Masomo ya Civics, Kiswahili na Historia yaondelewe yawekwe ya Kilimo, Ufugaji na Ufundi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,904
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Masomo ya O level kama Kiswahili, Civics na Historia yanapoteza tu muda watoto.

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na raslimali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaji vito vya madini,madini tunayo nk ili mtoto akimaliza Form Four awe tayari kukabiliana maisha.
 
Yasiondolewe ila yaongezwe,mwanafunzi achague mwenywe nini anataka kusoma,,,, lakinu hofu yangu kichwa kimoja mambo mengi kitamudu kweli
Yatakuwa mengi mno yataumiza mtoto kichwa hayo yasukumiwe kidato Cha tano mtu akiyataka akasome kidato Cha tano akaanzie huko huko na kuyamalizia huko yawe choice huko
 
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Misomo ya O level Kama kiswahili, Civics na historia yanapotezaa tu muda watoto

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na rasmali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaj viito madini tunayo nk ili mtoto akimaliza form four awe tayari kukabiliana maisha.
Somo la History na Civics ndo naona la kuunganishwa linakuwa 'History and Civic Education'

Agriculture iwe lazima kama Bios
 
Shule za zamani zilikua na shamba la shule, banda la kuku, ng'ombe na viwanja vya michezo, kuanzia utawala wa awamu ya pili hivi vitu vilianzakufutika kimoja baada ya kingine.

Somo la civics ni zuri ila nashangaa mpaka leo kwanini somo hili lisiitwe URAIA na lifundishwe ka lugha ya kiswahili shule za msingi na secondary.
 
Kuna mambo mengi Sana yanatakiwa yawekwe sawa kwenye elimu yetu kwa sasa, ila somo la Agriculture lilitakiwa litiliwe mkazo Sana mana ndani yake Kuna mambo mengi hasa zile branch zake zote.
 
Shule za zamani zilikua na shamba la shule, banda la kuku, ng'ombe na viwanja vya michezo, kuanzia utawala wa awamu ya pili hivi vitu vilianzakufutika kimoja baada ya kingine.

Somo la civics ni zuri ila nashangaa mpaka leo kwanini somo hili lisiitwe URAIA na lifundishwe ka lugha ya kiswahili shule za msingi na secondary.
uko sahihi mkuu,leo hii kupalilia kashamba ka mwalimu inaonekana ni dhambi kubwa. tunaharibu kizazi. sisi tulikuwa tunalima mpaka mashamba pamba ya kijiji. tukimaliza tunaanza ya walimu
 
Hii si iligeuzwa kuwa miradi ya walimu, wanafunzi wanahrnyeshwa hadi wanakosa muda wa kusoma halafu vitu vyenyewe wanakula walimu

Halafu ufugaji wenyewe ulikua wa kawaida tu haukuwa na utaalam wowote, hauwajengi wanafunzi kuwa wataalamu wa kilimo
 
Unashauri somo la Lugha inayotambulisha Taifa na Utamaduni wa Mtanzania iondolewe. Pia somo linalohusu maisha ya kila siku ya jamii yetu civics liondolewe???

Fikiri kwa mara ya pili.
Elimu inatakiwa isaidie mtoto kupambana na mazingira kwa kutumia raslimali zilizopo

Misomo ya O level Kama kiswahili, Civics na historia yanapotezaa tu muda watoto

Yawekwe masomo ya kilimo na ufugaji kuanzia wa wanyama, ndege, samaki na some la ufundi wa kutengeneza vitu kutokana na rasmali zetu kama kutengeneza viatu vya ngozi, ushonaji pamba tunayo, useremala miti tunayo, ugundi wa kupika vyakula mbalimbali kama chapati mazao tunayo nk utengenezaj viito madini tunayo nk ili mtoto akimaliza form four awe tayari kukabiliana maisha.
 
uko sahihi mkuu,leo hii kupalilia kashamba ka mwalimu inaonekana ni dhambi kubwa. tunaharibu kizazi. sisi tulikuwa tunalima mpaka mashamba pamba ya kijiji. tukimaliza tunaanza ya walimu
Kwani ishu tunayokabiliana nayo ni watu kulima au watu kulima kitaalamu na kuongezea tija?

Maana Kama ni kulima watu wanalima sana, Ila umasikini kwao ndio umekolea

Hayo mashamba ya shule na Kijiji si walikuwa wakilima kienyeji na uzalishaji unakuwa duni uleule? Sasa faida ya kuwalimisha watoto wetu ni Nini?

Hizo nchi ambazo hawana hata ardhi ya kutosha Ila wanalima hadi wanatoa msaada Tanzania enzi zile za Nyerere za mashamba ya Kijiji, walikuwa wakilimisha watoto?
 
Hayo masomo unayoyasemea yapo.Jaribu kupitia ratiba za Necta za form IV utayakuta.
Ulivyopendekeza Kiswahili kiondelewe sijui nimekufikiriaje yaani.Ungetuletea Case study ya nchi yoyote ile duniani isiyofundisha lugha yake mashuleni.Nchi za SADC zinaanza kufundisha kiswahili mashuleni halafu eti tukiteme.Sasa hata hao walimu wakufundisha kiswahili nchi zingine watatoka wapi? Au tunawaachia Kenya!!! Hili ni boko.
Pia elimu ya uraia haiwezi kuondolewa kwa namna yoyote ile.Umetoa boko tena hapa.
At least history naweza kukufikiria.Ila hayo mengine juu hata mjadala hayahitaji.
Kwa tathmini yangu juu yako, unahisi labda elimu inatakiwa imsaidie mwanafunzi baadaye kuvuta mkwanja tu,unakosea.Skills za maisha unazofundishwa kwenye uraia huna,hata msingi mzuri utakosa.
 
Back
Top Bottom