Masoud Kipanya: Maisha yangu mimi sio ya kuyaweka hadharani kama watu wanavyotaka

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,806
“Maisha yangu mimi sio ya kuyaweka hadharani kama watu wanavyotaka, dunia tuliyopo kuna vitu vikifanyika watu wanaona kawaida na vile vya kawaida vinaonekana sio sawa"

"Kuna mtu anaweza akawa na mwenza mmoja lakini nyuma yake ana 'watu' wengi sana na kila mwaka anabadilisha na watu wanaona sawa ila kuna mwingine akifuata dini inavyotaka inakuwa shida”

Masoud Kipanya

====

Siku za karibuni Masoud amekuwa akiandamwa na dada maarufu mtandaoni juu ya ndoa yake mpya ya mke wa nne ambayo anadai imepeleka huzuni kwa mke wake wa kwanza.

Pia, soma=> Masoud Kipanya aongeza mke wa nne

Masoud Kipanya.jpg
 
Ku maintain wanawake wanne lazima uwe tajiri, vinginevyo itakula kwenye mwili na mifupa yako............hapo kila mmoja akipata wastani wa watoto wanne, kumi na sita, jumla unakuwa na timu ya watu 20 kwenye familia bado ndugu na watoto wao ambao watakuwa wanakutegemea.​
 
Mke wa kwanza anahuzunika kuletewa mke wa nne wakati alishaletewa wawili? Kwa sababu zipi anahuzunika?
Mke wa kwanza mama wa Malcon yeye aliachwa muda kabla hata yule malaika kuondoka.

Mwenye kulalamika pengine atakuwa bi mkubwa namba mbili

Nawaza kidogo pia, huyu bwana mdogo ni imani tu ya kufanya kuoa hivyo au ni mengine

Nakaribia kuamini yaliyosemwa wakati uliopita.

Wanaume heeee heee, oeni wanne wanne walau wote tutakaribia kupata wanaume.
 
Baadhi ya wa Tanzania ni wapumbavu sana umbea umbea umbea umbea Yan watu wanalipia had app kwa Mange ili wapate umbea, sijui unafaidika nini ukishayajua maisha ya mtu

Kinachosikitisha hadi watoto wa kiume wamekuwa wakuda kinoma yani
 
Ku maintain wanawake wanne lazima uwe tajiri, vinginevyo itakula kwenye mwili na mifupa yako............hapo kila mmoja akipata wastani wa watoto wanne, kumi na sita, jumla unakuwa na timu ya watu 20 kwenye familia bado ndugu na watoto wao ambao watakuwa wanakutegemea.​
Bado hujaweka dada wa kazi kwa kila mke. Chakula cha jioni tu kilo mbili za mchele kwa nyumba moja
 
Back
Top Bottom