Mastaa 6 wa wafata nyayo za Messi kutundika daruga Argentina

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
13,215
Messi-Mascherano.jpg

Hii ni siku mbaya kwa soka la Argentina, baada ya kushindwa kutwaa taji la Copa America kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Chile, wachezaji wa Argentina mmoja baada ya mwingine wamekuwa wakitangaza kustaafu kuichezea timu yao ya taifa.

Mchezaji wa kwanza kutangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo alikuwa Leo Messi ambaye alitangaza uamuzi huo muda mfupi baada ya mchezo dhidi ya Chile kumalizika.

Muda mfupi baadaye striker wa Manchester City Sergio Aguero na mlinzi wa kati wa FC Barcelona Javier Mascherano nao pia walitanga kuachana na timu soka la kimataifa.

Kama vile haitoshi, ripoti kutoka Amerika ya Kusini zinadai kuwa, Angel Di Maria, Ezequiel Lavezzi, Gonzalo Higuain na Lucas Biglia nao pia wameamua kutundika daruga kuitumikia Argentina.

Chanzo: Shaffih Dauda
 
Huyu messi alikuwa anatafuta sababu tu, sidhani kama argentina iko moyoni mwake.
 
Duu hebu waache masihara, ni kweli inauma sn hata mie ninahuzunika sn kuona jitihada xote anazofanya Leo Messi kwa timu yake ya Argentina lkn znagonga mwamba. Lkn cungi mkono wao kufanya hvyo cz ndo watazidi kuiweka pabaya timu na kuwakatisha tamaa wachezaji wao wachanga!
 
Nilitegemea hili na si kwa Argentina pekee bali hii itakuwa fashion kwa dunia nzima.

Messi ni role model wa wengi tu na watafuata tu nyayo zake sababu hili liko ndani ya uwezo wao.
 
Ronaldo atabaki kuwa Juu... Unastaafu kwenye kombe la mabara? naona wamemgeza Ibrahimovic
 
BREXIT ndio chanzo
lol Bretix walijipanga for 6 years before cha kwanza waliweka uchumi imara usije tetereka na Tatizo la Euro vizinga vingi na Michango vilikuwa vinaangukia kwa Uk. Kusepa kwao hizo pesa walizokuwa wanatoa kwa umoja wa ulaya watawapa Mabenki na wafanya biashara watakao teteleka na kujiondoa kwao... so let UK get back their country
 
MeSSi sijawahi sikia kaacha Nyayo sehemu Zlatan Ibrahimovic ndio kaanza kwa Mwaka huu
 
timu ina kikosi kikali lakini wanashindwa kuchukua vikombe, kikosi kama hiki kilikuwepo brazil na walifanya kweli kila kombe walibeba, leo brazil imebaki jina tu, hawa nao wana kikosi kizuri wanashindwa kila kombe sijui watachukua lini tena
 
Back
Top Bottom