Masta wa bongo hovyo sana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masta wa bongo hovyo sana.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kitalolo, Aug 17, 2012.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  UTASEMAJE MME WAKO ANACHOKONOLEWA ANAJUA MAANA YA KUCHOKONOA!


  MAIMARTHA: WAMESHAANZA KUMCHOKONOA MUME WANGU - Global Publishers


  Na Gladness Mallya

  MTANGAZAJI wa Kituo cha Runinga cha TBC1, Maimartha Jesse ameeleza kusikitishwa kwake na baadhi ya watu wasioitakia mema ndoa yake kwa kuanza kumchokonoa mume wake kipenzi, Shaa.

  Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Maimartha alisema kuwa, kuna watu ambao mara kwa mara wanamtumia sms za kumponda mume wake huyo wakieleza kuwa, eti hawaendani na ‘ameingia chaka'.

  Alisema kuwa, kibaya zaidi mumewe amekuwa akizisoma meseji hizo lakini kwa bahati nzuri ni muelewa hivyo hakasiriki badala yake humtaka kuzipuuza kwani zinatumwa na watu wasiowatakia mema.

  "Wapo watu walionitabiria mabaya na sasa yanawageukia, wapo pia wengine bado wananifuatilia wanataka kuivunja ndoa yangu lakini nawaambia watashindwa,nampenda mume wangu na naamini tutadumu," alisema Maimartha.
   
 2. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Kumbe "Shaa" ni mwanaume??? :nerd:
   
 3. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  aisee siku zote shaa nilijua ni mwanamke tena mmbea na kichenchede kumbe mme wa mtu....abadili jina bwana
   
Loading...