Masoud Kipanya: Maisha plus ilipoteza mvuto baada ya kuingiza kina mama na mambo ya kilimo

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
x13395077_901064306687174_894571052_n-1.jpg.pagespeed.ic.JW4cWQFlT7.jpg


Mchoraji maarufu wa vibonzo na mtangazaji wa Clouds FM, Masoud Kipanya amekiri kuwa misimu miwili iliyopita ya shindano la Maisha Plus ilipoteza mvuto kutokana na kuwachanganya vijana na akina mama na pia kuingiza masuala ya kilimo.

Na sasa Masoud amedai kuwa msimu mpya ambao tayari umeanza usaili utarudisha ile Maisha Plus ya awali yenye burudani zaidi.

“Msimu wa tano unarudi kwa vijana peke yao, hakuna tena kina mama, wakulima wala nani hawahusiki. Sasa hivi ni vijana peke yao. Kwahiyo ule mchakamchaka, ile burudani ya nguvu ambayo vijana walikuwa wanaipata kupitia Maisha Plus ya kwanza nay a pili sasa watakuja kuipata tena katika msimu huu wa tano,” Masoud alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka.

Mwaka huu shindano litahusisha pia vijana kutoka Afrika Mashariki ambapo kutoka Tanzania watakuwa 14 na nchi zingine 16. Mshindi atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30.
 
Washiriki wawe na age ya 18 mpaka 26 dah kumbe kuanzia 27 + ni wazee
 
Washiriki wawe na age ya 18 mpaka 26 dah kumbe kuanzia 27 + ni wazee
27+ ni wazee aiseee.

Hata damu ishaacha kuchemka.

Ukifika umri huo unawaza kujenga familia tu, na sio kufanya mambo watu wakukubali.
 
Kumbe yupo clouds fm pia .... ila katika kitu kitakacho boa akiwaleta hao vijana 16 wa nchi zingine
 
Nafikiri kuusu rugha itakua ni kiswahili kwasababu mchezo/shindano hilo ni linahusisha nchi zinazozungumza lugha ya kiswahili... nadhan kiswahl ndo mpango mzma ili tukikuze vzur
 
Back
Top Bottom