Masoud Kipanya adai kupokea vitisho vya ujumbe kuwa anamuandama sana Rais Samia

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Masoud Kipanya akiwa anahojiwa na BBC amesema alipokea ujumbe kuwa anamuandama sana mama.

Masoud kupitia mahojiano na BBC amejitetea kuwa yeye hachori raisi bali anachora uraisi, na anapochora sio kuwa anamchukia huyo mtu. hivyo asichukuliwe vibaya.

Hili suala naona ni la ajabu kidogo hadi Sasa sijaona kwa nini viongozi na watu wanachukizwa na mawazo mbadala ya watu wengine.

Bado nashangaa unawezaje kuchukua katuni? Je ni kweli mama nae anachukia au ni watu wake tu ambao ni viherehere?

Wiki chache nyuma tuliona mchora katuni Opter Fwema akikamatwa kwa sababu ya katuni yake aliyomchora mama.

Je Ina maana hawa wachora katuni bawatakiwi kabisa kuchora uraisi? Au inabidi katuni zote zipitie kwanza huko ziwe edited ndio zifike kwa public?

Tuache haya mambo, kuna mengi ya kuconcentrate nayo kuliko hawa wachora katuni ambao hawana sana impact na katuni zao.

Screenshot_20211029-093956_1.jpg
 
Ni kawaida ya Ikulu ,hata aliyekuwa mpiga picha wa mchonga anadai aliwahi kumpiga picha mchonga pengo likaonekana na ikaprintiwa.

basi alipogundua hivo alikaa kwa hofu akijua muda wowote atawakiwa na Ikulu
 
Msanii Oppter Fwema anaendelea na kesi yake mahakamani inayotokana na walioutafsiri mchoro wake kuwa amemchora Rais.

Nadhani sisi wasanii sasa ni wakati wetu kukaa mguu sawa kwa gwaride la kuelekea korokoroni.

Wakitumaliza sisi, watakuja wengine ambao ni mahiri kuliko sisi.
 
Msanii Oppter Fwema anaendelea na kesi yake mahakamani inayotokana na walioutafsiri mchoro wake kuwa amemchora Rais.

Nadhani sisi wasanii sasa ni wakati wetu kukaa mguu sawa kwa gwaride la kuelekea korokoroni.

Wakitumaliza sisi, watakuja wengine ambao ni mahiri kuliko sisi
Inapaswa kupigwa vita Mara moja hii tabia
 
Msanii Oppter Fwema anaendelea na kesi yake mahakamani inayotokana na walioutafsiri mchoro wake kuwa amemchora Rais.

Nadhani sisi wasanii sasa ni wakati wetu kukaa mguu sawa kwa gwaride la kuelekea korokoroni.

Wakitumaliza sisi, watakuja wengine ambao ni mahiri kuliko sisi
katuni.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom