Masoud Kipanya na Joti wanaweza kugombea urais wa Tanzania

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,494
2,000
Ilianza kama mzaha miaka kumi iliyopita ambapo Andry Rajoelina “DJ Mstaafu” au kwa kimombo “The retired disc jockey” alipochukua uongozi wa nchi ya Madagasca toka kwa mtangulizi wake Marc Ravalomanana. Wakati dunia bado inashangaa mnamo mwaka 2017, aliyekuwa mchezaji bora wa dunia mwaka 1995 George Weah alipokea kijiti cha urais wa Liberia toka kwa Ellen Johnson Sirleaf.

Wakati shamrashamra za kumpokea George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah zikiwa bado hazijatulia mwishoni mwa mwaka 2018, dunia ilipokea kwa hamasa kubwa habari za aliyekuwa mcheza cricket mashuhuri duniani Imran Khan kuchakuliwa kuwa waziri mkuu wa Pakistan.akipokea uongozi toka kwa nawaz-sharif.

Kubwa kuliko yote, limetokea mwishoni wa wiki iliyopita tarehe 21/04/2019 ambapo mwigizaji mashuhuri asiye na uzoefu wowote wa kiuongozi Volodymyr Zelenskiy kuchaguliwa kuwa raisi wa Ukrainian akipokea kijiti toka kwa Petro Poroshenko. Volodymyr Zelenskiy amekuwa akiigiza kwa muda mrefu kama rais lakini Jumapili iliyopita mwigizaji wa Urais alikuwa rais kwelikweli.

Kwa kuangalia yaliyotokea katika hizo nchi nne hapo ambapo juu wasanii ( wanamichezo na waigizaji) wamechukua madaraka ya kuongoza nchi zao, je unadhani hapa kwetu kuna wasanii au wanamichezo ambao kama wakithubutu wanaweza kuuchukua uongozi wa taifa letu kwa madaraka ya uraisi?

Je, unadhani katika nchi yetu kuna wana michezo au wasanii walio na mvuto na ushawishi ambao wanaweza kuutumia kama silaha yao ya kuvuta wapiga kura wengi hasa kundi kubwa la vijana?

Mapovu yanaruhusiwa.

Karibuni
 

Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
22,984
2,000
Ukimtaja Kipanya uwe unaangalia na mtu mwingine wa kumtaja pamoja naye.

Huwezi kutaja Kipanya na Joti kwenye andiko moja, Ukimtaja Joti basi tafuta rika lake kwenye ufahamu na utimamu.
 
Top Bottom