasanii kutokea nchini South Korea ambao hawatumii kabisa mitandao ya kijamii.

Kwa chini hapo nitaweka picha kwa mpangilio ili uweze kuwatambua mastaa hao.



5. JANG HYUK

Mwamba aliyeigiza IRIS 2 : THE NEW GENERATION, VOICE na SLAVE HUNTER.
Ukienda Instagram sasa hivi kuna fan pages nyingi sana kuhusiana na huyu jamaa lakini hana account instagram na pia hana muda kabisa na mitandao ya kijamii.



4.GONG YOO.

Kama Umeangalia GOBLIN : THE LONELY AND GREAT GOD pia COFEE PRINCE ya 2007 yeye ndiye main actor.


Kwa wale wa movies pia ameigiza kama Stering kwenye TRAIN TO BUSAN.
Yoo nae hana muda na mitandao ya kijamaa na ilifikia wakati akaiita "Poisonous" maana inasababisha madhara mengi kuliko faida.





3 SOO AE


"Queen Of Sorrows " tunaweza kumuita hivyo. Ameigiza series kama EMPEROR OF THE SEA ya 2004 kama Jung hwa ila uwezo wake ulionekana sana kwenye "WOMAN OF AMBITION" stori inayoelezea mwanamke aliyetokea maisha ya chini hadi kuwa mke wa rais.


Pia Soo Ae alishirikiana na Jang Hyuk kwenye movie ya Flu mwaka 2013.
Sasa mimi binafsi nimemtafuta huko Instagram lakini sijamuona zilizopo ni fan page tu.





2.. SONG JOONGI KI


Ameigiza kwenye movie ya SPACE SWEEPERS lakini kwa wale wanaopenda series ameigiza DESCENDANTS OF THE SUN, VINCENZO,THE BATTLESHIP ISLAND na ARTHDAL CHRONICLES.

Joong Ki anasema yeye sio mtu wa teknolojia sana na ndio maana mambo ya mitandao hayafuatilii sana.





1. KIM TAE HEE.


Kama umeangalia IRIS 1 hapa namuongelea Choi Seung Hui mpenzi wa Kim Hyeonjun.


Kuna kipindi alishawahi kutajwa na jarida moja kuwa yeye ndiye mwanamke mrembo zaidi pale South Korea lakini hiyo haikumfanya yeye kujiunga kwenye mitandao ya kijamii.
Tae Hee ameolewa na mwanamuziki Rain.

Hao ni mimi ninaowafahamu je unamfahamu msanii mwengine kutokea South Korea ambae hayupo active kwenye mitandao?
e8f08a896f2949b49669f55283d651c3.jpg
75cd6efd0afb544a632e5063e7e1635f.jpg
0fb90863ac2cdaf8b6eba92a0ca07d07.jpg
]
09259115f645532329fc26d433445e86.jpg
 

Attachments

  • jgksa.jpg
    jgksa.jpg
    51.1 KB · Views: 7
Huwezi kumkuta kwenye mitandao ya kijamii ukimaanisha nini?

Sina muda wa kufuatilia wengine lakini Jumong yupo insta,na mara ya mwisho kupost ni mwezi jana tu hapo

Next joke please......


20210518_201415.jpg
 
Huwezi kumkuta kwenye mitandao ya kijamii ukimaanisha nini?

Sina muda wa kufuatilia wengine lakini Jumong yupo insta,na mara ya mwisho kupost ni mwezi jana tu hapo

Next joke please......


View attachment 1789992
Hapo of course niliteleza kidogo na nimerekebisha.

You didnt have to act sarcastic to pass your message.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom