Masoud Kipanya nimekusikia, bima inaonekana kutolipia magonjwa yasiyoambukiza

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,392
21,881
Serikali imekuwa ikituaminisha kuwa bima ya afya ni mkombozi kwenye maisha yetu lakini serikali hiyohiyo haikubali kuwapa bima waliopata maradhi yasiyo ya kuambukiza!

Nimekusikia ukisema neno linalotolewa na Watanzania wengi kuwa bima ya afya haitolewi kwa baadhi ya maradhi! Hii inamaanisha kuwa bima ya afya iko kibiashara zaidi kwa wasiopata maradhi ili bima ifaidike! Watanzania ni wakati sasa kutaka mabadiliko ili wazee na wenye maradhi waweze kununua bima badala ya kubaguliwa kwa kosa lisilo lao.

Narudia tena pole kwa mzigo wa gharama za matibabu inayoipata familia yako, Mungu awe nanyi

===
Pole sana Masoud!

Kidunia ni kawaida sana kwa mashirika ya Bima ya Afya kuzuia matibabu ya magonjwa fulani. Mashirika mengi ya BIMA huzuia baadhi ya magonjwa kuyatibu, mfano magonjwa ya kuzaliwa nayo (Congenital), matibabu ya VVU/UKIMWI, upasuaji wa kutengeneza urembo, kutibu utasa, kutibu magonjwa ya kinywa yasiyosababishwa na ajali, majeraha yako uliyoyasababisha mwenyewe, magonjwa yatokanayo na madhara ya kutumia madawa ya kulevya, kulazwa kwa magonjwa yatokanayo na vita au mionzi n.k.

Watu wengi hususani watanzania hawana elimu ya kutosha kuhusu Bima ya Afya. Hawajui mifuko inavyofanya kazi. Wengi wanadhani hii mifuko ni sawa na Vicoba au SACCOSS. Hawajui kwamba hii mifuko ya Bima ya Afya, inapaswa kuwa endelevu. Mifuko hii inajiendesha. Inalipa mishahara. Hawajui kwamba hakuna pesa ya mjomba inapelekwa Bima ya Afya ili iweze kutoa matibabu kwa wanachama wake. Hawajui kwamba matibabu yote yanatolewa kupitia michango ya wanachama. Hawafahamu kwamba mara nyingi matibabu ya mwanachama au tegemezi hata ya siku moja, yanazidi michango ya mwaka mzima ya mwanachama mkuu (Principal). Nasikia serikali iliwahi kopa pesa huku, hili ni kosa kubwa.

Pindi mfuko wetu mkubwa wa NHIF ukifa, mfumo mzima wa afya wa taifa utaporomoka. Kaziulize hospitali hapa Tanzania jinsi zinavyonufaika kwa kuwepo kwa mfuko wa Bima wa Afya, hata misamaha ya baadhi ya matibabu inategemea mapato yatokayo kwa wagonjwa wa Bima za Afya.

Mimi ni mongoni mwa wanachama wa kawaida wa NHIF, ambaye ninafurahia mfuko ukizidi kukua. Ninakatwa mshahara kila mwezi. Ninafurahia kutokutumia kadi yangu, ninatunza afya yangu, lakini pindi nikiumwa nina kadi nitaitumia.

Ukiacha la Masoud kuna vitu vingine kila mtu anaweza vifikiria na vikampa changamoto ya maamuzi. Hebu fikiria wewe unamiliki kampuni ya bima, halafu mtu analeta gari ambalo limeharibika kabisa anataka umpe insurance kuna vitu gani utaviangalia ili kumpa bima? Kuna mtu mwingine ana duka mtaani amekuja kukata Bima. Baada ya kumtembelea dukani umegundua huyu jana dukani kwake anavamiwa kila wiki, hivi ni vitu gani utaangalia ili kumpa au kutompa bima?

Ningekuwa kiongozi wa Bima ya Afya, labda ningeshauri mtoto wa Masoud apate Bima ila nikazuia baadhi ya benefits.

Kwa kuongeza elimu ya Bima ya Afya, tujue Bima sio vikoba na hivyo usitegemee kesho upate faida ya michango yako bila kuumwa, kwani hiyo sio maana ya Bima zote. Kwa kutokujua hili watu wengi kwa ujinga wao wanalazimisha kupata mafao ya Bima kwa kuchoma mali walizozikatia bima au kulazimisha kwenda hospitali.

Bima ya Afya na Bima nyingine usizifananishe na mifuko ya pensheni. Bima inaweza fanana na mtu mwenye duka, anayeamua kumgharamia mlinzi ili alinde biashara yake. Furaha ya mwenye duka si kuona akiibiwa, bali kuona mali yake ni salama. Lakini mwizi akija, atakutana na mlinzi. Hakuna siku mwenye duka atamwambia mlinzi ampe faida ya mshahara aliomlipa siku zote kwa sababu ya duka lake kutovamiwa na majambazi.
 
Serikali imekuwa ikituaminisha kuwa bima ya afya ni mkombozi kwenye maisha yetu, lakini serikali hiyohiyo haikubali kuwapa bima waliopata maradhi yasiyo ya kuambukiza
Sio bima tu hadi mifuko ya mafao kama NSSF na PSSSF ipo kibiashara tu ndio maana hawatoi pesa au wameondoa FAO LA KUJITOA ili wasipate hasara wawe na faida. WE NEED TOTAL REFORM
 
FAO LA kujitoa mbona lipo
 
Tena bora zamani kidogo hivi sasa bima imekuwa ya hovyo sijawahi kuona..ukienda hospital kuna dawa unaambiwa zimetolea (japo bima wanakataa lakini madocta wanatuambia ukweli kuwa zimetolewa) , hasa baadhi ya dawa kubwa kubwa kwa watu wenye hypertension.. sukari etc.

Bima kwa sasa ni usanii.

labda ya lissu itakuja na jibu maana ya jiwe inaumiza watu na kulalamikiwa sana.
Serikali imekuwa ikituaminisha kuwa bima ya afya ni mkombozi kwenye maisha yetu, lakini serikali hiyohiyo haikubali kuwapa bima waliopata maradhi yasiyo ya kuambukiza! Nimekusikia ukisema neno linalotolewa na watanzania wengi kuwa bima ya afya haitolewi kwa baadhi ya maradhi! Hii inamaanisha kuwa bima ya afya uko kibiashara zaidi kwa wasiopata maradhi ili bima ifaidike! Watanzania ni wakati sasa kutaka mabadiliko ili wazee na wenye maradhi waweze kununua bima badala ya kubaguliwa kwa kosa lisilo lao.
Narudia tena pole kwa mzigo wa gharama za matibabu inayoipata familia yako, Mungu awe nanyi.
 
Mkuu,serikali imekopa sana kwenye hii mifuko,na mikopo wameshindwa kuirejesha kama ilivyotarajiwa,Mifuko haina fedha kuweza kukidhi utoaji wa mafao kama ilivyokuwa zamani.

Hivyo kwakuwa serikali ndiyo iliyosababisha dhahama hiyo ikapeleka mswada bungeni kuondoa baadhi ya mafao hasa hili fao la kujitoa ili kuinusuru mifuko hiyo.
Sio bima tu hadi mifuko ya mafao kama NSSF na PSSSF ipo kibiashara tu ndio maana hawatoi pesa au wameondoa FAO LA KUJITOA ili wasipate hasara wawe na faida. WE NEED TOTAL REFORM
 
Pole sana Masoud!

Kidunia ni kawaida sana kwa mashirika ya Bima ya Afya kuzuia matibabu ya magonjwa fulani. Mashirika mengi ya BIMA huzuia baadhi ya magonjwa kuyatibu, mfano magonjwa ya kuzaliwa nayo (Congenital), matibabu ya VVU/UKIMWI, upasuaji wa kutengeneza urembo, kutibu utasa, kutibu magonjwa ya kinywa yasiyosababishwa na ajali, majeraha yako uliyoyasababisha mwenyewe, magonjwa yatokanayo na madhara ya kutumia madawa ya kulevya, kulazwa kwa magonjwa yatokanayo na vita au mionzi n.k.

Watu wengi hususani watanzania hawana elimu ya kutosha kuhusu Bima ya Afya. Hawajui mifuko inavyofanya kazi. Wengi wanadhani hii mifuko ni sawa na Vicoba au SACCOSS. Hawajui kwamba hii mifuko ya Bima ya Afya, inapaswa kuwa endelevu. Mifuko hii inajiendesha. Inalipa mishahara. Hawajui kwamba hakuna pesa ya mjomba inapelekwa Bima ya Afya ili iweze kutoa matibabu kwa wanachama wake.

Hawajui kwamba matibabu yote yanatolewa kupitia michango ya wanachama. Hawafahamu kwamba mara nyingi matibabu ya mwanachama au tegemezi hata ya siku moja, yanazidi michango ya mwaka mzima ya mwanachama mkuu (Principal). Nasikia serikali iliwahi kopa pesa huku, hili ni kosa kubwa.

Pindi mfuko wetu mkubwa wa NHIF ukifa, mfumo mzima wa afya wa taifa utaporomoka. Kaziulize hospitali hapa Tanzania jinsi zinavyonufaika kwa kuwepo kwa mfuko wa Bima wa Afya, hata misamaha ya baadhi ya matibabu inategemea mapato yatokayo kwa wagonjwa wa Bima za Afya.

Mimi ni mongoni mwa wanachama wa kawaida wa NHIF, ambaye ninafurahia mfuko ukizidi kukua. Ninakatwa mshahara kila mwezi. Ninafurahia kutokutumia kadi yangu, ninatunza afya yangu, lakini pindi nikiumwa nina kadi nitaitumia.

Ukiacha la Masoud kuna vitu vingine kila mtu anaweza vifikiria na vikampa changamoto ya maamuzi. Hebu fikiria wewe unamiliki kampuni ya bima, halafu mtu analeta gari ambalo limeharibika kabisa anataka umpe insurance kuna vitu gani utaviangalia ili kumpa bima? Kuna mtu mwingine ana duka mtaani amekuja kukata Bima. Baada ya kumtembelea dukani umegundua huyu jana dukani kwake anavamiwa kila wiki, hivi ni vitu gani utaangalia ili kumpa au kutompa bima?

Ningekuwa kiongozi wa Bima ya Afya, labda ningeshauri mtoto wa Masoud apate Bima ila nikazuia baadhi ya benefits.

Kwa kuongeza elimu ya Bima ya Afya, tujue Bima sio vikoba na hivyo usitegemee kesho upate faida ya michango yako bila kuumwa, kwani hiyo sio maana ya Bima zote. Kwa kutokujua hili watu wengi kwa ujinga wao wanalazimisha kupata mafao ya Bima kwa kuchoma mali walizozikatia bima au kulazimisha kwenda hospitali.

Bima ya Afya na Bima nyingine usizifananishe na mifuko ya pensheni. Bima inaweza fanana na mtu mwenye duka, anayeamua kumgharamia mlinzi ili alinde biashara yake. Furaha ya mwenye duka si kuona akiibiwa, bali kuona mali yake ni salama. Lakini mwizi akija, atakutana na mlinzi. Hakuna siku mwenye duka atamwambia mlinzi ampe faida ya mshahara aliomlipa siku zote kwa sababu ya duka lake kutovamiwa na majambazi.
Serikali imekuwa ikituaminisha kuwa bima ya afya ni mkombozi kwenye maisha yetu lakini serikali hiyohiyo haikubali kuwapa bima waliopata maradhi yasiyo ya kuambukiza!

Nimekusikia ukisema neno linalotolewa na watanzania wengi kuwa bima ya afya haitolewi kwa baadhi ya maradhi! Hii inamaanisha kuwa bima ya afya iko kibiashara zaidi kwa wasiopata maradhi ili bima ifaidike! Watanzania ni wakati sasa kutaka mabadiliko ili wazee na wenye maradhi waweze kununua bima badala ya kubaguliwa kwa kosa lisilo lao.

Narudia tena pole kwa mzigo wa gharama za matibabu inayoipata familia yako, Mungu awe nanyi.
 
Jukumu la kuelimisha wananchi jinsi Bima zinavyofanya kazi ni la nani?Mbona mnawalaumu wanachama?
 
Kwa kauli yako unatuambia serikali inatudanganya! Jana ilianzishwa huduma ya mkulima na familia yake lakini ukiangalia wakulima wengi ni wazee ambao bima inawakataa! Sasa itakuwaje?
 
Kwa msiojua Malcolm (chini ya 18 kama sijakosea) ambaye ni mwanae Masoud Kipanya ameanzisha kampeni kwa ajili ya kuwaelimisha wenye tatizo kama lake na watu wengine wenye uwezo wa kutoa misaada.

Naomba tusiweke mzaha kwenye Post hii kwani tutakuwa tunawakandamiza waathirika wa maradhi haya.
 
Huu ni ujambazi wa wazi! Bima inatakiwa igaramie kila kitu ila kwa nchi za Afrika ni ushezi jazz band!
 
Changamoto kubwa ni hii bima ya taifa ya kuitwa NHIF, hawa ndio wanakataa hata dawa za kikohozi tusipewe za nchi kama India nzuri baki wanalazimisha wote tunywe za pale mwenge au vingunguti, bahati nzuri madaktari ukiwabana kwanini amekuandikia hiyo anaongea kuwa sio yeye ila ni maekekezo!
 
Sio bima tu hadi mifuko ya mafao kama NSSF na PSSSF ipo kibiashara tu ndio maana hawatoi pesa au wameondoa FAO LA KUJITOA ili wasipate hasara wawe na faida. WE NEED TOTAL REFORM
Halafu utaenda kupiga kura Kwa magufuli eti
 
Tena bora zamani kidogo hivi sasa bima imekuwa ya hovyo sijawahi kuona..ukienda hospital kuna dawa unaambiwa zimetolea (japo bima wanakataa lakini madocta wanatuambia ukweli kuwa zimetolewa) , hasa baadhi ya dawa kubwa kubwa kwa watu wenye hypertension.. sukari etc.

bima kwa sasa ni usanii.

labda ya lissu itakuja na jibu maana ya jiwe inaumiza watu na kulalamikiwa sana.

Natoa Pole kwa familia ya Masoudi kwa gharama za kumhudumia mtoto, pia nampongenza mtoto kwa kampeni ya aliyoizindua, Mwenyezi Mungu amsaidie.

Nakubaliana nawe kwamba NHIF mwanzoni ilikuwa inahudumia wanachama wake vizuri. Pia sikubaliani nawe kwamba kwa sasa ni usanii tu kwani wapo wanaonufaika huduma zao.

Kwanza niweke wazi kwamba Mimi pia ni mnufaika wa huduma zitolewazo na NHIF kwa kipengele Cha wachangiaji binafsi, miaka ya nyuma ukichangia 1,540'000/= kwa mwaka unapata dawa zote na vipimo vyote isipokuwa kuna baadhi dawa na matibabu mengine kwa kibali maalum.

Shida imeaanza mwishoni mwa mwaka Jana baada ya utaratibu wa uchangiaji wa vifurushi walivyovigawa kulingana na hali ya mtu pamoja na umri, hapa ndipo tatizo limeanzia kwani kuna baadhi ya dawa zimeondolewa na baadhi ya matibabu yameondolewa hasa yasiyoambukiza.

Mimi ni mhanga wa kukosa huduma hizi kwani mme wangu alikuwa ana shida ya BP pamoja na kisukari dawa zote alikuwa anapata pasipo shida yoyote, mwishoni mwa mwaka Jana Figo zilishindwa kufanya kazi wakaanza kumsafisha( dialysis) na NHIF walikuwa wanagharamia fedha nyingi, kwa wiki anatakiwa asafishwe mara 3 x 240,000/= 720,000/huduma hii kwa sasa haitolewi tena kwa mchangiaji binafsi, mgonjwa anajilipia kwa mwananchi wa hali ya kawaida inakuwa ngumu kumudu gharama hizi NHIF badala ya kuwa mkombozi imekuwa tofauti.

Wagonjwa wengi wa Figo wanapoteza maisha kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu, ninaandika haya nikiwa na uchungu wa kumpoteza Mme wangu miezi 3 imepita.

NHIF waliangalie kwa upya hili la kutogharamia matibabu ya baadhi ya magonjwa yasiyo ambukiza likiwemo hili tatizo la mtoto wa ndugu yetu Masoud pamoja na watanzania wengi wanaougua maradhi mbalimbali yakiwemo ya Kansa kwani matibabu yake ni ghari mno.
 
Pole sana mama
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom